Ibada ya Makumbusho
KASISI
Ahimidiwe Mungu wetu, daima, sasa na siku zote, hata milele na milele.
( Amina. )
MSOMAJI
Utukufu kwako, Ee Mungu wetu, utukufu
Maombi ya Trisaghio.
Mungu Mtakatifu, Mweza Mtakatifu, Usiyekufa Mtakatifu, utuhurumie. (3)
Utukufu kwa Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu. Sasa na siku zote hata milele na milele. Amina.
Ee Utatu mtakatifu kamili, utuhurumie. Bwana, utusamehe dhambi zetu. Rabi, utuondolee makosa yetu. Mtakatifu, utukaribie na kutuponya magonjwa yetu, kwa ajili ya jina lako.
Bwana hurumia, Bwana hurumia, Bwana hurumia.
Utukufu kwa Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu. Sasa na siku zote hata milele na milele. Amina.
Baba yetu uliye Mbinguni; Jina lako litukuzwe; Ufalme wako uje; mapenzi yako yatimizwe, hapa Duniani kama huko Mbinguni. Utupe leo mkate wetu wa kila siku; na utusamehe deni zetu; kama sisi tuwasamehevyo wadeni wetu; tena usitutie majaribuni, lakini tuokoe na yule mwovu. [[SWA]]
KASISI
Kwa kuwa ufalme ni wako, na nguvu, na utukufu, wa Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu, sasa na siku zote hata milele na milele.
WATU
Evlogitaria ya Wafu
Sauti ya 5
Ee Bwana wahimidiwa, unifundishe zilizo haki zako.
Jamii ya watakatifu imeona chechemi ya uzima na lango la kuingia Paradiso, niweze nami kuiona njia hiyo kwa kutubu, maana mimi ndimi kondoo aliyepotea, Ee mwokozi unirejeshe na kuniokoa. [[SWA]]
Ee Bwana wahimidiwa, unifundishe zilizo haki zako.
Ewe uliye niumba kutoka bure na ukanipa heshima kwa mfano wako; lakini kwa kuasi amri zako ulinirudisha udongoni mahali nilipotoka, uniongoze na unirudishe katika tabia ya kale, nipate tena uzuri ule wa kwanza (Paradiso). [[SWA]]
Ee Bwana wahimidiwa, unifundishe zilizo haki zako.
Mimi ndimi mfano wa ufufuko wako usionenwa ingawa nina madoa ya dhambi. Ee Rabii, unirehemu mimi kiumbe chako na unisafishe kwa fadhili zako na unifanye tena mwana wa Paradiso. [[SWA]]
Ee Bwana wahimidiwa, unifundishe zilizo haki zako.
Ee Bwana Mungu umpumzishe mtumishi wako, na umweke katika paradiso, mahali pa jamii ya watakatifu, na wenye haki wanapong’ara kama jua, mrehemishe mtumishi wako huyu aliyelala na kuaga dunia, umsamehe hatia zake zote. [[SWA]]
Utukufu kwa Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu.
Kwa Utatu Mtakatifu wa Mungu, kwa utiifu wacha tuimbe tupaze sauti tukilia; ni wewe Mtakatifu Baba wa milele, na Mwana wako pamoja na Roho Mtakatifu, utuangazie mwanga wako sisi tulio na imani tukikuabudu wewe, utuokoe kutoka kwa moto wa milele. [[SWA]]
Sasa na siku zote hata milele na milele. Amina.
Salaamu, Mtakatifu wa utukufu, uliye mzaa Mungu kwa ajili ya wokovu wa wote, kupitia kwako jamii ya watu ilipata wokovu: Kupitia kwako tuipate paradiso, wewe mbarikiwa na mzazi Mungu. [[SWA]]
Alleluia, Alleluia, Alleluia, utukufu kwako ee Mungu. [[SWA]]
Kontakio. Sauti ya 8.
Pamoja na watakatifu, pumzisha, O Kristo, roho ya mtumishi wako mahali pasipo na uchungu, sikitiko au kuomboleza lakini uzima wa milele. [[SWA]]
Ee Mwokozi pumzisha roho ya mtumishi wako mahali pakupumzikia roho za Watakatifu wako na uiweke vema kwa kuishi pamoja na wewe mpenda wanadamu. [[SWA]]
Katika mapumziko yako Ee Bwana pumzisha roho ya mtumishi wako huyu kwa kuwa wewe ndiwe pekee usiyekufa. [[SWA]]
Utukufu kwa Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu.
Ni wewe Mungu wetu uliyeshuka kuzimuni kwa kufungua wale ambao waliokuwa wakiteseka kwa kifo; pumzisha roho ya mtumishi wako huyu, Ee Mwokozi. [[SWA]]
Sasa na siku zote hata milele na milele. Amina.
Ee Bikira, Mtakatifu peke yako ni wewe uliye mzaa Mungu, ombea roho ya mtumishi wako iokolewe. [[SWA]]
SHEMASI
Utuhurumie, Ee Mungu kadiri ya huruma yako kubwa, tunakuomba utusikilize na kutuhurumia.
( Bwana hurumia, Bwana hurumia, Bwana hurumia. )
Tena tunakuomba kwa ajili ya mapumziko ya roho ya mtumishi wa Mungu (jina) ambaye amelala, na kwa kusamehewa dhambi zake zote zile alitenda kwa kujua au pasipo kujua.
( Bwana hurumia, Bwana hurumia, Bwana hurumia. )
Ili Bwana Mungu, aiweke roho yake mahali ambapo watakatifu wanapumzika, na atampa rehema zake Mungu, ufalme wa mbinguni na maondoleo ya dhambi zake, Tumuombe Kristo mfalme asiyekufa tena Mungu wetu.
( Kidhi, Ee Bwana. )
SHEMASI
Tumwombe Bwana.
( Bwana, hurumia. )
KASISI
Ee Mungu wa mioyo yote na kila Mwili, uliye kanyanga kifo na kushinda shetani, nakuipa dunia yako uhai, kwa roho ya mtumishi wako (jina) aliyelala, pumzisha roho yake na uiweke mahali pa mwanga, utulivu na upole, pasipo na uchungu, masikitiko na kilio. Kila ubaya aliofanya kwa fikira, kwa maneno au kwa matendo, nakuomba kama Mungu wetu, mpenda wanadamu, tena mwenye huruma, umsamehe, ukijua hakuna mtu aliye hai asiyetenda dhambi isipokuwa wewe peke yako. Ukweli wako ni wa milele, tena amri yako ni ya ukweli.
SHEMASI
Tumwombe Bwana.
( Bwana, hurumia. )
KASISI
Kwa kuwa wewe ndiwe ufufuko, uhai tena mapumziko ya mtumishi wako (jina) aliyelala, Ee Kristo Mungu wetu; na kwako tunatoa utukufu kwa Baba yetu asiye na mwanzo na Roho Mtakatifu kamili, mwema na mpaji wa uhai, sasa na siku zote hata milele na milele.
( Amina. )
KASISI
Utukufu kwako, Ee Kristo Mungu wetu na matumaini yetu, utukufu kwako.
MSOMAJI
Utukufu kwa Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu. Sasa na siku zote hata milele na milele. Amina. Bwana, hurumia. (3) Ee padri mtakatifu, bariki.
KASISI
Yeye Kristo Mungu wetu wa kweli, ya mababu watakatifu wetu Ibrahimu, Isaka Na Yakobo; ya mtakatifu tena rafiki yako Lazaro; aliyemaliza siku nne kaburini; Uiweke roho ya mtumishi wako (jina), aliyeaga katika mahali pa watakatifu; mpumzishe katika kifua cha Ibrahimu, tena umhesabu kuwa mojawapo ya watakatifu, na utuhurumie na utuokoe kwa kuwa wewe u Mungu mwema na mpenda wanadamu. atuhurumie na atuokoe, yu Mungu mwema, mrahimu na mpenda wanadamu.
Makumbusho yako yawe ya milele ndugu (dada) wetu mbarikiwa na unayestahili kumbukwa. (3)
WATU
Sauti ya 3.
Makumbusho ya milele na milele. Makumbusho ya milele na milele. Makumbusho ya milele na milele. (3)
KASISI
Kwa maombi ya mababa wetu watakatifu, Ee Bwana Yesu Kristo Mungu wetu, utuhurumie na utuokoe.
( Amina. )