×




KASISI

Ahimidiwe Mungu wetu, daima, sasa na siku zote, hata milele na milele.

/MSOMAJI

Njooni, tumwinamie na tumsujudu Mungu mfalme wetu.

Njooni, tumwinamie na tumsujudu Kristo yu Mungu mfalme wetu.

Njooni, tumwinamie na tumsujudu yeye, Kristo aliye mfalme na Mungu wetu.

Zaburi ya 103 (104).

Ee nafsi yangu, umhimidi Bwana. Wewe, Bwana, Mungu wangu, umejifanya mkuu sana; umejivika heshima na adhama. Umejivika nuru kama vazi; umezitandika mbingu kama pazia; na kuziweka nguzo za orofa zake majini. Huyafanya mawingu kuwa gari lake, na kwenda juu ya mabawa ya upepo, huwafanya malaika zake kuwa pepo, na watumishi wake kuwa moto wa miali. Uliiweka nchi juu ya misingi yake, isitikisike milele. Uliifunika kwa vilindi kama kwa vazi, maji yalikuwa yakisimama juu ya milima. Kwa kukemea kwako yakakimbia, kwa sauti ya radi yako yakaenda zake kasi, yakapanda milima, yakatelemka mabondeni, mpaka mahali ulipoyatengeneza. Umeweka mpaka yasiupite, wala yasirudi kuifunikiza nchi. Hupeleka chemchemi katika mabonde; zapita kati ya milima; zamnywesha kila mnyama wa kondeni; punda mwitu huzima kiu yao. Kandokando hukaa ndege wa angani; kati ya matawi hutoa sauti zao. Huinywesha milima toka orofa zake; nchi imeshiba mazao ya kazi zako. Huyameesha majani kwa makundi, na maboga kwa matumizi ya mwanadamu; ili atoe chakula katika nchi, na divai imfurahishe mtu moyo wake. Aung''aze uso wake kwa mafuta, na mkate umburudishe mtu moyo wake. Miti ya Bwana nayo imeshiba, mierezi ya Lebanoni aliyoipanda. Ndimo ndege wafanyamo vitundu vyao, na korongo, misunobari ni nyumba yake. Milima mirefu ndiko waliko mbuzi wa mwitu, na magenge ni kimbilio la wibari. Aliufanya mwezi kwa ajili ya nyakati, jua latambua kuchwa kwake. Wewe hufanya giza, kukawa usiku, ndipo atambaapo kila mnyama wa mwitu. Wana-simba hunguruma wakitaka mawindo, ili kutafuta chakula chao kwa Mungu. Jua lachomoza, wanakwenda zao, na kujilaza mapangoni mwao. Mwanadamu atoka kwenda zake kazini, na kwenye utumishi wake mpaka jioni. Ee Bwana, jinsi yalivyo mengi matendo yako! Kwa hekima umevifanya vyote pia. Dunia imejaa mali zako. Bahari iko kule, kubwa na upana, ndimo mlimo viendavyo visivyohesabika, viumbe hai vidogo kwa vikubwa. Ndimo zipitamo merikebu, ndimo alimo lewiathani uliyemwumba acheze humo. Hao wote wanakungoja Wewe, uwape chakula chao kwa wakati wake. Wewe huwapa, wao wanakiokota; Wewe waukunjua mkono wako, wao wanashiba mema; Wewe wauficha uso wako, wao wanafadhaika; waiondoa pumzi yao, wanakufa, na kuyarudia mavumbi yao. Waipeleka roho yako, wanaumbwa, nawe waufanya upya uso wa nchi. Utukufu wa Bwana na udumu milele; Bwana na ayafurahie matendo yake. Aitazama nchi, inatetemeka; aigusa milima, inatoka moshi. Nitamwimbia Bwana maadamu ninaishi; nitamshangilia Mungu wangu nikiwa hai; kutafakari kwangu na kuwe kutamu kwake; mimi nitamfurahia Bwana. Wenye dhambi waangamizwe katika nchi, watendao ubaya wasiwepo tena. Ee nafsi yangu, umhimidi Bwana.

Jua latambua kuchwa kwake; Wewe hufanya giza kukawa usiku,

Ee Bwana, jinsi yalivyo mengi matendo yako! Kwa hekima umevifanya vyote pia. [[SWA]]

Utukufu kwa Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu. Sasa na siku zote hata milele na milele. Amina.

Alleluia, Alleluia, a|leluia. Utukufu kwako, Ee Mungu. (3)

Matumaini yetu, Ee Bwana, utukufu kwako.

(Wakati msomaji anapoanza kusoma zaburi 104, kasisi akisimama mbele ya Meza takatifu anasoma maombi haya kwa sauti ya chini,

KASISI

Ombi la kwanza.Tumwombe Bwaba, Bwana hurumia.

Tumwombe Bwana, Bwana hurumiaEe Bwana, mvumilivu, mwenye huruma nyingi na mpenda wanadamu yasikie sala zetu na utege sikio lako kwa sauti ya maombi yetu. Imarisha agano jema kwetu; ma utuongoze tuishi kwa ukweli wako. Furahisha mioyo yetu tulitii jina lako takatifu; u mkubwa na mtenda maajabu, Mungu wa pekee na hakuna mungu mwingine kama Wewe, Ee Bwana; wa fadhili na wa uwezo unayetusaidia, kutegemeza na kuwaokoa wanaotumaini jina lako takatifu. Kwa kuwa utukufu, heshima na usujudu ni haki yako, ya Baba na Mwanaa na Roho Mtakatifu, sasa na siku zote hata milelel na milelel. Amina.. [[SWA]]

Amina.

Tumwombe Bwana, Bwana hurumia Ee Bwana usitukemee na kutuadhibu kwa hasira yako, bali utupe kwa kadiri ya upole wako uliye mganga na mponyaji wa Roho zetu. UTuongoze kwenye kimbilio la nia yako na kuangaza mioyo yetu kujua ukweli walo. Tena, utujalie usiku huu na siku zote za maisha yetu ziwe za amani, bila dhambi, kwa maombi ya mzazi Mungu mtakatifu na ya watakatifu wote. Kwa kuwa utawala ni wako na ufalme na nguvu na utukufu ni vyako, vya Baba na Mwana na Roho Mtakatifu, sasa na siku zote hata milele na milele. [[SWA]]

Amina.

Ee Bwana Mungu wetu, utukumbuke sisi watumishi wako wenye dhambi wasiofaa tutajapo jina lako takatifu na tuwekapo tumaini letu kwa rehema yako, bali utujalie kwa yale yote tunayokuomba kwa ajili ya wokovu wetu, Ee Bwana; utufanye wafaao kukupenda na kukuogopa kwa mioyo yetu yote na kumarisha nia yako kwa vitu vyote. Kwa kuwa u Mwenye rhema na mpenda wanadamu na kwako tunatoa utukufu kwa Baba na MWana na Roho Mtakatifu, sasa na siku zote hata milele na milele. Amina. [[SWA]]

Amina.

Ewe, unayesifiwa kwa nguvu takatifu, kwa nyimbo za utukufu zisizo kuwa na mwisho, ujaze vinywa vyetu na utukufu wako ili tulihimidi jina lako takatifu; na utuunganishe na utupe urithi pamoja nao wakuogopao katika ukweli na wanaotunza amri zako; kwa maombi ya mtakatifu Mzazi Mungu na watakatifu wako, kwa kuwa wastahili wote, heshima na usjudu ni haki yako, ya Baba na Mwana na Roho Mtakatifu, sasa na siku zote hata milele na milele. Amina. [[SWA]]

Amina.

Ee Bwana, Ee Bwana ushikaye vitu vyote katika kiganja chako kisicho na doa, mvumilivu pamoja sisi sote na unayehuzunika na kubadirsha maamuzi kwa maovu yetu, kumbuka rehema zako na huruma zako, utembelee na ukarimu wako,; na utujalie tuepuke usiku huu wote katika mawazo mabaya ya muovu na tunza maisha yetu bila shambulio lolote kwa rehema ya roho yako takatifu kam ili. Na huruma na Upendo kwa mwandamu wa Mwana wako wa pekee pamoja naye unahimidiwa, pamoja na utakatifu wote na Roho mwema na mpaji wa uhai, sasa na siku zote hata milele na milelel. Amina, [[SWA]]

Amina.

Ee Mungu, mtukufu wa ajabu, unaye ongoza ulimwengu na wema wako usio erezeka na ulinzi tele, uliye tupatia mema yote ya dunia na uliye turidhia ufalme ulio tuahidi kwa mema yaote ulio tujalia; wewe uliye tuwezesha kwenda mbali na maovu kwa kipindi cha siku kilichopita, utujalie tuwe bila dhambi kwa wakati uliosalia mbele ya utukufu wako mtakatifu, tukutuze Mungu wetu pekee mwema na mpenda wanadamu. Kwa kuwa U Mungu wetu na kwako tunatoa utukufu kwa Baba na wana na Roho Mtakatifu, sasa na siku zote hata milele na milele. Amina. [[SWA]]

Amina.

Ee Mungu mtukufu na aliye huu, uliye pekee asiyekufa, unayeishi kwa mwanga usiyofikika; uliyeumba vitu vyote kwa hekima ; uliye gawanya mwanga na giza nakuweka jua kutawala mchana, na mwezi na nyota kutawala usiku; uliyetujalia sisi wenye dhambi kufikia uso wako wakati huu katika kutubu na kukutolea shukrani za maombi ya jioni; wee, Bwana mpenda wanadamu, elekeza maombi yetu yapae kwako kama uvumba na yakubali kama manukato ya kupendeza. Na jioni hii na usiku ujao uwe wa amani, utuvike siraha ya mwanga; utuokoe kutoka kila ogofya la siku na kutoka kila kinacho tembea gizani. na utupatie usingizi, ulio tujalia kupumzishakutoka magojwa yetu, tuwe huru kutoka mawazo maovu.Ndiyo, Ee Bwana mutawala, wa vitu vyote unaye tujaliaa mema, ili, tunapolla vitandani mwetu tukumbuke jina lako wakati wa usiku, na tukiwa tumeangazwa na amri zako, tuamke na kukutukuza wema na roho ya furaha, kwa kutoa sala na maombi kwa upendo wako kwa ajili ya dhambi zetu na kwa ajili ya watu wako, watu ambao unawatembelea kwa rehema, kwa utetezi wa mtakatifu Mzazi Mungu kwa U Mungu mwema na mpenda wanadamu na kwako tunatoa utukufu kwa Baba na Mwana na Roho Mtakatifu, sasa na siku zote hata milele na milele. Amina, [[SWA]]

Amina.

SHEMASI

Kwa amani, tumwombe Bwana.

WATU

Bwana, hurumia.

SHEMASI

Kwa ajili ya amani kutoka juu na ya wokovu wa roho zetu, tumwombe Bwana.

Kwa ajili ya amani ya dunia yote, na kusimama imara kwa Ekklesia Takatifu ya Mungu, na ya umoja wa wote, tumwombe Bwana.

Kwa ajili ya nyumba hii takatifu na waingiamo kwa imani, heshima na kumcha Mungu, tumwombe Bwana.

Kwa ajili ya wakristo wateule na waorthodoksi wote, tumwombe Bwana.

Kwa ajili ya Askofu wetu mkuu Askofu wetu mkuu (jina) Makasisi, Mashemasi wateule na watu wote tumwombe Bwana.

Kwa ajili ya taifa letu (jina) na raisi wetu (jina), na viongozi wetu, na wa majeshi wapendao dini, tumwombe Bwana.

Kwa ajili ya mji huu na miji yote na nchi zote na waishimo kwa imani, tumwombe Bwana.

Kwa ajili ya majira mema ya mwaka kupata mvua ya kutosha na hewa safi na rotuba ya kutosha kwa ardhi, tumwombe Bwana.

Kwa ajili ya wasafiri hewani juu, baharini majini, na nchini kavu, wachoshwa na mateka kupata uhuru, na kwa ajili ya wokovu wao, tumwombe Bwana.

Kwa ajili ya kuokolewa kwa kila sitikiko, ghadhabu, hatari na uhitaji, tumwombe Bwana.

Utusaidie, utuokoe, utuhurumie, utuhifadhi, Ee Mungu, kwa neema yako.

Tumkumbuke Maria Mtakatifu kamili, asiye na doa, Mbarikiwa zaidi kushinda wote, Bibi wetu mtukufu mzazi Mungu na bikira daima pamoja na watakatifu wote hata sisi pia wenyewe na kila mmoja wetu na wenzetu wote, hata maisha yetu, kujiweka mikononi mwa Kristo Mungu.

Kwako, Ee Bwana.

KASISI

Kwa kuwa utukufu wote na heshima na usujudu ni haki yako, ya Baba na Mwana na Roho Mtakatifu, sasa na siku zote, hata milele na milele.

WATU

Amina.

KATHISMATA YA 1.

Zaburi ya 1.

Heri mtu yule asiyekwenda katika shauri la wasio haki; wala hakusimama katika njia ya wakosaji; wala hakuketi barazani pa wenye mizaha. Bali sheria ya BWANA ndiyo impendezayo; na sheria yake huitafakari mchana na usiku. Naye atakuwa kama mti uliopandwa kandokando ya vijito vya maji, uzaao matunda yake kwa majira yake, wala jani lake halinyauki; na kila alitendalo litafanikiwa. Sivyo walivyo wasio haki; hao ni kama makapi yapeperushwayo na upepo. Kwa hiyo wasio haki hawatasimama hukumuni, wala wakosaji katika kusanyiko la wenye haki. Kwa kuwa BWANA anaijua njia ya wenye haki, bali njia ya wasio haki itapotea.

Zaburi ya 2.

Mbona mataifa wanafanya ghasia, na makabila wanatafakari ubatili? Wafalme wa dunia wanajipanga, na wakuu wanafanya shauri pamoja, juu ya BWANA, na juu ya masihi wake, Na tuvipasue vifungo vyao, na kuzitupia mbali nasi kamba zao. Yeye aketiye mbinguni anacheka, Bwana anawafanyia dhihaka. Ndipo atakaposema nao kwa hasira yake, na kuwafadhaisha kwa ghadhabu yake. Nami nimemweka mfalme wangu juu ya Sayuni, mlima wangu mtakatifu. Nitaihubiri amri; BWANA aliniambia, Ndiwe mwanangu, Mimi leo nimekuzaa. Uniombe, nami nitakupa mataifa kuwa urithi wako, na miisho ya dunia kuwa milki yako. Utawaponda kwa fimbo ya chuma, na kuwavunja kama chombo cha mfinyanzi. Na sasa, enyi wafalme, fanyeni akili, enyi waamuzi wa dunia, mwadibiwe. Mtumikieni BWANA kwa kicho, shangilieni kwa kutetemeka. Shikeni yaliyo bora, asije akafanya hasira nanyi mkapotea njiani, kwa kuwa hasira yake itawaka upesi; heri wote wanaomkimbilia.

Zaburi 3.

BWANA, watesi wangu wamezidi kuwa wengi, ni wengi wanaonishambulia. Ni wengi wanaoiambia nafsi yangu, Hana wokovu huyu kwa Mungu. Na Wewe, BWANA, U ngao yangu pande zote, utukufu wangu na mwinua kichwa changu. Kwa sauti yangu namwita BWANA naye aniitikia toka mlima wake mtakatifu. Nalijilaza nikalala usingizi, nikaamka, kwa kuwa BWANA ananitegemeza. Sitayaogopa makumi elfu ya watu, waliojipanga juu yangu pande zote. BWANA, uinuke, Mungu wangu, uniokoe, maana umewagiga taya adui zangu wote; umewavunja meno wasio haki. Wokovu una BWANA, baraka yako na iwe juu ya watu wako.

MSOMAJI

Utukufu kwa Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu.

MSOMAJI

Sasa na siku zote hata milele na milele. Amina.

Alleluia, Alleluia, Alleluia. Utukufu kwako, Ee Mungu. (3)

Bwana hurumia, Bwana hurumia, Bwana hurumia.

Utukufu kwa Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu.

MSOMAJI

Sasa na siku zote hata milele na milele. Amina.

Zaburi ya 4.

Ee Mungu wa haki yangu uniitikie niitapo; umenifanyizia nafasi wakati wa shida; unifadhili na kuisikia sala yangu. Enyi wanadamu, hata lini utukufu wangu utafedheka? Je! Mtapenda ubatili na kutafuta uongo? Bali jueni ya kuwa BWANA amejiteulia mtauwa; BWANA atasikia nimwitapo. Mwe na hofu wala umsitende dhambi; tafakarini vitandani mwenu na kutulia. Toeni dhabihu za haki, na kumtumaini BWANA. Wengi husema, Nani atakeyetuonyesha mema? BWANA, utuinulie nuru ya uso wako. Umenitia furaha moyoni mwangu, kupita yao wanapozidishiwa nafaka na divai. Katika amani nitajilaza na kupata usingizi mara, maana Wewe, BWANA, peke yako, ndiwe unijaliaye kukaa salama.

Zaburi ya 5.

Ee BWANA, uyasikilize maneno yangu, ukuangalia kutafakari kwangu. Uisikie sauti ya kilio changu, Ee Mfalme wangu na Mungu wangu, kwa maana Wewe ndiwe nikuombaye. BWANA, asubuhi utaisikia sauti yangu, asubuhi nitakupangia dua yangu na kutazamia. Maana huwi Mungu apendezwaye na ubaya; mtu mwovu hatakaa kwako. Wajivunao hawatasimama mbele za macho yako; unawachukia wote watendao ubatili. Utawaharibu wasemao uongo; BWANA humzira mwuaji na mwenye hila. Bali mimi, kwa wingi wa fadhili zako, nitaingia nyumbani mwako; na kusujudu kwa kicho, nikilielekea hekalu lako takatifu. BWANA, uniongoze kwa haki yako, kwa sababu yao wananaonitea. Uisawazishe njia yako mbele ya uso wangu, maana vinywani mwao hamna uaminifu; mtima wao ni shimo tupu, koo lao ni kaburi wazi, ulimi wao hujipendekeza. Wewe, Mungu, uwapatilize, na waanguke kwa mashauri yao. Uwatoe nje kwa ajili ya wingi wa makosa yao. Kwa maana wamekuasi Wewe. Nao wote wanaokukimbilia watafurahi; watapiga daima kelele za furaha. Kwa kuwa Wewe unawahifadhi, walipendao jina lako watakufurahia. Kwa maana Wewe utambariki mwenye haki; BWANA, utamzungushia radhi kama ngao.

Zaburi ya 6.

BWANA, usinikemee kwa hasira yako, wala usinirudi kwa ghadhabu yako. BWANA, unifadhili, maana ninanyauka; BWANA, uniponye, mifupa yangu imefadhaika. Na nafsi yangu imefadhaika sana; na Wewe, BWANA, hata lini? BWANA urudi, uniopoe nafsi yangu, uniokoe kwa ajili ya fadhili zako. Maana mautini hapana kumbukumbu lako; katika kuzimu ni nani atakayekushukuru? Nimechoka kwa kuugua kwangu; kila usiku nakieleza kitanda changu; nalilowesha godoro langu kwa machozi yangu. Jicho langu limeharibika kwa masumbufu, na kuchakaa kwa sababu yao wanaoniudhi. Ondokeni kwangu, ninyi nyote mtendao uovu; kwa kuwa BWANA ameisikia sauti ya kilio changu. BWANA ameisikia dua yangu; BWANA atakayetakabali maombi yangu. Adui zangu wote wataaibika na kufadhaika, watarudi nyuma, kwa ghafula wataaibika.

MSOMAJI

Utukufu kwa Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu.

MSOMAJI

Sasa na siku zote hata milele na milele. Amina.

Alleluia, Alleluia, Alleluia. Utukufu kwako, Ee Mungu. (3)

Bwana hurumia, Bwana hurumia, Bwana hurumia.

Utukufu kwa Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu.

MSOMAJI

Sasa na siku zote hata milele na milele. Amina.

Zaburi ya 7.

BWANA, Mungu wangu, nimekukimbilia Wewe, uniokoe na wote wanaonifuatia, uniponye. Asije akaipapura nafsi yangu kama simba, akiivunja-vunja pasipokuwa na wa kuponya. BWANA, Mungu wangu, ikiwa nimetenda haya, ikiwa mna uovu mikononi mwangu, ikiwa nimemlipa mabaya yeye aliyekaa kwangu salama; (hasha! Nimemponya yeye aliyekuwa mtesi wangu bila sababu;) basi adui na anifuatie, na kuikamata nafsi yangu; naam, aukanyage uzima wangu, na kuulaza utukufu wangu mavumbini. BWANA uondoke kwa hasira yako; ujiinue juu ya jeuri ya watesi wangu; uamke kwa ajili yangu; umeamuru hukumu. Kusanyiko la mataifa na likuzunguke, na juu yake uketi utawale. BWANA atawaamua mataifa, BWANA, unihukumu mimi, kwa kadiri ya haki yangu, sawasawa na unyofu nilio nao. Ubaya wao wasio haki na ukome, lakini umthibitishe mwenye haki. Kwa maana mjaribu mioyo na viuno ndiye Mungu aliye mwenye haki. Ngao yangu ina Mungu, awaokoaye wanyofu wa moyo. Mungu ni mwamuzi mwenye haki, naam, Mungu aghadhibikaye kila siku. Mtu asiporejea ataunoa upanga wake; ameupinda uta wake na kuuweka tayari; Naye amemtengenezea silaha za kufisha, akifanya mishale yake kuwa ya moto. Tazama, huyu ana utungu wa uovu, amechukua mimba ya madhara, amezaa uongo. Amechimba shimo, amelichimba chini sana, akatumbukia katika handaki aliyoifanya. Madhara yake yatamrejea kichwani pake; na dhulumu yake itamshukia utosini. Nitamshukuru BWANA kwa kadiri ya haki yake; nitaliimbia jina la BWANA aliye juu.

Zaburi ya 8.

Wewe, MUNGU, Bwana wetu, jinsi lilivyo tukufu jina lako dunia mwote! Wewe umeuweka utukufu wako mbinguni; vinywani mwa watoto wachanga na wanyonao umeiweka misingi ya nguvu; kwa sababu yao wanaoshindana nawe; uwakomeshe adui na mijilipiza kisasi. Nikiziangalia mbingu zako, kazi ya vidole vyako, mwezi na nyota ulizoziratibisha; mtu ni kitu gani hata umkumbuke, na binadamu hata umwangalie? Umemfanya mdogo punde kuliko Mungu; umemvika taji ya utukufu na heshima; umemtawaza juu ya kazi za mikono yako; umevitia vitu vyote chini ya miguu yake. Kondoo, na ng''ombe wote pia; naam, na wanyama wa kondeni; ndege wa angani, na samaki wa baharini; na kila kipitacho njia ya baharini. Wewe, MUNGU, Bwana wetu, jinsi lilivyo tukufu jina lako duniani mwote!

MSOMAJI

Utukufu kwa Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu.

Sasa na siku zote hata milele na milele. Amina.

Alleluia, Alleluia, Alleluia. Utukufu kwako, Ee Mungu. (3)

LITANIA FUPI

SHEMASI

Tena na tena kwa amani, tumwombe Bwana.

( Bwana, hurumia. )

Utusaidie, utuokoe, utuhurumie, utuhifadhi, Ee Mungu, kwa neema yako.

( Bwana, hurumia. )

Tumkumbuke Maria Mtakatifu kamili, asiye na doa, Mbarikiwa zaidi kushinda wote, Bibi wetu mtukufu mzazi Mungu na bikira daima pamoja na watakatifu wote hata sisi pia wenyewe na kila mmoja wetu na wenzetu wote, hata maisha yetu, kujiweka mikononi mwa Kristo Mungu.

( Kwako, Ee Bwana. )

KASISI

Kwa kuwa, utawala ni kwako na ufalme na uweza, na utukufu ni vyako, Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu, sasa na siku zote, hata milele na milele.

( Amina. )

Ahimidiwe Mungu wetu, daima, sasa na siku zote, hata milele na milele.

Zaburi ya 140 (141).

Ee Bwana nimekuita, unijie hima, unijie hima, Bwana. Ee Bwana nimekuita, unijie hima, uisikie sauti ya kilio changu, uisikie sauti yangu nikuitapo, Bwana. [[SWA]]

Sala yangu ipae mbele zako kama uvumba, Kuinuliwa mikono yangu kama dhabihu ya jioni; unijie hima, Bwana. . [[SWA]]

Ee BWANA, uweke mlinzi kinywani pangu, mngojezi mlangoni pa midomo yangu.

Usiuelekeze moyo wangu kunako jambo baya, nisiyazoelee matendo yasiyofaa,

pamoja na watu watendao maovu; wala nisile vyakula vyao vya anasa.

Mwenye haki na anipige, itakuwa fadhili; anikemee, itakuwa kama mafuta kichwani; kichwa changu kisikatae,

maana siachi kusali kati ya mabaya yao. Makadhi yao wakiangushwa kando ya genge,

watayasikia maneno yangu, maana ni matamu. Kama kupasua kuni na kuzichanja juu ya nchi, ndivyo ilivyo mifupa yetu mdomoni pa kuzimu.

Macho yangu yanakuelekea Wewe, MUNGU Bwana, nimekukimbilia Wewe, usiniache nafsi yangu.

Unilinde na mtego walionitegea, na matanzi yao watendao maovu.

Wabaya na waanguke katika nyavu zao wenyewe, pindi mimi ninapopita salama.

Zaburi ya 141 (142).

Kwa sauti yangu nitamlilia BWANA, kwa sauti yangu nitamwomba BWANA dua.

Nitafunua mbele zake malalamiko yangu, shida yangu nitaitangaza mbele zake.

Nilipozimia roho uliyajua mapito yangu;

katika njia niendayo wamenifichia mtego.

Utazame mkono wa kuume ukaone, kwa maana sina mtu anijuaye.

Makimbilio yamenipotea, hakuna wa kunitunza roho.

BWANA, nimekuita nikasema, Ndiwe kimbilio langu, fungu langu katika nchi ya walio hai.

Ukisikilize kilio changu, kwa maana nimedhilika sana.

Uniponye nao wanaonifuatia, kwa maana wao ni hodari kuliko mimi.

Zaburi ya 129 (130).

Ee Bwana, toka vilindini nimekulilia; Bwana, [[SWA]]

BWANA, kama Wewe ungehesabu maovu, Ee Bwana, nani angesimama? Lakini kwako kuna msamaha, [ili Wewe uogopwe]. [[SWA]]

Nimemngoja BWANA, roho yangu imengoja, na neno lake nimelitumainia. Nafsi yangu inamngoja Bwana, [[SWA]]

Kutoka makesha ya asubuhi hadi usiku, [[SWA]]

Maana kwa Bwana kuna fadhili, na kwake [[SWA]]

Zaburi ya 116 (117).

Msifuni Bwana enyi mataifa yote, msifuni [[SWA]]

Maana fadhili zake zimo juu yetu milele, na [[SWA]]

Utukufu kwa Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu. Sasa na siku zote hata milele na milele. Amina.

SHEMASI

Tumwombe Bwana.

Ombi la Kuingia.

KASISI

Jioni, asubuhi na adhuhuri twakusifu, twakuhimidi, twakushukuru na twakuomba, Ee Rabi wa wote, Bwana mpenda wanadamu. Elekeza maombi yetu mbele zako kama uvumba, na mioyo yetu isipotoshwe kwenye maneno namafikira maovu, utuokoe kwa kila jaribio rohoni mwetu; kwa kuwa macho yetu yaelekea kwako ewe Bwana na tumekukimbilia wewe, usituambishe, Ee Mungu wetu, (kwa sauti):Kwa kuwa utukufu wote na heshima na usujudu ni haki yako, Baba na Mwana na Roho Mtaktifu, sasa na siku zote hata milele na milele.

Kwa kuwa utukufu wote na heshima na usujudu ni haki yako, ya Baba na Mwana na Roho Mtakatifu, sasa na siku zote, hata milele na milele.

SHEMASI

Ee padri, bariki kuingia kutakatifu.

KASISI

SHEMASI

Amina.

Hekima. Simameni wima.

We Nuru ya furaha ya utukufu mtakatifu, ya Baba usiyekufa, wa mbinguni, mtakatifu, mhimidiwa, Yesu Kristo! Tukiwa tumefika wakati wa kuchwa kwa jua na kuona mwanga wa jioni tunamwimbia Baba, Mwana na Roho Mtakatifu Mungu. Ni wajibu wakati wote usifiwe kwa sauti safi, Ee Mwana wa Mungu, mpaji wa uhai; kwa hivyo dunia ya kutukuza. [[SWA]]

SHEMASI

Jioni prokimeno.

Zaburi Sauti ya 6.

BWANA ametamalaki, amejivika adhama, [[SWA]]

Mstari BWANA amejivika, na kujikaza nguvu.

BWANA ametamalaki, amejivika adhama, [[SWA]]

Mstari Naam, ulimwengu umethibitika usitikisike;

BWANA ametamalaki, amejivika adhama, [[SWA]]

Zaburi

Tazama, enyi watumishi wa BWANA, mhimidini BWANA, nyote pia. Ninyi mnaosimama usiku katika nyumba ya BWANA. (x 2)

Mstari

Tazama, enyi watumishi wa BWANA, mhimidini BWANA, nyote pia.

Ninyi mnaosimama usiku katika nyumba ya BWANA.

Zaburi Sauti 4.

BWANA atasikia nimwitapo.

Mstari Ee Mungu wa haki yangu uniitikie niitapo; umenifanyizia nafasi wakati wa shida;

Zaburi Sauti 1

Mstari BWANA ndiye mchungaji wangu, sitapungukiwa na kitu.

Zaburi Sauti 5.

Mstari Ee Mungu, uyasikie maombi yangu, uyasikilize maneno ya kinywa changu.

Zaburi Sauti ya 6.

Mstari Nitayainua macho yangu niitazame milima, msaada wangu utatoka wapi?

Zaburi Sauti ya 7

Mstari Ee Mungu wangu, uniponye na adui zangu, uniinue juu yao wanaoshindana nami.

LITANIA NDEFU (EKTENI)

SHEMASI

Tuseme sisi sote kwa roho yetu na kwa mawazo yetu yote tuseme hivi.

WATU

Bwana, hurumia.

SHEMASI

Ee Bwana Mwenyezi Mungu wa mababu wetu tunakuomba utusikilize na kutuhurumia.

WATU

Bwana, hurumia.

SHEMASI

Utuhurumie, Ee Mungu kadiri ya huruma yako kubwa, tunakuomba utusikilize na kutuhurumia.

WATU

Bwana, hurumia. (3)

SHEMASI

Tena tunaomba kwa ajili ya Askofu wetu mkuu (jina)

Tena tunakuomba kwa ajili ya huruma, uzima, amani, afya, wokovu, ulinzi, msamaha na maondoleo ya dhambi kwa watumishi wa Mungu, walinzi wasimamizi na washiriki wa Kanisa hili takatifu.

Tena tunakuomba kwa ajili ya warehemiwa wajengaji wa kanisa hili takatifu, ambao ni kwa makumbusho ya daima ya baba na ndugu zetu wote wa Orthodoksi warehemiwa, ambao wamelala hapa na mahali popote.

Tena tunakuomba kwa ajili yao wanaotenda matendo mema katika nyumba hii takatifu na heshimiwa, kwa ajili yao wenye juhudi, wanaoimba, hata ya watu wote wanaosimama hapa, wakingoja huruma yako kubwa na utajiri.

KASISI

Kwa kuwa U Mungu mrahimu na mpenda wanadamu, na kwako tunatoa utukufu, kwa Baba na Mwana na Roho Mtakatifu, sasa na siku zote hata milele na milele.

WATU

Amina.

MSOMAJI

Ee Bwana, utujalie, jioni hii tusiwe na dhambi, Wahimidiwa, Ee Bwana, Mungu wa baba zetu, na jina lako limesifiwa na limetukuzwa milele. Amina. Ee Bwana, huruma yako iwe nasi, tunavyokutumaini wewe. Wahimidiwa, Ee Bwana; unifundishe zilizo haki zako. Wahimidiwa, Ee Rabi; unifahamishe zilizo haki zako. Wahimidiwa, Ee Mtakatifu; uniangaze kwa zilizo haki zako. Ee Bwana, huruma yako niya milele; usidharau viumbe vya mikono yako. Sifa ni zako, kukuimbia ni kwako na utukufu ni wako, wa Baba na Mwana, na Roho Mtakatifu, sasa na siku zote, hata milele na milele. [[SWA]]

( Amina. )

SHEMASI

Tumalize maombi yetu ya jioni kwa Bwana.

Bwana, hurumia.

SHEMASI

Utusaidie, utuokoe, utuhurumie, utuhifadhi, Ee Mungu, kwa neema yako.

Bwana, hurumia.

SHEMASI

Jioni hii yote iwe kamili, takatifu, tulivu na bila dhambi, tuombe kwa Bwana.

Kidhi, Ee Bwana.

SHEMASI

Kwa ajili ya kuwa na Malaika wa amani, mwongozi mwaminifu, mlinzi wa roho zetu na miili yetu, tuombe kwa Bwana.

Kidhi, Ee Bwana.

SHEMASI

Kwa ajili ya msamaha na maondoleo ya dhambi zetu na makosa yetu, tuombe kwa Bwana.

Kidhi, Ee Bwana.

SHEMASI

Kwa ajili ya vitu vyema vifaavyo kwa roho zetu na amani ya dunia yote, tuombe kwa Bwana.

Kidhi, Ee Bwana.

SHEMASI

Kwa ajili ya kumaliza maisha yetu yanayobaki kwa amani na toba, tuombe kwa Bwana.

Kidhi, Ee Bwana.

SHEMASI

Tuombe ili mwisho wa maisha yetu uwe wa kikristo kwa amani, bila maumivu, aibu, tena tuone teto njema mbele ya kiti cha hukumu cha Kristo.

Kidhi, Ee Bwana.

SHEMASI

Tumkumbuke Maria Mtakatifu kamili, asiye na doa, Mbarikiwa zaidi kushinda wote, Bibi wetu mtukufu mzazi Mungu na bikira daima pamoja na watakatifu wote hata sisi pia wenyewe na kila mmoja wetu na wenzetu wote, hata maisha yetu, kujiweka mikononi mwa Kristo Mungu.

Kwako, Ee Bwana.

KASISI

Kwa kuwa U Mungu Mwema na mpenda wanadamu, na kwako tunatoa Utukufu, kwa Baba na Mwana na Roho Mtakatifu, sasa na siku zote, hata milele na milele.

Amina.

Amani kwa wote.

Na iwe kwa roho yako.

SHEMASI

Tuinamishe vichwa vyetu kwa Bwana.

Kwako, Ee Bwana.

KASISI (kwa mnong''ono)

Ee Bwana Mungu wetu, uliyeinamisha mbingu na kuja duniani kwa ajili ya wokovu wa wanadamu; tazama watumishi wako na urithi wako. Kwa kuwa watumishi wako wameinama vichwa vyao na shingo zao kwako,uliye Mungu wa kutisha na mpenda– wanadamu, wakiwa hawatumaini msaada kutoka kwa mtu, lakini wategemea huruma yako tena watazamia wokovu wako. Uwatunze wakati wote tena katika jioni hii na usiku ujao waweze kushinda madui wao wote, vitendo vyo vyote vya shetani, mawazo ya bure na kufahamu uovu.

KASISI

Uhimidiwe na Ubarikiwe, utukufu wa Ufalme wako, wa Baba, na Bwana, na Roho Mtakatifu, sasa na siku zote, hata milele na milele.

Amina.

Mstari Bwana ametamalaki; amejivika adhama; [[SWA]]

Mstari Kwa kuwa amekaza nchi ili isitikisike. [[SWA]]

Mstari Utakatifu umekuwa nyumba yako Ee Bwana [[SWA]]

Wimbo wa Simeoni.

Maombi ya Trisaghio.

Mungu Mtakatifu, Mweza Mtakatifu, Usiyekufa Mtakatifu, utuhurumie. (3)

Utukufu kwa Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu. Sasa na siku zote hata milele na milele. Amina.

Ee Utatu mtakatifu kamili, utuhurumie. Bwana, utusamehe dhambi zetu. Rabi, utuondolee makosa yetu. Mtakatifu, utukaribie na kutuponya magonjwa yetu, kwa ajili ya jina lako.

Bwana hurumia, Bwana hurumia, Bwana hurumia.

Utukufu kwa Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu. Sasa na siku zote hata milele na milele. Amina.

Baba yetu uliye Mbinguni; Jina lako litukuzwe; Ufalme wako uje; mapenzi yako yatimizwe, hapa Duniani kama huko Mbinguni. Utupe leo mkate wetu wa kila siku; na utusamehe deni zetu; kama sisi tuwasamehevyo wadeni wetu; tena usitutie majaribuni, lakini tuokoe na yule mwovu. [[SWA]]

KASISI

Kwa kuwa ufalme ni wako, na nguvu, na utukufu, wa Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu, sasa na siku zote hata milele na milele.

SHEMASI

Hekima.

( Ee Padri mtakatifu bariki. )

KASISI

Aliye himidiwa Kristo Mungu wetu, daima sasa na siku zote hata milele na milele.

WATU

Amina.

/MSOMAJI

Bwana, Mungu imarisha, imani Takatifu isiyo na lawama ya wakristo watawa wa Orthodoksi, na hili Kanisa Takatifu na mji huu, hata milele na milele.

( Amina. )

Uliye wa thamani kushinda waheruvi, uliye na utukufu kuwapita bila kiasi waserafi, uliyemzaa Mungu neno, umebaki bila kukuharibu, uliye mzazi-Mungu kweli tunakutukuza we.

Utukufu kwa Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu. Sasa na siku zote hata milele na milele. Amina.

Bwana, hurumia. (3) Ee Padri mtakatifu bariki.

Yeye ( aliyefufuka toka kwa wafu, ) Kristo Mungu wetu wa kweli, kwa maombi ya Mama yake asiye na doa na asiye na waa, mtakatifu kamili; kwa nguvu ya msalaba wenye thamani na mpaji wa uhai; kwa ulinzi wa nguvu zisizo na mwili waheshimiwa wa mbinguni; kwa maombi ya Yohana, Nabii, mtangulizi na mbatizaji, mheshimiwa na wa sifa; ya Mitume watakatifu, watukufu na wasifiwa; ya mashahidi watakatifu, wasifiwa na washindaji wazuri; ya watawa watakatifu na wacha Mungu; (Mtakatifu wa Kanisa); ya watakatifu na wenye haki Yohakim na Anna; na ya watakatifu wote, atuhurumie na atuokoe, yu Mungu mwema, mrahimu na mpenda wanadamu.

KASISI

Kwa maombi ya mababa wetu watakatifu, Ee Bwana Yesu Kristo Mungu wetu, utuhurumie na utuokoe.

WATU

Amina.

1.

Apolitikia.

Utukufu.

Sasa.

MSOMAJI

Bwana, hurumia. (x 40)

Utukufu kwa Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu. Sasa na siku zote hata milele na milele. Amina.

Uliye wa thamani kushinda waheruvi, uliye na utukufu kupita bila kiasi waserafi, uliyemzaa Mungu Neno na umebaki bikira, uliye Mzazi-Mungu kweli, tunakutukuza we.

Bwana, hurumia. Bwana, hurumia. Bwana, hurumia. Ee padri mtakatifu, bariki.

KASISI

Aliye himidiwa Kristo Mungu wetu, daima sasa na siku zote hata milele na milele.

MSOMAJI

Amina.

Ee Mfalme wa mbinguni, imarisha viongozi wetu waaminifu; adilisha imani, patanisha nchi, ipe dunia yote amani; linda hili kanisa Takatifu na mji huu; weka wazazi wetu na ndugu zetu walioaga dunia hii mahala pa walio haki; na kwa uzuri wako na huruma tupokee nasi pia katika kutubu na kuungama kama Bwana mpenda wanadamu.

Ee Maulana na Bwana wa uhai wangu, itoe roho yangu katika maisha ya uvivu, usumbufu, tamaa mbaya, pamoja na mazungumzo yasio na faida. ( )

Niridhie, mstumishi wako, roho ya busara, unyenyekevu, uvumilivu na upendo. ( )

Naam, Bwana na Mfalme; nifanye kuona makosa yangu, na wala sio kuhukumu ndungu yangu. ( )

2.

MAOMBI YA JIONI (VESPERS)

Mstari 1: Nimekuinulia macho yangu, Wewe uketiye mbinguni. Kama vile macho ya watumishi kwa mkono wa bwana zao, kama macho ya mjakazi kwa mkono wa bibi yake; hivyo macho yetu humwelekea BWANA, Mungu wetu, hata atakapoturehemu.

Mstari 2: Uturehemu, Ee BWANA, uturehemu sisi, kwa maana tumeshiba dharau. Nafsi zetu zimeshiba mzaha wa wenye raha, na dharau ya wenye kiburi.

Mstari 1: Mungu ni mwenye kutisha kutoka patakatifu pako.

Mstari 2: Watakatifu waliopo duniani ndio walio bora, hao ndio niliopendezwa nao.

Mstari 3: Heri mtu yule umchaguaye, na kumkaribisha akae nyuani mwako.

Yeye Kristo Mungu wetu wa kweli, kwa maombi ya Mama yake asiye na doa na asiye na waa, mtakatifu kamili; kwa ulinzi wa nguvu zisizo na mwili waheshimiwa wa mbinguni; ya Mitume watakatifu, watukufu na wasifiwa; (Mtakatifu wa Kanisa); ya watakatifu na wenye haki Yohakim na Anna; na ya watakatifu wote, atuhurumie na atuokoe, yu Mungu mwema, mrahimu na mpenda wanadamu.

Yeye Kristo Mungu wetu wa kweli, kwa maombi ya Mama yake asiye na doa na asiye na waa, mtakatifu kamili; kwa maombi ya Yohana, Nabii, mtangulizi na mbatizaji, mheshimiwa na wa sifa; ya Mitume watakatifu, watukufu na wasifiwa; (Mtakatifu wa Kanisa); ya watakatifu na wenye haki Yohakim na Anna; na ya watakatifu wote, atuhurumie na atuokoe, yu Mungu mwema, mrahimu na mpenda wanadamu.

Yeye Kristo Mungu wetu wa kweli, kwa maombi ya Mama yake asiye na doa na asiye na waa, mtakatifu kamili; kwa nguvu ya msalaba wenye thamani na mpaji wa uhai; ya Mitume watakatifu, watukufu na wasifiwa; (Mtakatifu wa Kanisa); ya watakatifu na wenye haki Yohakim na Anna; na ya watakatifu wote, atuhurumie na atuokoe, yu Mungu mwema, mrahimu na mpenda wanadamu.

Yeye Kristo Mungu wetu wa kweli, kwa maombi ya Mama yake asiye na doa na asiye na waa, mtakatifu kamili; ya Mitume watakatifu, watukufu na wasifiwa; ya mashahidi watakatifu, wasifiwa na washindaji wazuri; ya watawa watakatifu na wacha Mungu; (Mtakatifu wa Kanisa); ya watakatifu na wenye haki Yohakim na Anna; na ya watakatifu wote, atuhurumie na atuokoe, yu Mungu mwema, mrahimu na mpenda wanadamu.

[ ]

[ ]

[ ]

[ ]

SAA YA TISA

Wimbo wa Ufufuo

Apostika.

Kathisma.

Zaburi

Wimbo wa Mzazi-Mungu

Tropario.