Ibaada kwa Lugha Yangu
×




Utukufu kwako, Ee Mungu wetu, utukufu kwako.

Ee Mfalme wa mbinguni, mfariji, Roho wa kweli; uliye mahali po pote, na kuvijaza vitu vyote; uliye hazina ya mambo mema na mpaji wa uhai; njoo ukae kwetu na kutusafisha na kila doa, hata uziokoe roho zetu, Mwema we.

Maombi ya Trisaghio.

Mungu Mtakatifu, Mweza Mtakatifu, Usiyekufa Mtakatifu, utuhurumie. (3)

Ee Utatu mtakatifu kamili, utuhurumie. Bwana, utusamehe dhambi zetu. Rabi, utuondolee makosa yetu. Mtakatifu, utukaribie na kutuponya magonjwa yetu, kwa ajili ya jina lako.

Bwana hurumia, Bwana hurumia, Bwana hurumia.

Baba yetu uliye Mbinguni; Jina lako litukuzwe; Ufalme wako uje; mapenzi yako yatimizwe, hapa Duniani kama huko Mbinguni. Utupe leo mkate wetu wa kila siku; na utusamehe deni zetu; kama sisi tuwasamehevyo wadeni wetu; tena usitutie majaribuni, lakini tuokoe na yule mwovu.

Njooni, tumwinamie na tumsujudu Mungu mfalme wetu.

Njooni, tumwinamie na tumsujudu Kristo yu Mungu mfalme wetu.

Njooni, tumwinamie na tumsujudu yeye, Kristo aliye mfalme na Mungu wetu.

Zaburi ya 19 (20).

Bwana akujibu siku ya dhiki, Jina la Mungu wa Yakobo likuinue. Akupelekee msaada toka patakatifu pake, Na kukutegemeza toka Zayuni. Azikumbuke sadaka zako zote, na kuzitakabali dhabihu zako. Akujalie kwa kadiri ya haja ya moyo wako, na kuyatimiza mashauri yako yote. Na tuushangilie wokovu wako, Kwa jina la Mungu wetu tuzitweke bendera zetu. Bwana akutimizie matakwa yako yote. Sasa najua kuwa Bwana amwokoa masihi wake; Atamjibu toka mbingu zake takatifu, kwa matendo makuu ya wokovu ya mkono wake wa kuume. Hawa wanataja magari na hawa farasi, bali sisi tutalitaja jina la Bwana, Mungu wetu. Wao wameinama na kuanguka, Bali sisi tumeinuka na kusimama. Bwana, umwokoe mfalme, Utuitikie siku tukuitayo.

Zaburi ya 20 (21).

Ee Bwana, mfalme atazifurahia nguvu zako, na wokovu wako ataufanyia shangwe nyingi sana. Umempa haja ya moyo wake, wala hukumzuilia matakwa ya midomo yake. Maana umemsongezea baraka za heri, Umemvika taji ya dhahabu safi kichwani pake. Alikuomba uhai, ukampa, muda mrefu wa siku nyingi, milele na milele. Utukufu wake ni mkuu kwa wokovu wako, Heshima na adhama waweka juu yake. Maana umemfanya kuwa baraka za milele, wamfurahisha kwa furaha ya uso wako. Kwa kuwa mfalme humtumaini Bwana, na kwa fadhili zake Aliye juu hataondoshwa. Mkono wako utawapata adui zako wote, mkono Wako wa kuume utawapata wanaokuchukia. Utawafanya kuwa kama tunuru ya moto, Wakati wa ghadhabu yako. Bwana atawameza kwa ghadhabu yake, na moto utawala. Matunda yao utayaharibu na kuyaondoa katika nchi, na wazao wao katika wanadamu. Madhali walinuia kukutenda mabaya, waliwaza hila wasipate kuitimiza. Kwa maana utawafanya kukupa kisogo, kwa upote wa uta wako ukiwaelekezea mishale. Ee Bwana, utukuzwe kwa nguvu zako, nasi tutaimba na kuuhimidi uweza wako.

Utukufu kwa Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu. Sasa na siku zote hata milele na milele. Amina.

Maombi ya Trisaghio.

Mungu Mtakatifu, Mweza Mtakatifu, Usiyekufa Mtakatifu, utuhurumie. (3)

Ee Utatu mtakatifu kamili, utuhurumie. Bwana, utusamehe dhambi zetu. Rabi, utuondolee makosa yetu. Mtakatifu, utukaribie na kutuponya magonjwa yetu, kwa ajili ya jina lako.

Bwana hurumia, Bwana hurumia, Bwana hurumia.

Baba yetu uliye Mbinguni; Jina lako litukuzwe; Ufalme wako uje; mapenzi yako yatimizwe, hapa Duniani kama huko Mbinguni. Utupe leo mkate wetu wa kila siku; na utusamehe deni zetu; kama sisi tuwasamehevyo wadeni wetu; tena usitutie majaribuni, lakini tuokoe na yule mwovu.

KASISI

Kwa kuwa ufalme ni wako, na nguvu, na utukufu, wa Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu, sasa na siku zote hata milele na milele.

MSOMAJI

Amina.

Ee Bwana okoa watu wako na ubariki urithi wako, uwape wafalme kushinda juu ya wakafiri na kulinda jamii yako kwa msalaba wako. [[SWA]]

Utukufu kwa Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu.

Ee Kristo, uliyeinuliwa msalabani kwa hiari, ipe rehema yako jamii mpya iliyo na jina lako. Wafurahishe watawala wetu waaminifu katika nguvu yako ukiwapa kushinda juu ya maadui wao. Tuwe na msaada wako ulio silaha ya amani na alama isioshindikana. [[SWA]]

Sasa na siku zote hata milele na milele. Amina.

Ee Mzazi Mungu msifiwa, mhifadhi unayeogopwa na usiyeshindwa, usidharau maombi yetu Mwema we. Tegemeza jamii ya waorthodoksi na kuwaokoa ambao umewaamrisha kuwa watawala, na uwape ushindi toka mbinguni; kwa kuwa ulimzaa Mungu, wewe uliye mbarikiwa pekee. [[SWA]]

KASISI

Utuhurumie, Ee Mungu kadiri ya huruma yako kubwa, tunakuomba utusikilize na kutuhurumia.

( Bwana, hurumia. (3) )

Tena tunakuomba kwa ajili ya Wakristo watawa waorthodoksi wote.

( Bwana, hurumia. (3) )

( Bwana, hurumia. (3) )

Kwa kuwa U Mungu mrahimu na mpenda wanadamu, na kwako tunatoa utukufu, kwa Baba na Mwana na Roho Mtakatifu, sasa na siku zote hata milele na milele.

MWIMBAJI

Amina. Kwa jina la Bwana, Ee Padri bariki.

KASISI

Utatu mtakatifu mwenye asili moja, mpaji wa uhai, usiotegwa utukufu uwe kwako, daima, sasa na siku zote hata milele na milele.

MSOMAJI

Amina.

Zaburi Sita

Utukufu kwa Mungu juu pia, na nchini amani, urathi kwa wanadamu (3)

Ee Bwana fungua midomo yangu na kinywa changu kitazinena sifa zako. (x 2)

Zaburi 3.

Bwana, watesi wangu wamezidi kuwa wengi, ni wengi wanaonishambulia, ni wengi wanaoiambia nafsi yangu, hana wokovu huyu kwa Mungu. Na Wewe, Bwana, U ngao yangu pande zote, utukufu wangu na mwinua kichwa changu.Kwa sauti yangu namwita Bwana, naye aniitikia toka mlima wake mtakatifu.Nalijilaza nikalala usingizi, nikaamka, kwa kuwa Bwana ananitegemeza. Sitayaogopa makumi elfu ya watu, waliojipanga juu yangu pande zote. Bwana, uinuke, Mungu wangu, uniokoe, maana umewapiga taya adui zangu wote; umewavunja meno wasio haki. Wokovu una Bwana; baraka yako na iwe juu ya watu wako.

Nalijilaza nikalala usingizi, nikaamka, kwa kuwa Bwana ananitegemeza. [[SWA]]

Zaburi ya 37 (38).

Ee Bwana, usinilaumu katika ghadhabu yako, wala usiniadhibu kwa ukali wa hasira yako. Kwa maana mishale yako imenichoma, na mkono wako umenipata. Hamna uzima katika mwili wangu kwa sababu ya ghadhabu yako. Wala hamna amani mifupani mwangu kwa sababu ya hatia zangu. Maana dhambi zangu zimenifunikiza kichwa, kama mzigo mzito zimenilemea mno. Jeraha zangu zinanuka, zimeoza, kwa sababu ya upumbavu wangu. Nimepindika na kuinama sana, mchana kutwa nimekwenda nikihuzunika. Maana viuno vyangu vimejaa homa, wala hamna uzima katika mwili wangu. Nimedhoofika na kuchubuka sana, nimeugua kwa fadhaa ya moyo wangu. Bwana, haja zangu zote ziko mbele zako, kuugua kwangu hakukusitirika kwako. Moyo wangu unapwita-pwita, nguvu zangu zimeniacha; nuru ya macho yangu nayo imeniondoka. Wanipendao na rafiki zangu wanasimama mbali na pigo langu; naam, karibu zangu wamesimama mbali. Nao wanaoutafuta uhai wangu hutega mitego; nao wanaotaka kunidhuru hunena mabaya; na kufikiri hila mchana kutwa. Lakini kama kiziwi sisikii, nami ni kama bubu asiyefumbua kinywa chake. Naam, nimekuwa kama mtu asiyesikia, ambaye hamna hoja kunywani mwake. Kwa kuwa nakungoja Wewe, Bwana, Wewe utajibu, Ee Bwana, Mungu wangu. Maana nalisema, Wasije wakanifurahia; mguu wangu ukiteleza wajitukuza juu yangu. Kwa maana mimi ni karibu na kusita, na maumivu yangu yako mbele yangu daima. Kwa maana nitaungama uovu wangu, na kusikitika kwa dhambi zangu. Lakini adui zangu ni wazima wenye nguvu, nao wanaonichukia bure wamekuwa wengi. Naam, wakilipa mabaya kwa mema, huwa adui zangu kwa kuwa nalifuata lililo jema. Wewe, Bwana, usiniache, Mungu wangu, usijitenge nami. Ufanye haraka kunisaidia, Ee Bwana, wokovu wangu.

Wewe, Bwana, usiniache, Mungu wangu, usijitenge nami. Ufanye haraka kunisaidia, Ee Bwana, wokovu wangu. [[SWA]]

Zaburi ya 62 (63).

Ee Mungu, Mungu wangu, nitakutafuta mapema, nafsi yangu inakuonea kiu, mwili wangu wakuonea shauku, katika nchi kame na uchovu, isiyo na maji. Ndivyo nilivyokutazama katika patakatifu, nizione nguvu zako na utukufu wako. Maana fadhili zako ni njema kuliko uhai; midomo yangu itakusifu. Ndivyo nitakavyokubariki maadamu ni hai; kwa jina lako nitaiinua mikono yangu. Nafsi yangu itakinai kama kushiba mafuta na vinono; kinywa changu kitakusifu kwa midomo ya furaha. Ninapokukumbuka kitandani mwangu, nakutafakari Wewe makesha yote ya usiku. Maana Wewe umekuwa msaada wangu, na uvulini mwa mbawa zako nitashangilia. Nafsi yangu inakuandama sana; mkono wako wa kuume unanitegemeza. Bali waitafutao nafsi yangu, ili kuiharibu, wataingia pande za nchi zilizo chini. Watatolewa wafe kwa nguvu za upanga, watakuwa riziki za mbwa mwitu. Bali mfalme atamfurahia Mungu, kila aapaye kwa Yeye atashangilia, kwa maana vinywa vya waongo vitafumbwa.

Nakutafakari Wewe makesha yote ya usiku. Maana Wewe umekuwa msaada wangu, na uvulini mwa mbawa zako nitashangilia. Nafsi yangu inakuandama sana; mkono wako wa kuume unanitegemeza.

Utukufu kwa Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu. Sasa na siku zote hata milele na milele. Amina.

Alleluia, Alleluia, Alleluia. Utukufu kwako, Ee Mungu.

Alleluia, Alleluia, Alleluia. Utukufu kwako, Ee Mungu.

Alleluia, Alleluia, Alleluia. Utukufu kwako, Ee Mungu.

Bwana, hurumia. Bwana, hurumia. Bwana, hurumia.

Utukufu kwa Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu. Sasa na siku zote hata milele na milele. Amina.

Zaburi ya 87 (88).

Ee Bwana, Mungu wa wokovu wangu, mchana na usiku nimelia mbele zako. Maombi yangu yafike mbele zako, uutegee ukelele wangu sikio lako. Maana nafsi yangu imeshiba taabu, na uhai wangu umekaribia kuzimu. Nimehesabiwa pamoja nao washukao shimoni; nimekuwa kama mtu asiye na msaada. Miongoni mwao waliokufa nimetupwa, kama waliouawa walalao makaburini. Hao ambao Wewe huwakumbuki tena, wametengwa mbali na mkono wako. Mimi umenilaza katika shimo la chini, katika mahali penye giza vilindini. Ghadhabu yako imenilemea, umenitesa kwa mawimbi yako yote. Wanijuao umewatenga nami; umenifanya kuwa chukizo kwako; nimefungwa wala siwezi kutoka; jicho langu limefifia kwa ajili ya mateso. Bwana, nimekuita kila siku; nimekuita nimekunyoshea Wewe mikono yangu. Wafu je! Utawafanyia miujiza? Au waliofariki watasimama na kukuhimidi? Fadhili zako zitasimuliwa kaburini? Au uaminifu wako katika uharibifu? Miujiza yako itajulikana gizani? Au haki yako katika nchi ya usahaulifu? Lakini mimi nimekulilia Wewe, Bwana, na asubuhi maombi yangu yatakuwasilia. Bwana, kwa nini kuitupa nafsi yangu, na kunificha uso wako? Nateswa mimi hali ya kufa tangu ujana, nimevumilia vitisho vyako na kufadhaika. Hasira zako kali zimepita juu yangu, maogofya yako yameniangamiza. Yamenizunguka kama maji mchana kutwa, yamenisonga yote pamoja. Mpenzi na rafiki umewatenga nami, nao wanijuao wamo gizani.

Ee Bwana, Mungu wa wokovu wangu, mchana na usiku nimelia mbele zako. Maombi yangu yafike mbele zako, uutegee ukelele wangu sikio lako. [[SWA]]

Zaburi ya 102 (103).

Ee nafsi yangu, umhimidi Bwana, Naam, vyote vilivyo ndani yangu vilihimidi jina lake takatifu. Ee nafsi yangu, umhimidi Bwana, wala usizisahau fadhili zake zote. Akusamehe maovu yako yote, akuponya magonjwa yako yote, aukomboa uhai wako na kaburi, akutia taji ya fadhili na rehema, aushibisha mema uzee wako, ujana wako ukarejezwa kama tai; Bwana ndiye afanyaye mambo ya haki, na hukumu kwa wote wanaoonewa. Alimjulisha Musa njia zake, wana wa Israeli matendo yake. Bwana amejaa huruma na neema, haoni hasira upesi, ni mwingi wa fadhili. Yeye hatateta sikuzote, wala hatashika hasira yake milele. Hakututenda sawasawa na hatia zetu, wala hakutulipa kwa kadiri ya movu yetu. Maana kama mbingu zilivyoinuka juu ya nchi, kadiri ile ile rehema zake ni kuu kwa wamchao. Kama Mashariki ilivyo mbali na magharibi, ndivyo Bwana alivyoweka dhambi zetu mbali nasi. Kwa maana Yeye anatujua umbo letu, na kukumbuka ya kuwa sisi tu mavumbi. Mwanadamu siku zake zi kama majani; kama ua la kondeni ndivyo asitawivyo. Maana upepo hupita juu yake, kumbe haliko! Na mahali pake hapatalijua tena. Bali fadhili za Bwana zina wamchao tangu milele hata milele, na haki yake ina wana wa wana; maana, wale walishikao agano lake, na kuyakumbuka maagizo yake ili wayafanye. Bwana ameweka kiti chake cha enzi mbinguni, na ufalme wake unavitawala vitu vyote. Mhimidini Bwana, enyi malaika zake, ninyi mlio hodari, mtendao neno lake, mkiisikiliza sauti ya neno lake. Mhimidini Bwana, enyi majeshi yake yote, ninyi watumishi wake mfanyao mapenzi yake. Mhimidini Bwana, enyi matendo yake yote, mahali pote pa milki yake; Ee nafsi yangu, umhimidi Bwana.

Mahali pote pa milki yake; Ee nafsi yangu, umhimidi Bwana. [[SWA]]

Zaburi ya 142 (143).

Ee Bwana, uisikie sala yangu, uzisikilize dua zangu, kwa uaminifu wako unijibu kwa haki yako. Wala usimhukumu mtumishi wako, maana kwako hakuna aliye hai mwenye haki. Maana adui ameifuatia nafsi yangu, ameutupa chini uzima wangu, amenikalisha mahali penye giza, kama watu waliokufa zamani. Na roho yangu imezimia ndani yangu, moyo wangu ndani yangu umesituka. Nimezikumbuka siku za kale, nimeyatafakari matendo yako yote, naziwaza kazi za mikono yako. Nakunyoshea mikono yangu; nafsi yangu inakuonea kiu kama nchi kame. Ee Bwana, unijibu hima, roho yangu imelegea; usinifiche uso wako, nisifanane nao washukao shimoni. Unifanye kusikia fadhili zako asubuhi, kwa maana nimekutumaini Wewe. Unijulishe njia nitakayoiendea, kwa maana nakuinulia nafsi yangu. Ee Bwana, uniponye na adui zangu; nimekukimbilia Wewe, unifiche. Unifundishe kuyatenda mapenzi yako, kwa maana ndiwe Mungu wangu. Roho yako mwema aniongoze kwenye nchi sawa, Ee Bwana, unihuishe kwa ajili ya jina lako, kwa haki yako unitoe roho yangu taabuni; kwa fadhili zako utawakatilia mbali adui zangu; na kuwaangamiza wote wanitesao nafsi, kwa maana mimi ni mtumishi wako.

Unijibu kwa haki yako, wala usimhukumu mtumishi wako.

Unijibu kwa haki yako, wala usimhukumu mtumishi wako.

Roho yako mwema aniongoze kwenye nchi sawa. [[SWA]]

Utukufu kwa Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu. Sasa na siku zote hata milele na milele. Amina.

Alleluia, Alleluia, Alleluia. Utukufu kwako, Ee Mungu.

Alleluia, Alleluia, Alleluia. Utukufu kwako, Ee Mungu.

(yaimbwa)

Alleluia, Alleluia, Alleluia. Utukufu kwako, Ee Mungu. Matumaini yetu, Ee Bwana, utukufu kwako.

Bwana ndiye Mungu naye amefunuliwa kwetu, abarikiwe yeye ajaye kwa jina la Bwana. [[SWA]]

Mstari 1: Mshukuruni Bwana , litieni jina lake takatifu [[SWA]]

Mstari 2: Mataifa yote walinizunguka; kwa jina la Bwana niliwakatalia mbali.

Mstari 3: Neno hili limetoka kwa Bwana nalo ni la ajabu machoni mwetu

Alleluia. (3)

Mstari

Mstari

Mstari 1:

Alleluia, Alleluia, alleluia.

Mstari 2:

Mstari 3:

Mstari 4:

Sauti 2.

Mtakatifu ni Bwana, Mungu wetu. (3)

Mstari Asubuhi tumejazwa na huruma yako, Ee Bwana; [[SWA]]

Mstari Asubuhi tumejawa na huruma yako, Ee Bwana; tunashangilia na kuchangamka siku zetu zote. [[SWA]]

Mstari Tulishangilia katika siku ulizotunyenyekeza; miaka ambayo tuliona dhiki; tazama watumishi Wako, na kazi yako, na kuongoza watoto wao. [[SWA]]

Mstari Ubora wa Bwana Mungu wetu uwe juu yetu; atuongoze kwa kazi ya mikono yetu; hata kazi ya mikono yetu Aiongoze. [[SWA]]

Ni vyema kukiri kwa Bwana na kusifu jina lako, wewe uliye juu, pia kuihubiri huruma yako asubuhi na kuueleza ukweli wako wakati wa usiku. [[SWA]]

Mstari

Mstari

Mstari

Mstari