Ibaada kwa Lugha Yangu
×




JUMATATU YA ROHO MTAKATIFU BAADA YA JUMAPILI YA PENTEKOSTE

KATIKA JUMAPILI YA PENTEKOSTE TAKATIFU,

KASISI

Ahimidiwe Mungu wetu daima, sasa na siku zote, hata milele na milele.

MSOMAJI

Amina. Njooni, tumwinamie na tumsujudu Mungu wetu.

Njooni, tumwinamie na tumsujudu Kristo yu Mungu Mfalme wetu.

Njooni, tumwinamie na tumsujudu yeye Kristo, aliye mfalme na Mungu wetu.

Zaburi 103 (104 katika Union Version)

Ee nafsi yangu, umhimidi BWANA. Wewe, BWANA, Mungu wangu, Umejifanya mkuu sana; Umejivika heshima na utukufu. Umejivika nuru kama vazi; Umezitandika mbingu kama pazia; Na kuziweka nguzo za ghorofa zake majini. Huyafanya mawingu kuwa gari lake, Na kwenda juu ya mabawa ya upepo, Huwafanya malaika zake kuwa pepo, Na watumishi wake kuwa moto wa miali. Uliiweka nchi juu ya misingi yake, Isitikisike milele. Uliifunika kwa vilindi kama kwa vazi, Maji yalikuwa yakisimama juu ya milima. Kwa kukemea kwako yakakimbia, Kwa sauti ya radi yako yakaenda zake kasi, Yakapanda milima, yakateremka mabondeni, Mpaka mahali ulipoyatengenezea. Umeweka mpaka yasiupite, Wala yasirudi kuifunikiza nchi. Hupeleka chemchemi katika mabonde; Zapita kati ya milima; Zamnywesha kila mnyama wa porini; Kwayo punda mwitu huzima kiu yao. Kandokando hukaa ndege wa angani; Na kuimba wakiwa katika matawi. Huinywesha milima toka juu angani; Nchi umeitosheleza kwa mazao ya kazi zako. Huyameesha majani kwa makundi, Na maboga kwa matumizi ya mwanadamu; Ili atoe chakula katika nchi, Na divai imfurahishe mtu moyo wake. Aung'aze uso wake kwa mafuta, Na mkate umburudishe mtu moyo wake. Miti ya BWANA nayo imetoshelezwa maji, Mierezi ya Lebanoni aliyoipanda. Humo ndege hujenga viota vyao, Korongo, anayo makao katika misonobari. Milima mirefu ndiko waliko mbuzi wa mwitu, Na magenge ni kimbilio lao wibari. Aliufanya mwezi kwa ajili ya nyakati, Jua latambua kuchwa kwake. Wewe hufanya giza, kukawa usiku, Ndipo atambaapo kila mnyama wa mwitu. Wanasimba hunguruma wakitaka mawindo, Wakitafuta chakula chao kutoka kwa Mungu. Jua linapochomoza, wanakwenda zao, Na kujilaza mapangoni mwao. Mwanadamu atoka kwenda zake kazini, Na kwenye utumishi wake mpaka jioni. Ee BWANA, jinsi yalivyo mengi matendo yako! Kwa hekima umevifanya vyote pia. Dunia imejaa viumbe wako. Bahari iko kule, kubwa na upana, Ndimo mlimo viendavyo visivyohesabika, Viumbe hai wakubwa kwa wadogo. Ndimo zipitamo merikebu, Ndimo alimo Lewiathani uliyemwumba acheze humo. Hao wote wanakungoja Wewe, Uwape chakula chao kwa wakati wake. Wewe huwapa, Wao wanakiokota; Wewe waukunjua mkono wako, Wao wanashiba mema; Wewe wauficha uso wako, Wao wanafadhaika; Waiondoa pumzi yao, wanakufa, Na kuyarudia mavumbi yao, Waituma roho yako, wanaumbwa, Nawe waufanya upya uso wa nchi. Utukufu wa BWANA na udumu milele; BWANA na ayafurahie matendo yake. Aitazamaye nchi, ikatetemeka; Aigusaye milima, ikatoka moshi. Nitamwimbia BWANA maadamu ninaishi; Nitamshangilia Mungu wangu nikiwa hai; Kutafakari kwangu na kuwe kutamu kwake; Maana furaha yangu hutoka kwa BWANA. Wenye dhambi waangamizwe katika nchi, Watendao ubaya wasiwepo tena. Ee nafsi yangu, umhimidi BWANA.

Jua latambua kuchwa kwake. Wewe hufanya giza, kukawa usiku.

Ee BWANA, jinsi yalivyo mengi matendo yako! Kwa hekima umevifanya vyote pia. [Biblia "Union Version"]

Utukufu kwa Baba na Mwana na Roho Mtakatifu. Sasa na siku zote hata milele na milele. Amina.

Aleluya, Aleluya, Aleluya. Utukufu kwako, Ee Mungu. (3)

Utukufu kwako, Mungu matumaini yetu, utukufu kwako.

KASISI (kwa mnong'ono)

Ombi la kwanza.

Ee Bwana wa neema na rehema, mvumilivu na mwenye huruma nyingi uisikilize sala yetu uisikilize sauti za maombi yetu ya kusihi. Utufanyie ishara ya wema wako.Utufundishe njia yako ili tuenende katika ukweli wako. Changamsha mioyo yetu ili tuweze kuliheshimu jina lako takatifu, kwa kuwa wewe ndiwe mkuu na wewe ndiwe mfanya miujiza. Wewe ndiwe Mungu na katikati ya miungu hakuna kama wewe Bwana, mwenye nguvu na huruma, mwenye neema na fadhili za kusaidia kuhifadhi, na kuokoa wote wanaoamini jina lako adhimu. [PROPOSED TEXT]

Kwa maana utukufu wote, heshima na uabudu ni haki yako, Baba, Mwana na Roho Mtakatifu, sasa na siku zote na milele na milele. [NAIROBI] Amina.

Ombi la pili.

Usitulaumu katika ghadhabu yako, Ee Bwana Usituadhibu kwa ukali wa hasira yako lakini kama zilivyo rehema zako, ututendee sisi kwa ukarimu wako, Ee mganga na mponyaji wa roho zetu ili tufahamu maarifa au hekima ya ukweli wako. Kidhie, kwamba siku hii, na siku zote za maisha yetu zinazobaki ziwe kwa amani bila dhambi, kwa maombi ya mzazi Mungu na watakatifu wote. [PROPOSED TEXT]

Kwa kuwa utawala ni wako na ufalme, uweza na utukufu ni vyako, Baba, Mwana na Roho Mtakatifu, sasa na siku zote, hata milele na milele. [GB] Amina.

Ombi la tatu

Ee Bwana Mungu wetu, utukumbuke sisi watumwa wako wenye dhambi na wasiofaa mbele zako, tunapoliita jina lako adhimu na linaloheshimiwa. Usitufadhaishe tutarajiapo huruma zako; lakini tutimizie maombi yetu ya kusihi wokovu na utustahilishe, Ee Bwana kukupenda na kukuogopa wewe na mioyo yetu yote, ili tutende vitu vyote kulingana na mapenzi yako. [PROPOSED TEXT]

Kwa kuwa wewe u Mungu mwema na mpenda wanadamu, na kwako tunatoa utukufu kwa Baba na Mwana na Roho Mtakatifu. Sasa na siku zote hata milele na milele. [PROPOSED TEXT] Amina.

Ombi la nne

Ee Bwana unayeadhimishwa kwa nguvu takatifu kwa nyimbo mfulilizo zisizo na mwisho, ujaze vinywa vyetu na utukufu wako ili tuliinue jina lako takatifu na utuunganishe nao wakuogopao kwa kutenda na kulinda ukweli na amri zako.Kwa maombi ya mzazi Mungu mtakatifu na watakatifu wote; [PROPOSED TEXT]

Kwa kuwa Jina lako linahimidiwa na ufalme wako unatukuzwa, wa Baba na Mwana na Roho Mtakatifu, sasa na siku zote, hata milele na milele. [PROPOSED TEXT] Amina.

Ombi la Tano

Ee Bwana, Ee Bwana ushikaye vitu vyote katika kiganja chako kisicho na doa, mvumilivu pamoja sisi sote na unayehuzunika na kubadirsha maamuzi kwa maovu yetu, kumbuka rehema zako na huruma zako, utembelee na ukarimu wako,; na utujalie tuepuke usiku huu wote katika mawazo mabaya ya muovu na tunza maisha yetu bila shambulio lolote kwa rehema ya roho yako takatifu kamili. [PROPOSED TEXT]

Na huruma na upendo kwa mwanadamu wa Mwana wako wa pekee, pamoja naye unahimidiwa, pamoja na utakatifu wote na Roho mwema na mpaji wa uhai, sasa na siku zote hata milele na milele. [PROPOSED TEXT] Amina.

Ombi la sita

Ee Mungu, mtukufu wa ajabu, unaye ongoza ulimwengu na wema wako usio erezeka na ulinzi tele, uliye tupatia mema yote ya dunia na uliye turidhia ufalme ulio tuahidi kwa mema yaote ulio tujalia; wewe uliye tuwezesha kwenda mbali na maovu kwa kipindi cha siku kilichopita, utujalie tuwe bila dhambi kwa wakati uliosalia mbele ya utukufu wako mtakatifu, tukutuze Mungu wetu pekee mwema na mpenda wanadamu. [PROPOSED TEXT]

Kwa kuwa U mungu wetu na Kwako tunatoa utukufu, kwa Baba na Mwana na Roho Mtakatifu, sasa na siku zote, hata milele na milele. [PROPOSED TEXT] Amina.

Ombi la saba

Ee Mungu mtukufu na uliye huu, uliye pekee asiyekufa, unayeishi kwa mwanga usiyofikika; uliyeumba vitu vyote kwa hekima ; uliye gawanya mwanga na giza nakuweka jua kutawala mchana, na mwezi na nyota kutawala usiku; uliyetujalia sisi wenye dhambi kufikia uso wako wakati huu katika kutubu na kukutolea shukrani za maombi ya jioni; wee, Bwana mpenda wanadamu, elekeza maombi yetu yapae kwako kama uvumba na yakubali kama manukato ya kupendeza. Na jioni hii na usiku ujao uwe wa amani, utuvike siraha ya mwanga; utuokoe kutoka kila ogofya la siku na kutoka kila kinacho tembea gizani. na utupatie usingizi, ulio tujalia kupumzishakutoka magojwa yetu, tuwe huru kutoka mawazo maovu.Ndiyo, Ee Bwana mutawala, wa vitu vyote unaye tujaliaa mema, ili, tunapolla vitandani mwetu tukumbuke jina lako wakati wa usiku, na tukiwa tumeangazwa na amri zako, tuamke na kukutukuza wema na roho ya furaha, kwa kutoa sala na maombi kwa upendo wako kwa ajili ya dhambi zetu na kwa ajili ya watu wako, watu ambao unawatembelea kwa rehema, kwa utetezi wa mtakatifu Mzazi Mungu [PROPOSED TEXT]

Kwa kuwa wewe u Mungu mwema na mpenda wanadamu, na kwako tunatoa utukufu kwa Baba na Mwana na Roho Mtakatifu. Sasa na siku zote hata milele na milele. [PROPOSED TEXT] Amina.

Irinika (Litania Kubwa ya Amani)

SHEMASI:

Kwa amani tumwombe Bwana.

Watu

Bwana hurumia.

SHEMASI:

Kwa ajili ya amani kutoka juu na ya wokovu wa roho zetu, tumwombe Bwana.

Watu

Bwana hurumia.

SHEMASI:

Kwa ajili ya amani ya dunia yote na kusimama imara kwa Makanisa Matakatifu ya Mungu, na umoja wa wote, tumwombe Bwana.

Watu

Bwana hurumia.

SHEMASI:

Kwa ajili ya nyumba hii takatifu na wanaoingia humu kwa imani, heshima na kumcha Mungu, tumwombe Bwana.

Watu

Bwana hurumia.

SHEMASI:

Kwa ajili ya Wakristo Waorthodoksi wanaomcha Mungu, tumwombe Bwana.

Watu

Bwana hurumia.

SHEMASI:

Kwa ajili ya Askofu wetu mkuu (jina), mapadri waheshimiwa, mashemasi katika Kristo, wateule na watu wote, tumwombe Bwana.

Watu

Bwana hurumia.

SHEMASI:

Kwa ajili ya Taifa letu linalomcha Mungu, utawala na mamlaka yote ya nchi yetu, viongozi na majeshi yetu yanayompenda Kristo, tumwombe Bwana.

Watu

Bwana hurumia.

SHEMASI:

Kwa ajili ya mji huu na miji yote na nchi zote na waishimo kwa imani, tumwombe Bwana.

Watu

Bwana hurumia.

Kwa ajili ya majira mema ya mwaka, kupata mvua ya kutosha, hewa safi, rutuba ya kutosha kwa ardhi, na mazao ya kutosha tumwombe Bwana.

Watu

Bwana hurumia.

Kwa ajili ya wanaosafiri angani, baharini na nchi kavu, na kwa ajili ya wagonjwa, wanaolemewa, mateka na kwa wokovu wao, tumwombe Bwana.

Watu

SHEMASI:

Kwa ajili ya wote walio hapa, wakingoja neema ya Roho Mtakatifu, tumwombe Bwana.

Watu

Bwana hurumia.

SHEMASI:

Kwa ajili ya wote waelekezao nafsi zao na magoti yao mbele za Bwana, tumwombe Bwana.

Watu

Bwana hurumia.

SHEMASI:

Ili tuweze kutiwa nguvu katika kutimiza kazi zinazompendeza Bwana, Tumwombe Bwana.

Watu

Bwana hurumia.

SHEMASI:

Ili atuteremshie utajiri wa rehema Zake.

Watu

Bwana hurumia.

SHEMASI:

li akubali kupiga magoti kwetu, kuwe kama uvumba mbele Yake.

Watu

Bwana hurumia.

SHEMASI:

Kwa wale wote wanaohitaji msaada wake, tumwombe Bwana.

Watu

Bwana hurumia.

SHEMASI:

Kwa ajili ya kuokolewa kwa kila sikitiko, ghadhabu, hatari na uhitaji, tumwombe Bwana.

Watu

Bwana hurumia.

SHEMASI:

Utusaidie, utuokoe, utuhurumie, na utuhifadhi, Ee Mungu, kwa neema yako.

Watu

Bwana hurumia.

SHEMASI:

Tumemkumbuka Maria Mtakatifu kamili, asiye na doa, mbarikiwa zaidi kushinda wote, Mama yetu mtukufu, Mzazi-Mungu na Bikira daima, pamoja na watakatifu wote, tujiweke sisi wenyewe na kila mmoja wetu na wenzetu wote na maisha yetu yote mikononi mwa Kristo Mungu.

Watu Kwako. Ee Bwana.

Ahimidiwe Mungu wetu daima, sasa na siku zote, hata milele na milele.

WATU

Ee Bwana, nimekuita, unijie hima, unijie hima, Bwana. Ee Bwana, nimekuita, unijie hima, uisikie sauti ya kilio changu, uisikie sauti yangu nikuitapo, Bwana. [PROPOSED TEXT]

Sala yangu ipae mbele zako kama uvumba, Kuinuliwa mikono yangu kama dhabihu ya jioni. unijie hima Bwana [Biblia "Union Version"]

Ee BWANA, uweke mlinzi kinywani pangu, Mngojezi mlangoni pa midomo yangu.

Usiuelekeze moyo wangu kunako jambo baya, Nisiyazoelee matendo yasiyofaa,

Pamoja na watu watendao maovu; Wala nisile vyakula vyao vya anasa.

Mwenye haki na anipige, itakuwa fadhili; Anikemee, itakuwa kama mafuta kichwani; Kichwa changu kisikatae,

Maana siachi kusali kati ya mabaya yao. Wakuu wao wakiangushwa kando ya genge,

Watayasikia maneno yangu, maana ni matamu. Kama kupasua kuni na kuzichanja juu ya nchi, Ndivyo ilivyo mifupa yetu mdomoni pa kuzimu.

Macho yangu yanakuelekea Wewe, MUNGU Bwana, Nimekukimbilia Wewe, usiniache bila kinga.

Unilinde kutoka kwa mtego walionitegea, Na kutoka kwa matanzi ya watendao maovu.

Wabaya na waanguke katika nyavu zao wenyewe, Wakati ninapopita salama.

Kwa sauti yangu nitamlilia BWANA, Kwa sauti yangu nitamwomba BWANA dua.

Nitafunua mbele zake malalamiko yangu, Shida yangu nitaitangaza mbele zake.

Roho yangu inapozimia unayajua mapito yangu;

Katika njia niendayo wamenifichia mtego.

Utazame mkono wangu wa kulia ukaone, Kwa maana sina mtu anijuaye.

Makimbilio yamenipotea, Hakuna wa kunitunza roho.

BWANA, nimekuita nikasema, Ndiwe kimbilio langu, Fungu langu katika nchi ya walio hai.

Ukisikilize kilio changu, Kwa maana nimedhilika sana.

Uniponye kutoka kwa wanaonifuatia, Kwa maana wao ni hodari kuliko mimi.

Uitoe nafsi yangu kifungoni. Nipate kulishukuru jina lako.

Wenye haki watanizunguka, Kwa kuwa Wewe unanikirimu.

Ee BWANA, toka vilindini nimekulilia. Bwana, uisikie sauti yangu.

Masikio yako na yaisikilize Sauti ya dua zangu.


BWANA, kama Wewe ungehesabu maovu, Ee Bwana, nani angesimama? Lakini kwako kuna msamaha, Ili Wewe uogopwe. [Biblia "Union Version"]

Mataifa mengi yaliona mambo ya ajabu katika mji wa Daudi wakati Roho Mtakatifu alishuka katika ndimi za moto kama vile Luka mvuviwa alivyosimulia. Kwa maana anasema: "Walikuwa wote pamoja mahali pamoja. Ghafla ikasikika sauti kama ya uvumi wa upepo mkali ukivuma kasi, ikajaza nyumba yote waliyokuwa wameketi. Wote wakaanza kusema kwa lugha nyingine, na mafundisho mengine. mafundisho ya Roho Mtakatifu.” [NAIROBI]

Nimemngoja BWANA, roho yangu imengoja, Na neno lake nimelitumainia. Nafsi yangu inamngoja Bwana, [Biblia "Union Version"]

Mataifa mengi yaliona mambo ya ajabu katika mji wa Daudi wakati Roho Mtakatifu alishuka katika ndimi za moto kama vile Luka mvuviwa alivyosimulia. Kwa maana anasema: "Walikuwa wote pamoja mahali pamoja. Ghafla ikasikika sauti kama ya uvumi wa upepo mkali ukivuma kasi, ikajaza nyumba yote waliyokuwa wameketi. Wote wakaanza kusema kwa lugha nyingine, na mafundisho mengine. mafundisho ya Roho Mtakatifu.” [NAIROBI]

Kuliko walinzi waingojavyo asubuhi, Naam, walinzi waingojao asubuhi. [Biblia "Union Version"]

Roho Mtakatifu amekuwako siku zote, yuko sasa na atakua milele, bila mwanzo wala mwisho, ila mmoja na Baba na Mwana: uhai na mpaji wa uhai; wema wenyewe na chanzo cha wema, Ambaye kwa njia yake Baba anatambulishwa na Mwana anatukuzwa, na anajulikana na wote: nguvu moja, umoja mmoja, uabudu mmoja, wa Utatu Mtakatifu. [NAIROBI]

Ee Israeli, umtarajie BWANA; Maana kwa BWANA kuna fadhili, Na kwake kuna ukombozi mwingi. Yeye atamkomboa Israeli na maovu yake yote. [Biblia "Union Version"]

Roho Mtakatifu amekuwako siku zote, yuko sasa na atakua milele, bila mwanzo wala mwisho, ila mmoja na Baba na Mwana: uhai na mpaji wa uhai; wema wenyewe na chanzo cha wema, Ambaye kwa njia yake Baba anatambulishwa na Mwana anatukuzwa, na anajulikana na wote: nguvu moja, umoja mmoja, uabudu mmoja, wa Utatu Mtakatifu. [NAIROBI]

Enyi mataifa yote, msifuni BWANA, Enyi watu wote, mhimidini. [Biblia "Union Version"]

Roho Mtakatifu, nuru na uzima, na chemchemi ya akili iliyo hai. Roho wa hekima, Roho wa ufahamu, wa wema na uaminifu, ujuzi na ukuu, afutaye dhambi. Mungu anayefanya uungu; moto utokanao na moto, anenaye, atendaye, akitwaa zawadi; Ambaye kupitia kwake manabii wote na mitume wa Mungu pamoja na mashahidi walipewa taji. Sauti tofauti, mtazamo tofauti: moto ukigawanyika kuwa zawadi za neema. [NAIROBI]

Maana fadhili zake kwetu sisi ni kuu, Na uaminifu wa BWANA ni wa milele. [Biblia "Union Version"]

Roho Mtakatifu, nuru na uzima, na chemchemi ya akili iliyo hai. Roho wa hekima, Roho wa ufahamu, wa wema na uaminifu, ujuzi na ukuu, afutaye dhambi. Mungu anayefanya uungu; moto utokanao na moto, anenaye, atendaye, akitwaa zawadi; Ambaye kupitia kwake manabii wote na mitume wa Mungu pamoja na mashahidi walipewa taji. Sauti tofauti, mtazamo tofauti: moto ukigawanyika kuwa zawadi za neema. [NAIROBI]

Utukufu kwa Baba na Mwana na Roho Mtakatifu, sasa na siku zote hata milele na milele. Amina.

Ee mfalme wa mbiguni, Mfariji, Roho wa kweli; uliye mahali popote, na kuvijaza vitu vyote; wewe ni hazina ya mambo mema na mpaji wa uhai; njoo ukae kwetu na kutusafisha na kila doa, hata uziokoe roho zetu, Mwema we. [NAIROBI]

SHEMASI:

Tumwombe Bwana.

KASISI

Jioni, asubuhi na adhuhuri twakusifu, twakuhimidi, twakushukuru na twakuomba, Ee Rabi wa wote, Bwana mpenda wanadamu. Elekeza maombi yetu mbele zako kama uvumba, na mioyo yetu isipotoshwe kwenye maneno namafikira maovu, utuokoe kwa kila jaribio rohoni mwetu; kwa kuwa macho yetu yaelekea kwako ewe Bwana na tumekukimbilia wewe, usituambishe, Ee Mungu wetu,

Kwa maana utukufu wote, heshima na uabudu ni haki yako, Baba, Mwana na Roho Mtakatifu, sasa na siku zote na milele na milele.

SHEMASI:

Ee padri, bariki kuingia kutakatifu.

KASISI

Kubarikiwe kuingia kwa patakatifu pako, daima sasa na siku zote, hata milele na milele.

SHEMASI:

Amina.

Hekima! Simameni wima!

We Nuru ya furaha ya utukufu mtakatifu, ya Baba usiyekufa, wa mbinguni, mtakatifu, mhimidiwa, Yesu Kristo! Tukiwa tumefika wakati wa kuchwa kwa jua na kuona mwanga wa jioni tunamwimbia Baba, Mwana na Roho Mtakatifu Mungu. Ni wajibu wakati wote usifiwe kwa sauti safi, Ee Mwana wa Mungu, mpaji wa uhai; kwa hivyo dunia ya kutukuza. [[SWA]]

Prokimeno. Sauti ya 7

Ni Mungu yupi aliye mkuu kama Mungu wetu? Wewe ndiwe Mungu ufanyaye maajabu; [Biblia "Union Version"]

Mstari: Uliudhihirisha uweza wako kati ya mataifa.

Ni Mungu yupi aliye mkuu kama Mungu wetu? Wewe ndiwe Mungu ufanyaye maajabu;

Mstari: Nikasema, Ndio udhaifu wangu huo; Lakini nitaikumbuka miaka ya mkono wa kulia wake Aliye Juu.

Ni Mungu yupi aliye mkuu kama Mungu wetu? Wewe ndiwe Mungu ufanyaye maajabu;

Mstari: Nitayakumbuka matendo ya BWANA; Naam, nitayakumbuka maajabu yako ya kale.

Ni Mungu yupi aliye mkuu kama Mungu wetu? Wewe ndiwe Mungu ufanyaye maajabu;

SHEMASI:

Tena, kwa kupiga magoti, tumwombe Bwana.

Watu Bwana hurumia.

KASISI

Ee Bwana msafi sana, usiye na doa, uliyepo tangu milele, usiyeonekana, Mtakatifu usiyechunguzika, usiyebadirika, usiyeshindwa, usiyepimika, mvumilivu; wewe pekee utukuzwe, ukaaye kwenye mwanga usiofikika; uliyefanya mbingu, na nchi, na bahari, na vyote vilivyomo; uwaponye watu wote mahitaji yao kabla hawajaomba; tunakuomba, tunakusihi, Ee mpenda wanadamu, Baba wa Bwana wetu na Mungu na Mwokozi wetu Yesu Kristo, aliyeshuka toka mbinguni kwa ajili yetu wanadamu, na kwa ajili ya wokovu wetu, kupitia kwa Roho Mtakatifu, na kupitia kwa Maria Bikira daima, Mheshimiwa sana, Mzazi Mungu; ambaye kwanza alifundisha kwa maneno, na ambaye alijionyesha kwa matendo, alipotumia maumivu ya ukombozi, aliyetafuta wanyenyekevu wako na wenye dhambi na watumishi wasiostahili, ya kwamba tutoe maombi kwako, tukiinamisha shingo na magoti yote, kwa ajili ya dhambi zetu wenyewe na kwa kutojua kwa watu.

Wewe Mungu, mwenye rehema na mpenda wanadamu, utusikie siku ile tutakapokuita; na hasa siku ya leo ya Pentekoste, ambapo baadaye Bwana wetu Yesu Kristo alipanda juu mbinguni, na kukaa kuume kwako, uliye Mungu wake na Baba yake, alituma Roho wake Mtakatifu juu ya wanafunzi wake watukufu na mitume; aliyewakalia juu ya kila mmoja wao na ambapo walijazwa rehema zako zisizoisha, na kutangaza ukuu wako kwa namna ya lugha mbalimbali, na kutabiri.

Hivyo, tusikie sisi tunaokuomba, na utukumbuke sisi wanyenyekevu na tunaoshutumiwa, na utuhurumie kama tulivyo, na ugeuze roho zetu zilizotekwa, tukijizoesha wema wako kwetu, tutoao maombi kwako sasa. Tukubali sisi tunaoanguka mbele yako, na kupaza sauti kwako: Tumefanya dhambi! Tumejitenga nawe toka kwenye matumbo ya mama zetu; Wewe ni Mungu wetu, lakini kwa kuwa tumepoteza siku zetu bure, tumetapanya msaada wako. Lakini kwa uhakika wa rehema zako, tunakuomba; usikumbuke dhambi za ujana na kutojua kwetu, na utusafishe na dhambi zote za siri. Usitutenge siku za uzee wetu, wakati nguvu zetu zitakapotuishia; tena tutakaporudi kwako usitukatae, tujalie neema tuweze kukimbilia kwako na kupokelewa kwa sababu ya neema na upendeleo wako.

Pima udhaifu wetu kulingana na kipimo cha wingi wa rehema zako; kwa wingi wa rehema zako tuondolee makosa yetu. Tazama chini toka juu kwenye utukufu wako, Ee Bwana, juu ya watu wako wale walioko hapa, ambao wanapokea utajiri wa huruma wanayopokea kutoka kwako; ututembelee katika wema wako, utuondolee kila mtego wa shetani; ongoza maisha yetu kwenye amri zako takatifu na kuu. Wape watu wako malaika, walinzi waaminifu; tukusanye sisi sote kwenye ufalme wako; wape msamaha watu waaminio kwako; wasamehe dhambi wao pamoja nasi; tutakase kwa kushirikiana na Roho wako Mtakatifu; batilisha hila zote za adui kwetu. [ARUSHA]

Umehimidiwa, Bwana, Bwana Mwenyezi, kwa kuwa unamulikia mchana kwa mwanga wa jua na kuangaza usiku kwa miale ya moto. Ulituwezesha kupitisha muda wa mchana na kwa hivyo tukafika mwanzo wa usiku. Sikia maombi yetu na ya watu Wako wote, na utusamehe dhambi zetu zote za kujua na za kutojua; pokea maombi yetu ya jioni na utume wingi wa rehema na huruma Yako juu ya urithi Wako.

Tuzungukie na Malaika Wako watakatifu; tuvike silaha za haki yako; Utuimarishe ndani ya ukweli wako; fanya nguvu zako kuwa ngome yetu, utuepushe na hali zote mbaya na mashambulio yote ya adui. Mwishowe, tukidhie kwamba jioni hii, na usiku unaokuja, uwe mkamilifu, mtakatifu, wa amani, usio na dhambi, usio na maono sumbufu, na siku zote za maisha yetu, kupitia maombi ya Mzazi Mungu Mtakatifu na ya Watakatifu wote ambao wamekupendeza tangu zamani. [NAIROBI]

SHEMASI:

Utusaidie, utuokoe, tuhurumie, utuinue na utuhifadhi, Ee Mungu, kwa neema yako.

Watu: Bwana hurumia.

SHEMASI:

Tumemkumbuka Maria Mtakatifu kamili, asiye na doa, mbarikiwa zaidi kushinda wote, Mama yetu mtukufu, Mzazi-Mungu na Bikira daima, pamoja na watakatifu wote, tujiweke sisi wenyewe na kila mmoja wetu na wenzetu wote na maisha yetu yote mikononi mwa Kristo Mungu.

Watu: Kwako. Ee Bwana.

KASISI

Kwa kuwa kutuhurumia na kutuokoa ni kwako, Ee Mungu wetu, na kwako tunatoa utukufu, Baba na Mwana na Roho Mtakatifu, sasa na siku zote, hata milele na milele.

Watu: Amina.

SHEMASI:

Tuseme sisi sote kwa roho yetu na kwa mawazo yetu yote tuseme hivi.

WATU

Bwana hurumia.

SHEMASI:

Ee Bwana, Mwenyezi Mungu wa mababa wetu tunakuomba utusikilize na kutuhurumia.

SHEMASI:

Utuhurumie Ee Mungu kadiri ya huruma yako kubwa tunakuomba utusikie na kutuhurumia.

WATU

Bwana hurumia. (3)

SHEMASI:

Tena tunaomba kwa ajili ya Askofu wetu mkuu (jina)

WATU

Bwana hurumia. (3)

SHEMASI:

Tena tunaomba kwa ajili ya Taifa letu, utawala na mamlaka yote ndani lake.

Tena tunaomba kwa ajili ya neema, uzima, amani, afya, wokovu na msamaha wa dhambi za watumishi wa Mungu, wote wanaomcha Mungu, Wakristo Waorthodoksi wanaokaa katika mji hii, na ndugu wanaofanya kazi katika Kanisa hili.

Tena tunaomba kwa ajili ya warehemiwa wajengaji wa nyumba hii takatifu, ambao tunawakumbuka, hata ya baba na ndugu zetu wote Waothodoksi warehemiwa, ambao wamelala hapa na mahali popote.

Tena tunaomba kwa ajili yao wanaotenda matendo mema katika nyumba hii takatifu na heshimiwa, kwa ajili yao wenye juhudi, wanaoimba hata ya watu wote waliosimama hapa, wakingoja huruma yako kubwa na ya utajiri.

KASISI

Kwa kuwa wewe ndiwe Mungu mrahimu na mpenda-wanadamu; na kwako tunatoa utukufu, kwa Baba, na Mwana, na Roho Makatifu, sasa na sikuzote, hata milele na milele.

WATU

Amina.

SHEMASI:

Tena, kwa kupiga magoti, tumwombe Bwana.

Watu Bwana hurumia.

KASISI

Ee Bwana Yesu Kristo, Mungu wetu, uliyewapa amani watu wako, na kipawa cha Roho wako Mtakatifu ambaye, wakati ule ulipokuwa bado nasi kwenye maisha haya, uliwapa watu wako urithi ambao hawatanyang’anywa milele; ambaye leo umeshusha rehema zako hizi juu ya wanafunzi na mitume wako, kwa njia iliyo safi kabisa, na ulipamba ndimi zao kwa ndimi za moto. Kwa hao sasa, na sisi pia pamoja na watu wote, tukishapokea kupitia kwa kusikia na masikio yetu maarifa matukufu kwenye lugha zetu, tumeangazwa na mwanga wa Roho na tumeachana na madanganyo ya giza, kwa kupewa vifaa na ndimi za moto uonekanao, na pia maajabu ya ushirika sawa, ambapo tumejazwa imani mbele yako, na utukuzwaye pamoja na Baba na Roho Mtakatifu, kwa Umungu mmoja, na uwezo mmoja.

Na umejazwa nguvu wewe, ambaye ni Mwanga wa Baba, kwa asili na umbo lake, gumu lisilobadilika, chemchemi ya hekima na ya neema, fumbua kinywa changu mimi mwenye dhambi, na nifundishe namna ya matakwa ninayopashwa kuomba. Kwa kuwa najua wingi wa dhambi zangu, lakini kwa kupenda kwako wema tumeshinda ubaya huo; tazama nasimama mbele yako, na nayatupa matatizo yote ya moyo wangu kwa rehema zako. Ongoza maisha yangu, utawale viumbe vyote kwa neno lako, kwa uwezo wa hekima zako zisizoeleweka, Ee bandari ya utulivu kwa msukosuko wa mawimbi unijulishe njia nitakayofuata.

Nijalie fahamu zangu Roho ya hekima zako, juu ya kutojua kwangu Roho ya fahamu zako; funika matendo yangu kwa Roho ya woga wako na ufanye upya Roho wa kweli ndani yangu; imarisha mawazo yangu dhaifu; ili nikilindwa daima, na Roho mwema, kwa yale yanayonifaa, kwa kuzishika sheria zako na kuwa na mawazo ya utukufu wako, kwako tena na mambo yote niliyoyatenda yastahiliyo adhabu; na usituachie kupotezwa na raha za kutatanisha za ulimwengu huu, lakini niweze kutamani kupigania hazina zijazo. Kwa kuwa, Ee Mkuu, ulisema chochote mtu atakachoomba kwa jina lako, atakipata bure kutoka kwa Mungu wako na Babako asiye na mwanzo wala mwisho; hivyo mimi pia mwenye dhambi, wakati wa kushuka Roho Mtakatifu, naomba wema wako ili unijalie vitu nilivyoomba ambavyo ni vya wokovu. Ndio, Ee Bwana, mpaji wa mema kwa kila pato, na mgawaji wa haraka; kwa kuwa ni wewe ugawaye rehema kwa wale wakuombao. Wewe ni mwenye huruma na neema, na umefanywa kuwa mshiriki wa mwili wetu, hata hivyo bila dhambi, na umetega masikio yako kwa kupenda wema wako usiopimika kwa wale wapigao magoti kwako, ambaye pia umefanya upatanisho kwa dhambi zetu.

Hivyo, Ee Bwana, gawa rehema zako kwa watu wako; usikie toka kwenye mbingu zako tukufu; tutakase kwa uwezo wa mkono wako wa kuume uokoao; tufunike kwa kivuli cha mabawa yako, na usidharau kazi ya mikono yako. Kwako pekee tumekosa na wewe pekee tunakutumikia; hatujui kutumikia miungu mingine, wala hatujui kuiinulia mikono yetu kwa mungu mwingine, Ee Bwana. Samehe dhambi zetu na ukubali maombi yetu haya tuombayo wakati tumepiga magoti; tuzidishie misaada ya mkono wako; pokea maombi ya watu wote, kama uvumba ukupendezao, ukubalikao mbele ya Ufalme wako mtukufu. [ARUSHA]

Inaongezwa sala hii

Ee Bwana, Bwana uliyetuokoa kwa mishale irukayo mchana, utuokoe pia na uovu wote wa giza. Kubali dhabihu zetu za jioni, hata kuinuliwa mikono yetu. Tujalie usiku wote tusiwe na dhambi, bila kujaribiwa na mambo ya kishetani; utuokoe na kila shida, ubaya na huzuni, vitokavyo kwa mwovu. Patia mioyo yetu kitubio, na akili zetu, wasiwasi ya kuchunguza sana mambo yatakavyokuwa siku ile ya kuogofya ya hukumu ya haki. Sulubisha miili yetu kwa kukuogopa, na tuisha waumini wetu; ili kwa usingizi wa utulivu, tutaangazwa kwa maneno ya hukumu zako. Pia tuondolee mawazo yasiyoonekana na maumivu ya kimwili. Tuamshe tena kwa sala; tukilindwa kwenye imani na kuelekea kuzishika amri zako. [ARUSHA]

SHEMASI:

Utusaidie, utuokoe, tuhurumie, utuinue na utuhifadhi, Ee Mungu, kwa neema yako.

Watu: Bwana hurumia.

SHEMASI:

Tumemkumbuka Maria Mtakatifu kamili, asiye na doa, mbarikiwa zaidi kushinda wote, Mama yetu mtukufu, Mzazi-Mungu na Bikira daima, pamoja na watakatifu wote, tujiweke sisi wenyewe na kila mmoja wetu na wenzetu wote na maisha yetu yote mikononi mwa Kristo Mungu.

Watu: Kwako. Ee Bwana.

KASISI

Kwa neema na rehema ya Mwanao wa pekee, ambaye pamoja naye unahimidiwa, pamoja na Roho wako mtakatifu kamili, mwema na mpaji wa uhai, sasa na siku zote hata milele na milele.

Watu: Amina.

Msomaji

Ee Bwana utujalie jioni hii tusiwe na dhambi. Wahimidiwa Ee Bwana, Mungu wa Baba zetu na jina lako limesifiwa na limetukuzwa milele. Amina. Ee BWANA, fadhili zako zikae nasi, Kama tunavyo kutumainia Wewe. Ee BWANA, umehimidiwa, Unifundishe amri zako. Wahimidiwa Ee Rabi, unifahamishe zilizo haki zako. Wahimidiwa, Ee Mtakatifu; uniangaze kwa zilizo haki zako. Ee BWANA, fadhili zako ni za milele; Usiiache kazi ya mikono yako. Sifa ni zako, kukuimbia ni kwako na utukufu ni wako, wa Baba na Mwana na Roho Mtakatifu, sasa na siku zote hata milele na milele. Amina.

( Amina. )

SHEMASI:

Tena, kwa kupiga magoti, tumwombe Bwana.

Watu Bwana hurumia.

KASISI

Ee chemichemi isiyokauka, iishiyo, iangazayo, enye nguvu ya uumbaji, mshirika mkuu wa Baba, Kristo Mungu wetu; uliyekamilisha mipango ya wokovu wa watu; uliyepasua vifungo vya mauti na vya kuzimu, na umeyakanyaga majeshi ya mwovu chini ya miguu yako; uliyejitoa mhanga bila lawama kwa ajili yetu, ukitoa dhabihu isiyoharibika, ambayo ni mwili wako na msamaha wa kila dhambi, ambayo, kupitia kwa tendo lako kuu la dhabihu isiyoelezeka, umetujalia uzima wa milele; uliyeshuka kuzimuni, na kuvunja kwa wale walioishi sehemu za chini ya ardhi; na kwa hekima zako ukiwashawishi asili ya madhara na joka la kuzimu; ukiwa umevutiwa na busara tukufu za kuvutia, ufunge kamba gizani au kwa moto mkali usiozimika milele kwa pingu zisizofunguka.

Ee hekima kuu itukuzwayo na Baba; ulijionyesha kama msaidizi mkuu kwa wanaoshambuliwa na ukawapa nguvu waliokaa gizani kwenye uvuli wa mauti. Ee Bwana, mwenye utukufu usioisha na Mwana mpendwa wa Baba aliye juu; Mwanga wa milele; Jua la haki, tusikie tukuombao bila kukoma; zipumzishe roho za watumishi wako, mababa na ndugu zetu, na jamaa zetu wengine, na wote tulio wa nyumba na imani moja, waliofariki na wale ambao tunawakumbuka leo; kwa kuwa Wewe ni mweza yote, na mikononi mwako umeushika ulimwengu wote. Ee Mwenyezi Mkuu, Mungu wa mababa zetu na Mungu wa huruma, Muumbaji wa koo zifaazo na zisizofaa, na tabia ya kila binadamu, ambayo imeletwa pamoja na kutunganisha tena; Muumbaji wa uhai na wa kifo, muda wa kukaa ulimwenguni na ufafanuzi wa ulimwengu ujao; umetugawia miaka ya maisha, na kuamuru siku ya kifo; Wewe unaua, nawe pia unafufua; unafanya kwa udhaifu, na unafungua kwa nguvu; ukiamua vitu vilivyopo kulingana na udhaifu wake, na kuamuru vitu vijavyo kuwa na manufaa; kuhimiza kwa matumaini ya ufufuo kwa wote walioteuliwa waliokuwa wamechomwa na mauti, kwa kuwa U mkweli.

Ee Mkuu wa watu wote, Mungu Mwokozi wetu, matumaini ya maisha yote ya dunia na wote walio mbali baharini; mwishoni mwa sikukuu hii ya ukombozi wa Pentekoste, umetufunulia siri, fumbo la Utatu Mtakatifu, asili na ushirika mmoja usiotengana na mamlaka sawa; na ulinyunyiza Roho wako Mtakatifu, Mpaji wa uhai, kwa namna ya ndimi za moto juu ya Mitume wako watakatifu, na ulimwamuru kuwa majumbe wa habari wa hekima la Hekima Tukufu ya Kweli; ambao leo hii, kwenye siku ya wokovu, kwa neema umekubali kuridhika, na maombi ya wafungwa wa kuzimu na kutuahidi sisi tulio utumwani matumaini makubwa ya kufunguliwa kutoka upotofu unaotutatiza sisi na wengine, na utatuma mfariji.

Tusikie sisi wanyenyekevu wako, tufanyao maombi kwako; na uzipatie nyoyo zilizolala za watumishi wako, mahali pa mwanga, kwenye nafasi ya usitawi, mahali pa raha, mahali ambapo hakuna magonjwa, huzuni, wala kusaga meno; na weka roho zao kwenye hema za watakatifu, na wajalie neema na amani na msamaha; kwa kuwa, Ee Bwana, wafu hawatakutukuza na wala walio kuzimuni, tujasirishe kutubu dhambi; ndipo sisi tulio hai tukuhimidi na kutoa maombi ya kukuridhisha na kafara kwa ajili ya roho zao. [ARUSHA]

Anaongeza sala hii

Ee Mungu Mkuu na wa milele, uliye mtakatifu na mpenda wanadamu, uliyetujalia wakati huu kusimama mbele ya utukufu wako usioelezeka, kuimba na kutukuza miujiza Yako, tutakase sisi watumishi wako tusiostahili; na tupe rehema, ili kwa moyo mkunjufu usio na majivuno, ili tukutolee wimbo wa mtakatifu mara tatu wa kukusifu, na kukushukuru kwa ajili ya vipaji viheshimiwa, ulivyotupa leo na kila siku. Ee Bwana, kumbuka udhaifu wetu, na usituangamize kwa sababu ya dhambi zetu, lakini uoneshe huruma kwa unyenyekevu wetu; ili, tukishaokolewa gizani, tuweze kutembea kwenye nuru ya haki; na ili tubaki imara tuweze kupiga shambulizi lolote la mwovu, na kwa ujasiri tuweze kukutukuza kwa vyovyote Wewe, Mungu wa kweli pekee, ambaye pia ni mpenda wanadamu.

Kwa kuwa, Ee Bwana na Muumbaji wa wanadamu wote, ni fumbo kwako kuu na la kweli, kifo cha muda kwa viumbe wako, na baadaye kufanya hai tena na kupumzishwa milele. Tunakiri rehema zako kwa vitu vyote, kuja kwetu ulimwenguni na kuondoka, na matumaini ya kufufuka tena, na kuishi milele, ambavyo tumedhaminiwa kupita kwa ahadi zako zisizoshindwa; ambazo tutazipokea ujapo mara ya pili. Kwa kuwa Wewe ndiwe Mfalme wa ufufuo wetu, na mwamuzi wa haki, mpole na mkarimu wa waliokufa, na ni Mkuu na Bwana wa malipo; uliyeshiriki ubinadamu kama tulivyo mwili na damu, kwa sababu ya fadhili zako kuu, kwa hiari yako ulijiweka majaribuni, kwa kukubali mateso kwa huruma yako ukateseka; lakini kwa kuwa nawe ulijaribiwa, umekuwa msaada wetu, sisi kama ulivyoahidi; na kutuongoza kwako kusikokuwa na mateso.

Kwa hiyo, Ee Mungu, pokea sala na maombi haya, na uwape mababa pumziko pamoja na mama, watoto, ndugu, dada na jamaa zetu wa damu moja na ukoo wa kila mmoja wetu, na kwa roho zote zilizokwishalala mbele yetu na weka roho zao kwenye tumaini la ufufuo na uzima wa milele; na yaandike kwenye kifua cha Ibrahimu, Isaaka na Yakobo, kwenye nchi ya wahai, kwenye ufalme wa mbinguni, kwenye Paradiso ya utamu, na, kwa malaika wako wang’arao, wakilinda wote kwenye jumba lako tukufu; waamuke pamoja nawe pia miili yetu siku ile uliyoamuru, kwa ahadi zako tukufu za uaminifu. Sababu umeshinda kifo, Ee Bwana, kwa kuwa watumishi wako tuhamapo toka miili, na kuja kwako Mungu wetu, lakini tunabadilika kutoka kwa vitu vya kusikitisha mpaka kwenye wema ufurahishao, kwenye pumziko na starehe.

Kwa hivyo, kama tumefanya makosa yoyote kwako, tuhurumie sisi na wao; kwa kuwa mbele yako hakuna asiye na doa, angalau mara moja kwa siku zote za maisha yake; okoa Wewe uliyejionyesha duniani pekee bila dhambi, Ee Bwana wetu Yesu Kristo, ambaye kwako tunauhakika wa kupata rehema na msamaha wa dhambi zetu.

Kwa hayo, Wewe Mungu mrahimu na mpenda wanadamu, sisi pamoja na hawa tusamehe, tuondolee, tuhurumie dhambi zetu za hiari, ama zisizo za hiari, tulizotenda aidha kwa mapenzi yetu, au sababu ya kutojua, zionekanazo, au zisizoonekana, za matendo, au mawazo, au maneno, na zozote zile kwa matendo ya maisha yetu yote; na kwa waliolala wape ondoleo na msamaha, na tubariki sisi tulioko hapa sasa, ukitujalia, pamoja na watu wako wote, mwisho mwema wenye amani, na tufungulie wema wa rehema zako na upendo wako kwa wanadamu, kwenye siku ile ya kutisha ya kuja kwako mara ya pili; na utustahilishe kwenye Ufalme wako wa mbinguni. [ARUSHA]

Na hapa inaongezwa sala hii

Ee Mungu Mkuu na wa juu sana, Wewe pekee hufi na unaishi kwenye mwanga usiofifia; kwa busara zako uliviumba vyote, ulitenga nuru toka gizani, na kuweka kutawala mchana, na mwezi na nyota kutawala usiku; uliyetujalia sisi wenye dhambi saa hii kuja mbele ya utukufu wako, ili tutubu, na kukutolea dhabihu yetu ya jioni ya kukusifu Wewe. Ee mpenda wanadamu uongoze sala zetu mbele yako kama uvumba na ukubali kama manukato matamu. Na tujalie kumaliza jioni hii na usiku unaokuja kwa amani; tupatie silaha ya nuru; tuokoe na mwogofyo wa usiku, na kila kitu kitembeacho usiku; na tujalie usingizi uliotupa kwa pumziko la udhaifu wetu, uwe bila mawazo ya kishetani. Ndio, Ee Mkuu wa juu ya wote, mpaji wa mema; tukiwa tunaenda kwenye vitanda vyetu kwa masikitiko, tuweze kulikumbuka jina Lako takatifu wakati wote wa usiku; kwa kuelimishwa na fikira kwa amri Zako, tutaamka na mioyo ya furaha kutukuza wema Wako, tukitoa sala na maombi kwa wingi wa mapendo Yako, kwa dhambi zetu na za watu wako wote, ulionao kwa neema, kwa maombi ya Mzazi Mungu Mtakatifu. [ARUSHA]

SHEMASI:

Utusaidie, utuokoe, tuhurumie, utuinue na utuhifadhi, Ee Mungu, kwa neema yako.

Watu: Bwana hurumia.

SHEMASI:

Tumemkumbuka Maria Mtakatifu kamili, asiye na doa, mbarikiwa zaidi kushinda wote, Mama yetu mtukufu, Mzazi-Mungu na Bikira daima, pamoja na watakatifu wote, tujiweke sisi wenyewe na kila mmoja wetu na wenzetu wote na maisha yetu yote mikononi mwa Kristo Mungu.

Watu: Kwako. Ee Bwana.

KASISI

Kwa kuwa Wewe ni mapumziko ya roho zetu na miili yetu, na kwako tunatoa utukufu, Baba na Mwana na Roho Mtakatifu, sasa na siku zote, hata milele na milele.

Watu: Amina.

SHEMASI:

Tumalize maombi yetu ya jioni kwa Bwana.

Watu: Bwana hurumia.

SHEMASI:

Utusaidie, utuokoe, utuhurumie, na utuhifadhi, Ee Mungu, kwa neema yako.

Watu: Bwana hurumia.

SHEMASI:

Jioni hii yote iwe kamili, takatifu, tulivu na bila dhambi, tuombe kwa Bwana.

Watu: Kidhi, Ee Bwana.

SHEMASI:

Kwa ajili ya kuwa na malaika wa amani, mwongozi mwaminifu, mlinzi wa roho zetu na mili yetu, tuombe kwa Bwana.

Watu: Kidhi, Ee Bwana.

SHEMASI:

Kwa ajili ya msamaha wa maondoleo ya dhambi na makosa yetu, tuombe kwa Bwana.

Watu: Kidhi, Ee Bwana.

SHEMASI:

Kwa ajili ya vitu vyema vinavyofaakwa roho zetu na amani ya dunia yote, tuombe kwa Bwana.

Watu: Kidhi, Ee Bwana.

SHEMASI:

Kwa ajili ya kumaliza maisha yetu yanayobaki kwa amani na toba, tuombe kwa Bwana.

Watu: Kidhi, Ee Bwana.

SHEMASI:

Tuombe ili mwisho wa maisha yetu uwe wa kikristo kwa amani, bila maumivu, aibu, tena tuone teto njema mbele ya kiti cha hukumu cha Kristo.

Watu: Kidhi, Ee Bwana.

SHEMASI:

Tumemkumbuka Maria Mtakatifu kamili, asiye na doa, mbarikiwa zaidi kushinda wote, Mama yetu mtukufu, Mzazi-Mungu na Bikira daima, pamoja na watakatifu wote, tujiweke sisi wenyewe na kila mmoja wetu na wenzetu wote na maisha yetu yote mikononi mwa Kristo Mungu.

Watu: Kwako. Ee Bwana.

KASISI

Kwa kuwa wewe u Mungu mwema na mpenda wanadamu, na kwako tunatoa utukufu kwa Baba na Mwana na Roho Mtakatifu. Sasa na siku zote hata milele na milele.

Watu: Amina.

Amani kwa wote.

Watu: Na iwe kwa roho yako.

SHEMASI:

Watu: Kwako. Ee Bwana.

KASISI (Kwa mnong’ono)

Ee Bwana, Mungu wetu, uliyeleta mbingu karibu nasi, na uliyekuja duniani kwa ajili ya wokovu wa wanadamu, tazama watumishi wako na warithi wako; kwa kuwa watumishi wako wameinamisha vichwa vyao, na shingo zao kwako, uliye Mungu wa kutisha na mpenda wanadamu, wakiwa hawatumaini msaada toka kwa mtu, lakini wanategemea huruma yako tu, na wanatazamia wokovu wako; uwatunze wakati wote, tena katika jioni hii na usiku ujao, waweze kushinda maadui wowote, vitendo vyovyote vya shetani, mawazo ya bure na ufahamu uovu.

KASISI (Kwa sauti.)

Ihimidiwe na itukuzwe himaya ya ufalme wako, wa Baba na Mwana na Roho Mtakatifu, sasa na siku zote, hata milele na milele.

Watu: Amina.

Mstari: Ee Mungu, uniumbie moyo safi, Uifanye upya na kuithibiti roho yangu. [Biblia "Union Version"]

Mstari: Usinitenge na uso wako, Wala roho yako mtakatifu usiniondolee. [Biblia "Union Version"]

Sasa Bwana, umetimiza ahadi yako, umruhusu mtumishi wako aende kwa amani. Maana kwa macho yangu nimeuona wokovu ulioleta, ambao umeutayarisha uonekane na watu wote: Mwanga utakaowaangazia watu wa mataifa, na utukufu kwa watu wako Israeli.

Mungu Mtakatifu, Mweza Mtakatifu, Usiyekufa Mtakatifu, utuhurumie. (3)

Utukufu kwa Baba na Mwana na Roho Mtakatifu. Sasa na siku zote hata milele na milele. Amina.

Ee Utatu mtakatifu kamili, utuhurumie. Bwana, utusamehe dhambi zetu. Rabi, utuondolee makosa yetu. Mtakatifu, utukaribie na kutuponya magonjwa yetu, kwa ajili ya jina lako.

Bwana hurumia. Bwana hurumia. Bwana hurumia.

Utukufu kwa Baba na Mwana na Roho Mtakatifu. Sasa na siku zote hata milele na milele. Amina.

Baba yetu uliye mbinguni, jina lako litukuzwe, Ufalme wako uje, mapenzi yako yatimizwe, hapa duniani kama huko mbinguni. Utupe leo mkate wetu wa kila siku, na utusamehe deni zetu, kama nasi tuwasamehevyo wadeni wetu, tena usitutie majaribuni, lakini utuokoe maovuni.

KASISI

Kwa kuwa ufalme, nauwezo, na utukufu ni wako, wa Baba na Mwana na Roho Mtakatifu, sasa na siku zote hata milele na milele.

Wahimidiwa Kristo Mungu wetu, uliyeonesha wavuvi kuwa wa busara, ulipowapelekea Roho Mtakatifu, na kwa ajili yao ukauvuta ulimwengu, Mpenda wanadamu utukufu kwako. [ARUSHA] (3)

SHEMASI:

Hekima!

( Bariki! )

KASISI

Aliye himidiwa Kristo Mungu wetu, daima sasa na siku zote hata milele na milele.

WATU

Amina.

MSOMAJI

Bwana, Mungu imarisha, imani Takatifu isiyo na lawama ya wakristo watawa wa Orthodoksi, na hili Kanisa Takatifu na mji huu, hata milele na milele.

Uliye wa thamani kushinda waheruvi, uliye na utukufu kuwapita bila kiasi waserafi, uliyemzaa Mungu neno, umebaki bila kukuharibu, uliye mzazi-Mungu kweli tunakutukuza we.

KASISI

Utukufu kwako, Ee Kristo Mungu, matumaini yetu, utukufu kwako.

WATU

Utukufu kwa Baba na Mwana na Roho Mtakatifu. Sasa na siku zote hata milele na milele. Amina.

Bwana hurumia. (3) Bariki!

KASISI

Yeye aliyejitoa kifuani mwa Baba mbinguni, na kushuka duniani na kutwaa umbo letu lote, na kulipa utukufu, na baadaye akapaa mbinguni tena, na kukaa kuume kwa Mungu Baba, ambaye pia aliwatumia wanafunzi wake na Mitume Roho Mtakatifu, aliye mmoja nawe, sawa kwa mamlaka na pia kwa utukufu na mwenye asili moja, na kwa njia yake uliwangazia, tena kupitia kwao aliuangazia ulimwengu wote, Kristo Mungu wetu wa kweli, kwa maombi ya Mama yake asiye na doa, asiye na kasoro, na ya wahubiri watakatifu wa Mungu na wasifiwa sana, na Mitume wabeba Roho Mtakatifu, na ya watakatifu wote, utuhurumie na utuokoe, kwa kuwa U mwema na mpenda wanadamu.

Watu

Amina.

KASISI

Kwa maombi ya mababa wetu watakatifu, Ee Bwana Yesu Kristo Mungu wetu, utuhurumie na utuokoe.

WATU

Amina.