×




SKARAMENTI YA NDOA TAKATIFU


IBADA YA PETE

SHEMASI

Ee padri, himidi.

KASISI

Ahimidiwe Mungu wetu, daima, sasa na siku zote, hata milele na milele.

( Amina. )

SHEMASI

Kwa amani, tumwombe Bwana.

( Bwana, hurumia. )

Kwa ajili ya amani kutoka juu na ya wokovu wa roho zetu, tumwombe Bwana.

Kwa ajili ya amani ya dunia yote, na kusimama imara kwa Ekklesia Takatifu ya Mungu, na ya umoja wa wote, tumwombe Bwana.

Kwa ajili ya nyumba hii takatifu na waingiamo kwa imani, heshima na kumcha Mungu, tumwombe Bwana.

Kwa ajili ya Askofu wetu mkuu (J) makasisi, mashemashi wetu wateule na ya watu wote, tumwombe Bwana.

Kwa ajili ya watumishi wa Mungu (J) na (J) ambao kwa Sasa wanaozwa na kwa wokovu wao,tumwombe Bwana.

Ili wapate pendo kamilifu na la amani na msaada wa Mungu,tumwombe Bwana.

Ili watunzwe na wabarikiwe na umoja wa fikira na imani timilifu, tumwombe Bwana.

Ili wadumishwe kwa mwenendo bora na maisha yasiyo na lawama, tumuombe Bwana.

Ili Bwana Mungu wetu awape ndoa yenye heshima isiyo na lawama, tumuombe Bwana.

Kwa ajili ya kuokolewa kwa kila sitikiko, ghadhabu, hatari na uhitaji, tumwombe Bwana.

Utusaidie, utuokoe, utuhurumie, utuhifadhi, Ee Mungu, kwa neema yako.

Tumkumbuke Maria Mtakatifu kamili, asiye na doa, Mbarikiwa zaidi kushinda wote, Bibi wetu mtukufu mzazi Mungu na bikira daima pamoja na watakatifu wote hata sisi pia wenyewe na kila mmoja wetu na wenzetu wote, hata maisha yetu, kujiweka mikononi mwa Kristo Mungu.

( Kwako, Ee Bwana. )

Kwa kuwa utukufu wote na heshima na usujudu ni haki yako, ya Baba na Mwana na Roho Mtakatifu, sasa na siku zote, hata milele na milele.

( Amina. )

SHEMASI

Tumwombe Bwana.

( Bwana, hurumia. )

KASISI

Ee Mungu wa milele, uliyefanya watu waliotengana kuwa na umoja, na ukaanzisha uelewano usiovunjika kwao; na ukawabariki Isaka na Rebeka na kuwafanya warithi wa hadi, yako: Wabariki hawa watumishi wako (jina) na (jina) na uwaongoze kwa kila kazi njema.

Kwa kuwa U Mungu mrahimu na mpenda wanadamu, na kwako tunatoa utukufu, kwa Baba na Mwana na Roho Mtakatifu, sasa na siku zote hata milele na milele.

( Amina. )

Amani kwa wote.

( Na iwe kwa roho yako. )

SHEMASI

Tuinamishe vichwa vyetu kwa Bwana.

( Kwako, Ee Bwana. )

KASISI

Ee Bwana Mungu wetu, unayelifanya Kanisa kuwa bikira asiye na ndoa toka kwa mataifa yote; ubariki pete hizi na uwaunganishe na uwahifadhi watumish (majina) wako, kwa amani na mapatano.

Kwa kuwa utukufu wote na heshima na usujudu ni haki yako, ya Baba na Mwana na Roho Mtakatifu, sasa na siku zote, hata milele na milele.

( Amina. )

Mtumishi wa Mungu (Jina) anatoa ahadi kumuoa mtumishi wa Mungu (Jina), kwa jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu. ( Amina. ) (3)

Mtumishi wa Mungu (jina) anaahidi kuolewa na mtumishi wa Mungu (Jina), kwa jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu. ( Amina. ) (3)

SHEMASI

Tumwombe Bwana.

( Bwana, hurumia. )

KASISI

Ee Bwana Mungu wetu, uliyeambatana na mtumishi wa Ibrahimu kwenda Mesopotamia, ambapo alikuwa ametumwa kumtafuta mchumba wa Isaka, kwenye kisima alichoonyeshwa kwamba ni sharti kumposa Rebeka kama mchumba. Bariki uchumba wa hawa watumishi wako (Majina), na imarisha ahadi ambazo wameahidiana kwa umoja wa utakatifu, kwa kuwa tangu mwanzo uliwaumba Mme na Mke, na kwa mapenzi yako Mke anaungana na Mme kusaidiana na kuendeleza ubinadamu. Ndiwe uliyetuma ukweli wako na urithi wako na ahadi yako kwa watumishi wa Baba zetu, na wateule wako kutoka kizazi hata kiazi, watunze hawa watumishi wako jina (majina) na uimarishe ndoa yao kwa imani, mapatano, ukweli na upendo; kwa kuwa wee Bwana ndiwe ulitufunza kufunga harusi kwa ahadi ya pete na kuaminiana kwa kila jambo. Kutokana na pete, Yusufu alipewa madaraka katika nchi ya Misiri. Kwa kutumia pete, Danieli alitukuzwa katika Babiloni; Damari alitambuliwa kuwa na haki, kutokana na pete. Baba yetu wa Mbinguni alionyesha huruma kwa Mwana mpotevu; akisema "Weka Pete kwenye kidole chake na umlete Dume aliyenona achinjwe ili tule na kushangilia. Ee Bwana mkono wa kuume ulimwenzesha Musa kuvuka bahari ya Sham, kwa maneno yako ya ukweli, mbingu zilimarishwa na nchi kubwa; uwambariki hawa waumishi wako kwa mkono wako wa kuume. Sasa Ee, Bwana kwa baraka za mbinguni, bariki kuvalishana huku na Pete. Malaika wa Bwana awe nao katika maisha yao yote.

( Amina. )


IBAADA YA TAJI

Zaburi ya 127 (128).

KASISI

WATU

Utukufu kwako, Ee Mungu wetu, utukufu

KASISI

WATU

Utukufu kwako, Ee Mungu wetu, utukufu

KASISI

WATU

Utukufu kwako, Ee Mungu wetu, utukufu

KASISI

WATU

Utukufu kwako, Ee Mungu wetu, utukufu

KASISI

WATU

Utukufu kwako, Ee Mungu wetu, utukufu

KASISI

WATU

Utukufu kwako, Ee Mungu wetu, utukufu

Tazama, atabarikiwa hivyo, yule amchaye BWANA.

WATU

Utukufu kwako, Ee Mungu wetu, utukufu

BWANA akubariki toka Sayuni; uone uheri wa Yerusalemu siku zote za maisha yako;

WATU

Utukufu kwako, Ee Mungu wetu, utukufu

naam, ukawaone wana wa wanao. Amani ikae na Israeli.

WATU

Utukufu kwako, Ee Mungu wetu, utukufu

SHEMASI

Ee padri, himidi.

KASISI

Mhimidiwa ni Ufalme wa Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu, sasa na siku zote hata milele na milele.

( Amina. )

SHEMASI

Kwa amani, tumwombe Bwana.

( Bwana, hurumia. )

Kwa ajili ya amani kutoka juu na ya wokovu wa roho zetu, tumwombe Bwana.

Kwa ajili ya amani ya dunia yote, na kusimama imara kwa Ekklesia Takatifu ya Mungu, na ya umoja wa wote, tumwombe Bwana.

Kwa ajili ya nyumba hii takatifu na waingiamo kwa imani, heshima na kumcha Mungu, tumwombe Bwana.

Kwa ajili ya Askofu wetu mkuu Askofu wetu mkuu (jina) Makasisi, Mashemasi wateule na watu wote tumwombe Bwana.

Kwa ajili ya watumishi wa Mungu (majina) ambao wanaunganishwa kwa ndoa na kwa ajili ya wokovu wao, tumuombe Bwana.

Ili hii ndoa ibarikiwe kama iliyokuwepo Kana ya Galilaya, tumuombe Bwana.

Ili wapewe hukumu ya utu na watoto kwa manufaa yao, tumuombe Bwana.

Ili wajazwe kwa furaha wakiwaona wavulana na wasichana, tumuombe Bwana.

Ili wambarikiwe na watoto wema na maisha ya haki, tumuombe Bwana.

Ili Mungu apokee maombi ya wokovu wetu, tumuombe Bwana.

Utusaidie, utuokoe, utuhurumie, utuhifadhi, Ee Mungu, kwa neema yako.

Tumkumbuke Maria Mtakatifu kamili, asiye na doa, Mbarikiwa zaidi kushinda wote, Bibi wetu mtukufu mzazi Mungu na bikira daima pamoja na watakatifu wote hata sisi pia wenyewe na kila mmoja wetu na wenzetu wote, hata maisha yetu, kujiweka mikononi mwa Kristo Mungu.

( Kwako, Ee Bwana. )

Kwa kuwa utukufu wote na heshima na usujudu ni haki yako, ya Baba na Mwana na Roho Mtakatifu, sasa na siku zote, hata milele na milele.

( Amina. )

SHEMASI

Tumwombe Bwana.

( Bwana, hurumia. )

KASISI

Ee Mungu usiye na doa, muumba wa vitu vyote kwa upendo wako kwa mwanadamu ulimuumba Eva kwa Ubavu wa babu yetu Adamu na ukawabariki ukisema " Zaeni makaongezeke mkaijze nchi na mkaitawale." nawe ukawafanya wote kuwa kitu kimoja kwa kuwaunganisha kwa hivyo Mme atawaacha Baba na mama na kuambatana na mke nao watakuwa mwili mmoja na yale ambayo umeunganisha, mwanadamu asiwatenganishe. Ulimpatia Sara kwa Ibrahimu na ukawabariki kuwapa mtoto na kumafanya Baba wa mataifa. Uliunganisha Isaka na Rebeka na ukawabariki kwa kuwapa mtoto, pia ulinganisha Yakobo na Recho na kwao mababu kumi na wawili wakazaliwa; uliwaunganisha Yosifu na Asenati na ukawapa Ephraim na Manasseh kama watoto wao, uliitikia Zacharia na Elizabeth na ukamfanya Mwana wao kuwa mtangulizi, na kwa uzao wa Jesee ilimteua Bikira Maria ambapo ulizawa ukiwa mtu asilikwa wokovu wa mwandamu, kwa neema yako isiyoelezeka na wema wako ulisafiri huko Kana ya Galilaya ukabariki harusi huko; kwa uzao wa watoto ni kwa mapenzi yako. Kwako Ee Bwana Mtakatifu wa wote; uyakubali maombi yetu na jinsi ulivyokuwa huko na pia uwe nasi hapa kwa kutoonekaana kwako.Ibariki ndoa hii na uwape watumishilifu wako (majina) maisha ya furaha miaka ming, hukumu timilifu mapenzi kati yao na umoja wa amani, maisha marefu, neema kwa watoto wao na taji ya utukufu wa milele - uwawezeshe kuwaona wajukuu wao. Dumisha ndoa yao isiabke na uwape baraka toka mbinguni na utajiri wa ulimwengu. Ijaze nyumba yao kwa ngano, divai na chote kilichochema, ili waweze kuwasaidia wale wanaohitaji. Na utustahilishe sisi tulioko hapa kwa maombi yanayotuongoza kwa wokovu.

( Amina. )

SHEMASI

Tumwombe Bwana.

( Bwana, hurumia. )

KASISI

Uhimidiwe Ee Bwana Mungu wetu uliye mwidhinishaji wa ibada hii ya Ndoa (Sakramenti) takatifu, uliye mchungaji mwema wa zawadi ya maisha haya. Mwanzoni Ee Bwana uliumba mtu, ukamfanya kuwa kiongozi katika ulimwengu ukisema "Si vyema Mme kuwa peke yake, nitamfanya mzaidizi wa kufanana naye". Kwa kutoa ubavu wake mmoja ulimuumba Eva hapo Adamu alipomuona alisema,"Sasa huyu ni mfupa wangu, basi ataitwa mwanamke, kwa maana ametawaliwa na mwnaume ataawacha Baba na Mama na kuambatana na mkewe, nao watakuwa mwile mmoja na wale ambao wameunganishwa na Mungu, mwanadamu asiwatenganishe. Ee Bwana Mungu wetu, shukisha neema yako toka Mbinguni kwa hawa watumishi wako (majina). Fanya bibi harusi kuwa mtiifu kwa Mmewe, na huyu mtumishi ako awe kiongozi wa Mke, ili waishi kwa mapenzi yako. Wambariki Bwana Mungu wetu jinsi ulivyowabariki Abraham na Sara, Isaka na Rebeka, Yakobo na Recho nao wengine kama Yosefu na Asenati, Musa na Zipora, Yoakim na Anna, Zakaria na Elizabeth. Walinde kama vile ulivylimlinda Nuhu kwenya Safina, Yona tumboni mwa Nyangumi nao vijana watatu watakatifu toka motoni. Wabariki kwa baraka za mbinguni na uwajaze kwa furaha kuu kama ile iliyo mjaa Helena alipoupata Msalaba wenye dhamana. Wakumbuke kama ulivyowakumbuka Enoka Shem Eliya na pia mashahidi Arobaini waliyotunukia taji la mbinguni, uwakumbuke Ee Bwana Mungu, wazazi walio walea, kwa baraka zao wazazi imarisha msingi wa nyumba yao. Bwana Mungu watumishi wako wote walioko hapa wanao hudhuria ndoa hii. Wakumbuke Bwana ba Bibi arusi (majina) na uwabariki kwa uzao wa watoto wema, na miili na mioyo yao iwe kitu kimoja. Watukuze kama miche ya Lebanoni iliyo mizabibu ya kupendeza, waweze kuaona wajukuu wao miti mipya ya mizeituni iliyopandwa kuzingira meza yao. Waing''aishe kama nyota za mbinguni; kwako tunatoa utukufu, utawala, heshima na usujudu; ni haki yako sasa na siku zote hata milele na milele

( Amina. )

SHEMASI

Tumwombe Bwana.

( Bwana, hurumia. )

KASISI

Mungu Mtakatifu uliye muumba mtu kwa udongo na Mwanamke kwa ubavu wake na kuwaunganisha kwake awe msaidizi wake. Kwa vile kulionekana kwamba Mme asiwe peke yake ulimwenguni, Nyoosha mkono wako toka kwenye makao yako matakatifu na uwaunganishe hawa watumishi wako (Majina) pamoja kwa ajili hiyo Mke ataungana na Mme. Waunganishe katika fikira moja, wavike taji ya pingu za maisha katika mwili mmoja; wajalie uzao wa tumbo, na kuwepo kwa watoto wsenye baraka.

Kwa kuwa, utawala ni kwako na ufalme na uweza, na utukufu ni vyako, Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu, sasa na siku zote, hata milele na milele.

( Amina. )

KASISI

Mtumishi wa Mungu (jina) anvikwa Taji na mtumishi wa Mungu (Jina), kwa jina la Baba na la Mwana na Roho Mtakatifu, Kwa jina la Baba na Mwana na Roho Mtakatifu. ( Amina. ) (3)

Kwa kuwa utawala ni wako na ufalme na uweza na utukufu, ni wa Baba na Mwana na Roho Mtakatifu, sasa na siku zote hata milele na milele. Kwa jina la Baba na Mwana na Roho Mtakatifu. ( Amina. ) (3)

Wavike taji Ee Bwana Mungu wetu, kwa heshima na utukufu wako. x 3. [[SWA]]

MASOMO

SHEMASI

Tusikilize.

Zaburi Zaburi ya 20 (21).

MSOMAJI

Mstari

SHEMASI

Hekima.

MSOMAJI

Somo kutoka kwa

SHEMASI

Tusikilize.

MSOMAJI

(5: 20-33)

Ndugu zangu, mshukuruni Mungu Baba daima kwa ajili ya yote, kwa jina la Bwana wetu Yesu Kristo. Kila mmoja amstahili mwenzake kwa sabau ya kumcha Kristo. Wake watii waume wao kama kumtii Bwana. Maana Mme anayo mamlaka juu ya mkewe, kama vile Kristo alivyo na mamlaka juu ya Kanisa; naye Kristo mwenyewe hulikomboa Kanisa, mwili wake kama vile kanisa linavyomtii Kristo vivyo hivyo, wake wawatii waume zao katika mambo yote nanyi waume wapendeni wake zenu kama Kristo alivyo penda Kanisa, akajitoa mwenyewe Sadaka kwa ajili yake. Alifanya hivyo, ili kwa neno lake, aliweke wafu kwa Mungu, baada ya kulifanya safi kwa kuliosha kaika maji, kusudi aliache lililo takatifu na safi kabisa, Kanisa lisilo na doa, kasoro au chochote cha namna hiyo. Basi, waume wanapaswa kuwapenda wake zao kama miili yao wenyewe. (Hakuna mtu yeyote auchukiaye mwili wake. Badala ya kuuchukia, huulisha na kuuvika. Ndivyo na ye Kristo anavyolitunza Kanisa, maana sisi ni viungo vya mwili wake) kama yasemavyo maandiko matakatifu: "Kwa hiyo mwanaumme atamuacha Baba na Mama yake, ataungana na mkewe nao wawili watakua mwili mmoja" Kwa ukweli uliyofichika katika maneno haya, nami naona kwamba yamhusu Kristo na Kanisa lake. Lakini yanawahusu ninyi pia. Kila Mme lazima ampende Mkewe kama nafsi yake mwenyewe, naye Mke anapashwa kumheshimu Mmewe. [[SWA]]

KASISI

Amani kwako Ee Msomaji.

MSOMAJI

Na iwe kwa roho yako.

WATU

Alleluia.

Alleluia, Alleluia, a|leluia. [[SWA]]

Mstari 1:

Alleluia, Alleluia, a|leluia. [[SWA]]

Mstari 1:

Alleluia, Alleluia, a|leluia. [[SWA]]

SHEMASI

Hekima. Simameni wima. tusikilize Evanjelio Takatifu.

KASISI

Amani kwa wote.

( Na iwe kwa roho yako. )

Injili Takatifu kama ilivyoandikwa na

SHEMASI

Tusikilize.

( Utukufu kwako, Ee Bwana, utukufu kwako. )

Siku ya tatu kulikuwa na harusi mjini Kana, mkoani Galilaya. Mama yake Yesu alikuwapo, naye Yesu alikuwa amealikwa harusini pamoja na wanafunzi wake. Divai ilipokwisha, mama yake akamwambia, "Hawana divai!" Yesu akamjibu, "Mama, usiniambie la kufanya. Saa yangu bado." Hapo mama yake akawaambia watumishi, "Lolote atakalowaambieni, fanyeni." Hapo palikuwa na mitungi sita ya mawe, ambayo kila mmoja uliweza kuchukua kiasi cha madebe mawili au matatu. Ilikuwa imewekwa hapo kufuatana na desturi ya Kiyahudi ya kutawadha. Yesu akawaambia, "Ijazeni mitungi hiyo maji." Nao wakaijaza mpaka juu. Kisha akawaambia, "Sasa choteni mkampelekee mkuu wa karamu." Mkuu wa karamu alipoonja hayo maji, kumbe yalikuwa yamegeuka kuwa divai. Yeye hakujua ilikotoka, (lakini wale watumishi waliochota maji walijua). Mkuu wa karamu akamwita bwana arusi, akamwambia, "Kila mtu huandaa divai nzuri kwanza hata wakisha tosheka huandaa ile hafifu. Lakini wewe umeiweka divai nzuri mpaka sasa!" Yesu alifanya ishara hill ya kwanza huko Kana, Galilaya, akaonesha utukufu wake; nao wanafunzi wake wakamwamini.

( Utukufu kwako, Ee Bwana, utukufu kwako. )

SHEMASI

Utuhurumie, Ee Mungu kadiri ya huruma yako kubwa, tunakuomba utusikilize na kutuhurumia.

( Bwana hurumia, Bwana hurumia, Bwana hurumia. )

( Bwana hurumia, Bwana hurumia, Bwana hurumia. )

KASISI

Kwa kuwa U Mungu mrahimu na mpenda wanadamu, na kwako tunatoa utukufu, kwa Baba na Mwana na Roho Mtakatifu, sasa na siku zote hata milele na milele.

( Amina. )

SHEMASI

Tumwombe Bwana.

( Bwana, hurumia. )

KASISI

Ee Bwana Mungu wetu ulitoa wokovu na kuamuru ndoa ya heshima kwa kushiriki kwako Kana ya Galilaya; Waweke kwenye amani na mapatano hawa watumishi wako (Majina) ambao wamefurahia kuunganishwa kwa kwao pamoja. Ifanye ndoa yao kuwa yenye heshima, na uhifadhi, ili waweze kuishi pamoja bila hatia. Wape maisha marefu kwa kutimiza amri na moya mwema.

( Amina. )

SHEMASI

Utusaidie, utuokoe, utuhurumie, utuhifadhi, Ee Mungu, kwa neema yako.

( Bwana, hurumia. )

Siku hii yote iwe kamili, takatifu, tulivu na bila dhambi, tuombe kwa Bwana.

( Kidhi, Ee Bwana. )

Kwa ajili ya kuwa na Malaika wa amani, mwongozi mwaminifu, mlinzi wa roho zetu na miili yetu, tuombe kwa Bwana.

( Kidhi, Ee Bwana. )

Kwa ajili ya msamaha na maondoleo ya dhambi zetu na makosa yetu, tuombe kwa Bwana.

( Kidhi, Ee Bwana. )

Kwa ajili ya vitu vyema vifaavyo kwa roho zetu na amani ya dunia yote, tuombe kwa Bwana.

( Kidhi, Ee Bwana. )

Kwa ajili ya kumaliza maisha yetu yanayobaki kwa amani na toba, tuombe kwa Bwana.

( Kidhi, Ee Bwana. )

Tuombe ili mwisho wa maisha yetu uwe wa kikristo kwa amani, bila maumivu, aibu, tena tuone teto njema mbele ya kiti cha hukumu cha Kristo.

( Kidhi, Ee Bwana. )

Tukiomba umoja wa imani na ushirika wa Roho Mtakatifu, sisi na kila mmoja wetu, na wenzetu wote hata maisha yetu, kujiweka mikononi mwa Kristo Mungu.

( Kwako, Ee Bwana. )

KASISI

Na utustahilishe, Ee Bwana wa Mabwana, tukiwa na uthabiti, bila hukumu, tuwe na ujasiri kukuita Baba, wewe Mungu uliye mbinguni, na kusema:

WATU

Baba yetu uliye Mbinguni; Jina lako litukuzwe; Ufalme wako uje; mapenzi yako yatimizwe, hapa Duniani kama huko Mbinguni. Utupe leo mkate wetu wa kila siku; na utusamehe deni zetu; kama sisi tuwasamehevyo wadeni wetu; tena usitutie majaribuni, lakini tuokoe na yule mwovu.

KASISI

Kwa kuwa ufalme ni wako, na nguvu, na utukufu, wa Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu, sasa na siku zote hata milele na milele.

( Amina. )

Amani kwa wote.

( Na iwe kwa roho yako. )

Tuinamishe vichwa vyetu kwa Bwana.

SHEMASI

( Kwako, Ee Bwana. )

SHEMASI

Tumwombe Bwana.

( Bwana, hurumia. )

KASISI

Ee Mungu uliye umba vitu vyote kwa uwezo wako, ulimwengu tena ukarembesha vyote ulivyoumba. Bariki kikombe hiki cha ushirika kwa baraka zako takaktifu na kuwapatia wanaoungana katika ndoa.

Kwa kuwa Jina Lako limebarikiwa, na Ufalme Wako umetukuzwa, wa Baba na Mwana na Roho Mtakatifu, sasa na siku zote, hata milele na milele.

( Amina. )

WATU

Alleluia.

Enyi mashahidi watakatifu wapiganaji wema ambao wamevikwa taji, mtuombee ili azihurumie roho zetu [[SWA]]

Utukufu Kwako Ee Kristo Mungu wetu, Mitume Kristo wetu, mitume wasifiwa na wenye fahari na mashahidi wapendwa walio na ujumbe wa utatu mtakatifu. [[SWA]]

KASISI

Ewe Bwana harusi utukuzwe kama Ibrahimu na ubarikiwe kama Isaka na uwe na uzao kama vile Yakobo: utembee kwa haki na utimize amri zake Mungu.

KASISI

Nawa Bibi harusi , utukuzwe kama vile Sara na uwe na furaha kama Rebeka, uwe na uzao kama Recho ukishangilia katika Bwana wako, na kuzingatia wajibu wa sheria kwa kuwa Mungu amefurahia.

SHEMASI

Tumwombe Bwana.

( Bwana, hurumia. )

KASISI

Ee Mungu, Mungu wetu aliye kwenda mjini Kana ya Galilaya na ukambariki ndoa huko, ubariki hawa watumishi wako, ambao kwa uwezo wako wameungana pamoja na jamii kwa ndoa, Bariki kwenda na kurejea kwao. Wafariji na maisha ya ut, vitu vyema chukua taji zao (* Anatoa taji vichwani mwao). Katika ufalme wako zikihifadhiwa bila kuharibika, kulaumiwa na kuambika hadi milele na milele.

( Amina. )

KASISI

Amani kwa wote.

( Na iwe kwa roho yako. )

SHEMASI

Tuinamishe vichwa vyetu kwa Bwana.

( Kwako, Ee Bwana. )

KASISI

Kwa uweza wa Mungu Baba, Mungu Mwana Roho Matakatifu, utatu mtakatifu usiotengana na ufalme wako, uwape watoto wazuri, maisha ya ufanisi, kukua katika imani na uwajaze na vitu vyote vyema vya ulimwenguni; Wafurhishe na wema wa baraka zilizoahidiwa kwetu. Kwa maombezi ya Maria Mtakatifu na watakatifu wote.

( Amina. )

KASISI

Utukufu kwako, Ee Kristo Mungu wetu na matumaini yetu, utukufu kwako.

MSOMAJI

Utukufu. Sasa.

Bwana, hurumia. Bwana, hurumia. Bwana, hurumia. Ee padri mtakatifu, bariki.

Kristo Mungu wa ukweli ambaye kuja kwake Kana ya Gallaya na kufanya ndoa kuwa yenye heshima. Kwa maombi ya Maria Mzazi Mungu asiye na ndoa lo lote, mitume watukufu na wasifiwa na kwa wafalme watukufu na wasifiwa na Mungu sawa na mitume. Constantino na Hellen shahidi mtakatifu Prokopius na watakatifu wote utuhurumie na kutuokoa kwa kuwa yu Mungu mwema na mpenda wanadamu.

Kwa maombi ya mababa wetu watakatifu, Ee Bwana Yesu Kristo Mungu wetu, utuhurumie na utuokoe.

( Amina. )


MSOMAJI

Amina.

KASISI

Amani kwa wote.

MSOMAJI

Na iwe kwa roho yako.

SHEMASI

MSOMAJI

Kwako, Ee Bwana.

KASISI

MSOMAJI

Amina.