×




Ee padri, himidi.

Mhimidiwa ni Ufalme wa Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu, sasa na siku zote hata milele na milele.

( Amina. )

Ee padri, himidi.

Mhimidiwa ni Ufalme wa Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu, sasa na siku zote hata milele na milele.

( Amina. )

SHEMASI

Kwa amani, tumwombe Bwana.

WATU

Bwana, hurumia.

SHEMASI

Kwa ajili ya amani kutoka juu na ya wokovu wa roho zetu, tumwombe Bwana.

Kwa ajili ya amani ya dunia yote, na kusimama imara kwa Ekklesia Takatifu ya Mungu, na ya umoja wa wote, tumwombe Bwana.

Kwa ajili ya nyumba hii takatifu na waingiamo kwa imani, heshima na kumcha Mungu, tumwombe Bwana.

Kwa ajili ya wakristo wateule na waorthodoksi wote, tumwombe Bwana.

Kwa ajili ya Askofu wetu mkuu Askofu wetu mkuu (jina) Makasisi, Mashemasi wateule na watu wote tumwombe Bwana.

Kwa ajili ya taifa letu (jina) na raisi wetu (jina), na viongozi wetu, na wa majeshi wapendao dini, tumwombe Bwana.

Kwa ajili ya mji huu na miji yote na nchi zote na waishimo kwa imani, tumwombe Bwana.

Kwa ajili ya majira mema ya mwaka kupata mvua ya kutosha na hewa safi na rotuba ya kutosha kwa ardhi, tumwombe Bwana.

Kwa ajili ya wasafiri hewani juu, baharini majini, na nchini kavu, wachoshwa na mateka kupata uhuru, na kwa ajili ya wokovu wao, tumwombe Bwana.

Kwa ajili ya kuokolewa kwa kila sitikiko, ghadhabu, hatari na uhitaji, tumwombe Bwana.

Utusaidie, utuokoe, utuhurumie, utuhifadhi, Ee Mungu, kwa neema yako.

Tumkumbuke Maria Mtakatifu kamili, asiye na doa, Mbarikiwa zaidi kushinda wote, Bibi wetu mtukufu mzazi Mungu na bikira daima pamoja na watakatifu wote hata sisi pia wenyewe na kila mmoja wetu na wenzetu wote, hata maisha yetu, kujiweka mikononi mwa Kristo Mungu.

Kwako, Ee Bwana.

KASISI (kwa mnong''ono)

OMBI LA ANTIFONO YA KWANZA

Ee Bwana, Mungu wetu mwenye enzi yote na utukufu kupita kila ufahamu, uliye na huruma sana, tena mpenda wanadamu usiye elezeka; wewe ndiwe Bwana wa Mabwana, kulingana na huruma yote utazame sisi na hekalu hii takatifu na utupatie sisi pamoja nao tunaokuomba huruma, utajiri na rehema.

KASISI

Kwa kuwa utukufu wote na heshima na usujudu ni haki yako, ya Baba na Mwana na Roho Mtakatifu, sasa na siku zote, hata milele na milele.

WATU

Amina.

WATU

Antifono ya 1

(Mistari ya zaburi inaandamana na wimbo:)

Kwa maombi ya Mzazi- Mungu, Ee mwokozi, utuokoe.

LITANIA FUPI

SHEMASI

LITANIA FUPI

SHEMASI

Tena na tena kwa amani, tumwombe Bwana.

Bwana, hurumia.

SHEMASI

Utusaidie, utuokoe, utuhurumie, utuhifadhi, Ee Mungu, kwa neema yako.

Bwana, hurumia.

SHEMASI

Tumkumbuke Maria Mtakatifu kamili, asiye na doa, Mbarikiwa zaidi kushinda wote, Bibi wetu mtukufu mzazi Mungu na bikira daima pamoja na watakatifu wote hata sisi pia wenyewe na kila mmoja wetu na wenzetu wote, hata maisha yetu, kujiweka mikononi mwa Kristo Mungu.

Kwako, Ee Bwana.

KASISI (kwa mnong''ono)

Sala ya Itikio (antifono) ya 2

Ee Bwana, Mungu wetu, uwaokoe watu na ubariki uriithi wako; ilinde jamii ya Ekklisia lako; tena utakase hao wanopenda uzuri wa nyumba yako; wewe uwape utukufu kwa uweza wako wa Umungu, na usijitenge nasi tunaokutumaini wewe.

KASISI

Kwa kuwa, utawala ni kwako na ufalme na uweza, na utukufu ni vyako, Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu, sasa na siku zote, hata milele na milele.

WATU

Amina.

WATU

Antifon ya 2

(Mistari ya Zaburi inaandamana na wimbo:)

Ee Mwana wa Mungu, uliye fufuka toka wafu, utokoe sisi twakuimbia . Alleluia.

Utukufu kwa Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu.

Sasa na siku zote hata milele na milele. Amina.

Uliye Mwana tena Neno la Mungu, ukiwa usiyekufa, ukakubali kwa ajili ya wokovu wetu, kupata mwili, kwa Maria Mzazi Mungu, tena Bikira daima, ukawa mtu, bila kujigeuza; na ukasulubiwa, Ee Kristo Mungu, ukakanyaga kifo kwa kifo; ukiwa mmoja wa utatu Mtakatifu, na unatukuzwa pamoja na Baba na Roho Mtakatifu, utuokoe.

LITANIA FUPI

SHEMASI

Tena na tena kwa amani, tumwombe Bwana.

Bwana, hurumia.

SHEMASI

Utusaidie, utuokoe, utuhurumie, utuhifadhi, Ee Mungu, kwa neema yako.

Bwana, hurumia.

SHEMASI

Tumkumbuke Maria Mtakatifu kamili, asiye na doa, Mbarikiwa zaidi kushinda wote, Bibi wetu mtukufu mzazi Mungu na bikira daima pamoja na watakatifu wote hata sisi pia wenyewe na kila mmoja wetu na wenzetu wote, hata maisha yetu, kujiweka mikononi mwa Kristo Mungu.

Kwako, Ee Bwana.

KASISI (kwa mnong''ono)

Sala ya Itikio (antifono) ya 3

Ee Bwana uliyetupatia sala hizi za pamoja; uliyeahidi kwa watu wawili hata kwa hao watakao patana kwa jina lako. Kuwasikiliza na kutimiza dua zao; wewe ndiwe utimizaye dua za watumwa wako kwa faida yetu, ukitupatia ujuzi wa kujua kamili ukweli wako katika dunia hii, tena uzima wa milele katika ulimwengu utakaokuja.

KASISI

Kwa kuwa U Mungu Mwema na mpenda wanadamu, na kwako tunatoa Utukufu, kwa Baba na Mwana na Roho Mtakatifu, sasa na siku zote, hata milele na milele.

WATU

Amina.

WATU

Antifon ya 3

(Mistari ifaayo ya zaburi inaandamana na Apolitikio)


(Apolitikio inapoimbwa, kasisi akibeba Kitabu cha Injili anakuja kwenye Mlango Bora huku akitanguliwa na vijana waliobeba mishumaa, na kusema ombi hili kwa mnong''ono)

Tumwombe Bwana.

OMBI LA INGILIO

KASISI (kwa mnong''ono)

Ee Bwana wa mabwana, Mungu wetu, uliyeweka mbunguni makundi ya majeshi ya Malaika, na Malaika majemadari kuadhimisha utukufu wako, ufanye kuingia kwetu kuwe pamoja na Malaika watakatifu, wanao adhimisha pamoja nasi kutoa utukufu kwa wema wako. Kwa kuwa kila utukufu, na heshima, na usujudu ni haki yako ya Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu, sasa na siku zote hata milele na milele. Kwa kuwa utukufu wote na heshima na usujudu ni haki yako, ya Baba na Mwana na Roho Mtakatifu, sasa na siku zote, hata milele na milele.

SHEMASI (kwa mnong''ono)

Ee padri, bariki kuingia kutakatifu.

Kubarikiwa kuwe kuingia kwa patakatifu pako, daima sasa na siku zote, hata milele na milele. Amina.

SHEMASI

Hekima. Simameni wima.

WATU

Wimbo wa kuingia Sauti 2.

Njooni tumsujudie, na kumwangukia, Kristo, Ee Mwana wa Mungu, uliye fufuka toka wafu, utokoe sisi twakuimbia . Alleluia.

(Siku za juma tunaimba: ("uliye wa ajabu kati ya watakatifu"), nazo Sikukuu za Bwana zina Nyimbo zake za kuingia za kipekee.)

(Kasisi anaingia kwenye madhabahu. Apolitikio inarudiwa kuimbwa na Tropario ya Kanisa pamoja na Kontakio ya siku zinaimbwa.)


Uliye ulinzi wa Wakristo, usiyeaibika, mneneaji kwa Mwumba usiyeaibika: usidharau sauti za maombi ya wenye dhambi, lakini tangulia kama mwema we kutusaidia sisi wenye kupaza sauti kwako. Harakisha kututetea, na ufanye hima kutuombea, uliyetunza daima waliokuheshimu, Ee Mzazi-Mungu. [[SWA]]

SHEMASI

Tumwombe Bwana.

WATU

Bwana, hurumia.

KASISI (kwa mnong''ono)

WIMBO TAKATIFU TATU (TRISAGHIO)

Ee Mungu, uliye Mtakatifu, na kukaa ndani ya watakatifu; unayesifiwa na waserafi kwa sauti takatifu ya Utatu, tena waadhimishwa na waheruvi, na kusujudiwa na nguvu zote za mbinguni juu; uliyefanya vitu vyote toka bure, na vikawa. Uliye mwumba binadamu kwa sura na mfano wako, tena kumpamba kwa vipaji vyotevya neema yako. Unayempa yeyote anaye kuuliza hekima na busara, usiye mdharau mwenye dhambi, bali ulimwekea kutubu, kama njia ya wokovu; Uliye tustahilisha hata sisi watumwa wako, wanyenyekevu na wasiostahili, hata wakati huu kusimama mbele ya utukufu wa madhabahu yako matakatifu, na kukuletea kusujudu na sifa iliyo haki zako. Bwana, upokee wimbo huu wa Utatu Mtakatifu tunao utoa midomoni mwetu, sisi wanadamu wenye dhambi, na ututembelee kwa wema wako. Utusamehe kila dhambi ambayo tumeifanya kwa hiari ama kwa kutotaka, Utakase roho na miili yetu, na utustahilishe kukuabudu kwa utakatifu siku zote za maisha yetu, kwa maombi ya Mzazi-Mungu wetu mtakatifu, na ya Watakatifu wote waliokupendeza tangu milele.

KASISI

Kwa kuwa Wewe, Mungu wetu ni Mtakatifu, na Kwako tunatoa utukufu kwa Baba; na Mwana na Roho Mtakatifu, sasa na sikuzote,

SHEMASI

hata milele na milele.

WATU

Amina.

Wimbo wa Utatu Mtakatifu (Wimbo wa Trisagio)

Mungu Mtakatifu, Mweza Mtakatifu, Usiyekufa Mtakatifu. Utuhurumie. (3)

Utukufu kwa Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu. Sasa na siku zote hata milele na milele. Amina.

Usiyekufa Mtakatifu. Utuhurumie.

SHEMASI

Kwa nguvu.

SHEMASI (kwa mnong''ono)

Padri, Amuru.

KASISI (kwa mnong''ono)

Abarikiwe yeye ajaye kwa jina la Bwana.

SHEMASI (kwa mnong''ono)

Ee Padri himidi kiti cha Enzi kilicho juu.

KASISI (kwa mnong''ono)

Mhimidiwa ni wewe uliye katika kiti cha Enzi cha ufalme wako, uketiye begani pa Wakheruvi, daima, sasa na siku zote, hata milele na milele. Amina

WATU

Kwa nguvu.

Mungu Mtakatifu, Mweza Mtakatifu,Usiyekufa Mtakatifu, utuhurumie.

MASOMO

WARAKA

SHEMASI

Tusikilize.

KASISI

Amani kwa wote.

WATU

Na iwe kwa roho yako.

SHEMASI

Hekima.

MSOMAJI

…

SHEMASI

Tusikilize.

(Msomaji anasoma mistari ya Zaburi.)

SHEMASI

Hekima.

SHEMASI

Tusikilize.

MSOMAJI

(Msomaji anasoma Barua ya siku.)

KASISI

Amani kwako Ee Msomaji.

WATU

Alleluia, Alleluia, a|leluia.

KASISI (kwa mnong''ono)

Ee Bwana wa Mabwana, mpenda wanadamu, angaza mioyo yetu na nuru yako takatifu ya ujuzi wa kujua Mungu; tena ufungue macho ya fikiria zetu, ili tufahamu mahubiri ya Evangelio yako. Uweke ndani yetu uchaji wa amri zako, kusudi tupate kuzikanyanga tamaa mbaya zote za kimwili, na kufuata njia ya kuishi kiroho, hata kifikiri na kutenda vitu vyote vinavyo kupendeza. Kwa kuwa wewe ndiwe mwanga wa roho na miili yetu, Ee Kristo Mungu, na kwako tunatoa utukufu, pamoja na Baba yako asiye na mwanzo, na Roho wako Mtakatifu kamili, mwema na mpaji wa uhai, sasa na siku zote hata milele na milele. Amina.

INJILI

(jina)

KASISI

(jina)

Amina.

SHEMASI

Hekima. Simameni wima. tusikilize Evanjelio Takatifu.

KASISI

Amani kwa wote.

WATU

Na iwe kwa roho yako.

SHEMASI

Somo katika Evanjelio Takatifu kama ilivyoandikwa na Mtakatifu (Jina).

KASISI

Tusikilize.

WATU

Utukufu kwako, Ee Bwana, utukufu kwako.

SHEMASI

(Dikoni anasoma fungu la Injili Takatifu.)

KASISI

Amani iwe kwako.

WATU

Utukufu kwako, Ee Bwana, utukufu kwako.


MAHUBIRI

LITANIA NDEFU (EKTENI)

SHEMASI

Tuseme sisi sote kwa roho yetu na kwa mawazo yetu yote tuseme hivi.

( Bwana, hurumia. )


Ee Bwana Mwenyezi Mungu wa mababu wetu tunakuomba utusikilize na kutuhurumia.

( Bwana, hurumia. )


Utuhurumie, Ee Mungu kadiri ya huruma yako kubwa, tunakuomba utusikilize na kutuhurumia.

( Bwana, hurumia. (3) )


Tena tunaomba kwa ajili ya Askofu wetu mkuu (jina)

Tena tunakuomba kwa ajili ya huruma, uzima, amani, afya, wokovu, ulinzi, msamaha na maondoleo ya dhambi kwa watumishi wa Mungu, walinzi wasimamizi na washiriki wa Kanisa hili takatifu.

Tena tunakuomba kwa ajili ya warehemiwa wajengaji wa kanisa hili takatifu, ambao ni kwa makumbusho ya daima ya baba na ndugu zetu wote wa Orthodoksi warehemiwa, ambao wamelala hapa na mahali popote.

Tena tunakuomba kwa ajili yao wanaotenda matendo mema katika nyumba hii takatifu na heshimiwa, kwa ajili yao wenye juhudi, wanaoimba, hata ya watu wote wanaosimama hapa, wakingoja huruma yako kubwa na utajiri.

SALA YA LITANIA NDEFU (EKTENIA)

KASISI (kwa mnong''ono)

Ee Bwana Mungu wetu, pokea maombi haya yenye moyo wa bidii ya watumwa wako, na utuhurumie kadiri ya wingi wa huruma zako; utupatie sisi Baraka zako na kwa watu wako wote wanaongoja huruma yako kubwa nay a utajiri.

KASISI

Kwa kuwa U Mungu mrahimu na mpenda wanadamu, na kwako tunatoa utukufu, kwa Baba na Mwana na Roho Mtakatifu, sasa na siku zote hata milele na milele.

( Amina. )

SHEMASI

Enyi Wakatekumeno ombeni kwa Bwana.

( Bwana, hurumia. )

Sisi tulioamini tuwaombee wakatekumeno.

( Bwana, hurumia. )

Ili kwamba, Bwana awahurumie.

( Bwana, hurumia. )

Ili kwamba Bwana awafundishe neno lake la kweli.

( Bwana, hurumia. )

Ili kwamba awafunulie Injili yake ya haki.

( Bwana, hurumia. )

Ili kwamba awaunganishe na Kanisa Lake Takatifu, Katoliki na la Mitume.

( Bwana, hurumia. )

Uwaokoe, uwahurumie, uwasaidie na uwalinde Ee, Bwana kwa neema yako.

( Bwana, hurumia. )

Enyi wakatekumeno inamishemi vichwa vyenu kwa Bwana.

( Kwako, Ee Bwana. )

MAOMBI YA WAKATEKUMENO

KASISI (kwa mnong''ono)

Ee Bwana, Mungu wetu, unayekaa juu, na kulinda walio wanyenyekevu, Ulimtuma Mwana wako wa Pekee na Mungu, Bwana wetu Yesu Kristo, kwa ajili ya wokovu wa wanadamu, watazame watumwa wako, wakatekumeno, walio inamisha shingo zao mbele yako; na uwakidhie wakati ufaao wa kuzaliwa upya kupitia ubatizo, msamaha wa dhambi, vazi lisilo haribika. Uwaunganishe na Kanisa lako Takatifu, Katoliki na la Mitume, na uwahesabu kati ya zizi lako teule.

KASISI

Ili hata hawa pamoja nasi walitukuze jina lako adhimu na linalo heshimiwa, la Baba na la Mwana, na Roho Mtakatifu, sasa na siku zote hata milele na milele.

( Amina. )

SHEMASI

Wote walio wakitumeno tokeni nje. Wakitumeno tokeni nje. Wote walio wakatikumeno tokeni. Wakatikumeno wasibaki.

LITURGHIA YA WAUMINI

Tena na tena, sisi tulio amini, kwa amani tumwombe Bwana.

( Bwana, hurumia. )

Utusaidie, utuokoe, utuhurumie, utuhifadhi, Ee Mungu, kwa neema yako.

( Bwana, hurumia. )

Hekima.

OMBI LA KWANZA KWA WALIO AMINI

KASISI (kwa mnong''ono)

Tunakushukuru, Ee Bwana Mungu wa Majeshi, Ambaye umetustahirisha ata sasa kusimama mbele ya Madhabahu yako atakatifu na kuanguka mbele Zako tukiomba rehema Zako kwa ajili ya dhambi zetu na zile watu wako walizotenda bila kujua. Kubali, Ee Bwana maombi yetu. Tustahilishe kukuletea maombi, teto na hata dhabihu isiyo ya damu kwa ajili ya watu wako. Na utustahilishe kwa uwexa wa Roho Wako Mtakatifu, kwamba sisi uliotawaza kwa huduma hii Yako, tuwe bila lawama au kifungo, na kwamba tukishuhudiwa na fikra isiyo na lawama, tuweze kukuita wakati wowote na mahali popote, na ili kwamba, ukitusikia, uweze kutuhurumia kupitia kwa wema wako mkuu.

KASISI

Kwa kuwa utukufu wote na heshima na usujudu ni haki yako, ya Baba na Mwana na Roho Mtakatifu, sasa na siku zote, hata milele na milele.

( Amina. )

SHEMASI

Tena na tena kwa amani, tumwombe Bwana.

( Bwana, hurumia. )

Utusaidie, utuokoe, utuhurumie, utuhifadhi, Ee Mungu, kwa neema yako.

( Bwana, hurumia. )

Hekima.

OMBI LA PILI LA WALIO AMINI

KASISI (kwa mnong''ono)

Tena na mara nyingi sisi huanguka mbele zako ana kukusihi, Ee Mwema na mpenda wanadamu: Kwamba Wewe, ukishakadiria ombi letu, utatakasa roho ma miili yetu kutokana na unajisi wa roho na mwili, na utukidhie kusimama mbele ya Altari yako ya dhabihu, bila lawama au hukumu. Wakidhie pia, Ee Bwana, wale waombao pamoja nasi, maendeleo katika maisha, imani na ujuzi wa kiroho. Wakidhie kwamba wakuabudu milele kwa heshima na upendo, washiriki fumbo Lako bila lawama au hukumu, na wastahilishwe kuingia katika Ufalme wako wa Mbinguni.

KASISI

Ili sisi tukilindwa daima kwa kutawala kwako, tutoe utukufu, kwa Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu, sasa na sikuzote hata milele na milele.

( Amina. )

KUINGIA KUKUU / INGILIO KUBWA

WATU

Kama Waheruvi, kwa siri tunaofanana na tunaoimbia Utatu mpaji wa uhai wimbo Mtakatifu wa Utatu, (wimbo wa Trisaghio) tuweke mbali kila tafakari ya maisha. kwa kuwa mfalme wa wote tutamkaribisha.

SALA YA WIMBO WA WAHERUVI

KASISI (kwa mnong''ono)

Mtu wa tamaa na anasa za mwili hastahili kukujia au kukukaribia na kukuabudu, Ee mfalme wa utukufu; kwa kuwa kukutumikia ni kwa hofu sana, hata kwa Majeshi wa mbinguni: Lakini kwa kuwa unapenda binadamu kwa hali ya ajabu, umejifanya Kuhani Mkubwa wetu bila kujigeuza au kubadilika; na wewe ndiwe umetupatia kuadhimisha dhabihu hii isiyo na damu, wewe uliye Bwana wa Mabwana wa vitu vyote. Kwa kuwa ndiwe, Bwana Mungu wetu wa pekee watawala vilivyo mbinguni na duniani, unayeketi katika kiti cha enzi begani mwa Wakheruvi, uliye Bwana wa Waserafi tena mfalme wa Israeli. Ndiwe Mtakatifu wa pekee uliyepumzika kati ya watakatifu, basi nakusihi wewe uliye mwema pekee na kusikia rahisi; uniangazie mimi mtumwa wako mwenye dhambi na asiyefaa; utakase roho na moyo wangu na kila dhamira mbaya; tena unijalie kwa nguvu ya roho Mtakatifu ili, nikivaa neema ya ukasisi, nisimame mbele ya Meza yako hii Takatifu; na kuadhimisha Mwili wako Mtakatifu na wa usafi na Damu yako ya thamani. Kwa kuwa nakujia wewe, nikiinamisha shingo yangu, nakusihi ; usinifiche uso wako; mbali mimi mtumwa wako mwenye dhambi nisiyestahili, unistahilishe kukuletea vipaji hivi. Kwa kuwa wewe ndiwe uliyetoa na uliyetolewa, uliyepokea tena uliyegawanya, Ee Kristo Mungu wetu, na kwako tunatoa utukufu, pamoja na Baba yako asiye, na mwanzo na kwa Roho wako Mtakatifu kamili, mwema na mpaji wa uhai, sasa na siku zote, hata milele na milele. Amina.

KASISI

Kama Waheruvi, kwa siri tunaofanana na tunaoimbia Utatu mpaji wa uhai wimbo Mtakatifu wa Utatu, (wimbo wa Trisaghio) tuweke mbali kila tafakari ya maisha.

SHEMASI

kwa kuwa mfalme wa wote tutamkaribisha. Akifuatwa na majeshi ya Malaika kwa kutoonekana. Alleluia, Alleluia, Alleluia.

Tukiwa tumeona ufufuko wake Kristo tumsujudu Yesu Bwana Mtakatifu aliye pekee bila dhambi. Tunasujudu Msalaba wako. Ee Kristo, tena tunasifu na kutukuza ufufuko wako mtakatifu. Kwa kuwa wewe ndiwe Mungu wetu, tunajua wewe pekee, hatumjui mwingine , jina lako tunaliita. Njooni, enyi waumini wote, tusujudu ufufuko mtakatifu wa Kristo. Kwa kuwa kwa Msalaba furaha umefika dunia yote, tukimhimidi Bwana siku zote, tunasifu utukufu wake; kwa sababu akivumilia msalaba kwa ajili yetu, aliangamiza kifo kwa kifo chake.

Njooni, tumwinamie na tumsujudu Mungu mfalme wetu. Njooni, tumwinamie na tumsujudu Kristo yu Mungu mfalme wetu. Njooni, tumwinamie na tumsujudu yeye, Kristo aliye mfalme na Mungu wetu.

Ee Mungu, unirehemu, sawasawa na fadhili zako. Kiasi cha wingi wa rehema zako, uyafute makosa yangu. Unioshe kabisa na uovu wangu, unitakase dhambi zangu. Maana nimejua mimi makosa yangu, na dhambi yangu i mbele yangu daima. Nimekutendea dhambi Wewe peke yako, na kufanya maovu mbele za macho yako. Wewe ujulikane kuwa una haki unenapo, na kuwa safi utoapo hukumu. Tazama, mimi naliumbwa katika hali ya uovu; mama yangu alinichukua mimba hatiani. Tazama, wapendezwa na kweli iliyo moyoni; nawe utanijulisha hekima kwa siri, unisafishe kwa hisopo nami nitakuwa safi, unioshe, nami nitakuwa mweupe kuliko theluji. Unifanye kusikia furaha na shangwe, mifupa uliyoiponda ifurahi. Usitiri uso wako usitazame dhambi zangu; uzifute hatia zangu zote. Ee Mungu, uniumbie moyo safi, uifanye upya roho iliyotulia ndani yangu. Usinitenge na uso wako, wala roho yako mtakatifu usiniondolee. Unirudishie furaha ya wokovu wako; unitegemeze kwa roho ya wepesi. Nitawafundisha wakosaji njia zako, na wenye dhambi watarejea kwako. Ee MUNGU, Mungu wa wokovu wangu, uniponye na damu za watu, na ulimi wangu utaiiimba haki yako. Ee Bwana, uifumbue midomo yangu, na kinywa changu kitazinena sifa zako. Maana hupendezwi na dhabihu au ningeitoa, Wewe huridhii sadaka ya kuteketezwa. Dhabihu za Mungu ni roho iliyovunjika; moyo uliovunjika na kupondeka, Ee Mungu, hutaudharau.

Ee padri, inua.

Painulieni patakatifu mikono yenu, na kumhimidi BWANA.

Bwana Mungu, utukumbuke sisi sote katika ufalme wako, daima, sasa na siku zote, hata milele na milele.

WATU

Amina.

WATU

kwa kuwa mfalme wa wote tutamkaribisha. Akifuatwa na majeshi ya Malaika kwa kutoonekana. Alleluia, Alleluia, Alleluia.

SHEMASI

KASISI (kwa mnong''ono)

Uitendee mema Sayuni kwa radhi yako, uzijenge kuta za Yerusalemu. Ndipo utakapopendezwa na dhabihu za haki, na sadaka za kuteketezwa, na kafara. Ndipo watakapotoa ng''ombe juu ya madhabahu yako.

SHEMASI (kwa mnong''ono)

KASISI (kwa mnong''ono)

LITANIA YA KUMALIZIA

SHEMASI

Tumalize maombi yetu kwa Bwana.

( Bwana, hurumia. )

Kwa ajili ya Vipaji viheshimiwa vilivyowekwa mbele, tumwombe Bwana.

( Bwana, hurumia. )

Kwa ajili ya nyumba hii takatifu na waingiamo kwa imani, heshima na kumcha Mungu, tumwombe Bwana.

( Bwana, hurumia. )

Kwa ajili ya kuokolewa kwa kila sitikiko, ghadhabu, hatari na uhitaji, tumwombe Bwana.

( Bwana, hurumia. )

Utusaidie, utuokoe, utuhurumie, utuhifadhi, Ee Mungu, kwa neema yako.

( Bwana, hurumia. )

Siku hii yote iwe kamili, takatifu, tulivu na bila dhambi, tuombe kwa Bwana.

( Kidhi, Ee Bwana. )

Kwa ajili ya kuwa na Malaika wa amani, mwongozi mwaminifu, mlinzi wa roho zetu na miili yetu, tuombe kwa Bwana.

( Kidhi, Ee Bwana. )

Kwa ajili ya msamaha na maondoleo ya dhambi zetu na makosa yetu, tuombe kwa Bwana.

( Kidhi, Ee Bwana. )

Kwa ajili ya vitu vyema vifaavyo kwa roho zetu na amani ya dunia yote, tuombe kwa Bwana.

( Kidhi, Ee Bwana. )

Kwa ajili ya kumaliza maisha yetu yanayobaki kwa amani na toba, tuombe kwa Bwana.

( Kidhi, Ee Bwana. )

Tuombe ili mwisho wa maisha yetu uwe wa kikristo kwa amani, bila maumivu, aibu, tena tuone teto njema mbele ya kiti cha hukumu cha Kristo.

( Kidhi, Ee Bwana. )

Tumkumbuke Maria Mtakatifu kamili, asiye na doa, Mbarikiwa zaidi kushinda wote, Bibi wetu mtukufu mzazi Mungu na bikira daima pamoja na watakatifu wote hata sisi pia wenyewe na kila mmoja wetu na wenzetu wote, hata maisha yetu, kujiweka mikononi mwa Kristo Mungu.

( Kwako, Ee Bwana. )

SALA YA PROTHESI

KASISI (kwa mnong''ono)

Ee Bwana, uliye Mungu mwenye enzi na mtakatifu pekee, unayepokea dhabihu ya sifa ya hawa waliokuita kwa moyo wao wote, upokee hata maombi yetu sisi tulio na dhambi, na uyalete juu ya madhahabu yako matakatifu. Tena utujalie kukuletea vipaji na dhabihu za roho kwa ajili ya dhambi zetu na ya makosa ya mkutano. Tena utustahilishe kuona neema kwako, ili upezwe na dhabihu yetu, na Roho mwema wa neema yako akae juu yetu na juu vipaji hivi na watu wako wote.

KASISI

Kwa huruma za Mwana wako wa pekee, pamoja na wewe unayehimidiwa, na Roho wako Mtakatifu kamili, mwema, na mpaji wa uhai, sasa na sikuzote, hata milele na milele.

WATU

Amina.

KASISI

Amani kwa wote.

WATU

Na iwe kwa roho yako.

SHEMASI

Tupendane sisi kwa sisi, ili sote kwa nia moja tuungame.

WATU

Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu, Utatu wa asili moja, na asiyetengana.

Wewe, BWANA, nguvu zangu, nakupenda sana; BWANA ni jabali langu, na boma langu, na mwokozi wangu,

SHEMASI

Milango; milango; tusikilize kwa hekima.

WATU

Nasadiki Mungu mmoja, Baba, Mwenyezi, mwumba wa Mbingu, na Nchi, hata vyote vilivyo onekana na visivyo onekana. Tena Bwana mmoja, Yesu Kristo, Mwana wa pekee wa Mungu, aliyezaliwa na Baba kabla ya wakati wowote. Nuru toka Nuru, Mungu kweli toka Mungu kweli, aliyezaliwa, hakuumbwa, aliye wa asili moja na Baba, kwa yeye vyote vilifanya. Aliyeshuka mbinguni kwa ajili yetu wanadamu na ya wokovu wetu, akapata mwili kwa Maria bikira na kwa Roho Mtakatifu, hata kuwa mtu. Aliye sulubiwa kwa ajili yetu wakati wa enzi ya Pontio Pilato, akateswa, akawekwa kaburini. Aliyefufuka siku ya tatu, kama Maandiko yanenavyo. Akapaa mbinguni ndipo anapokaa kuume kwa Baba. Atakaye kuja mara ya pili kwa utukufu kuwahukumu wa hai na wafu; na ufalme wake utakuwa bila mwisho. Tena nasadiki Roho Mtakatifu, yu Bwana, yu mpaji wa uhai; anayetoka kwa Baba, anayesujudiwa na kutukuzwa pamoja na Baba na Mwana, aliyenena kwa midomo ya manabii. Tena nasadiki Ekklesia Moja, Takatifu, Katholiki na la Mitume. Naungama ubatizo moja kwa maondoleo ya dhambi. Natumaini ufufuo wa wafu, hata uzima wa ulimwengu utakaokuja. [[SWA]]

WATU

Amina.

SADAKA (ANAFORA) TAKATIFU

SHEMASI

Tusimame wima vizuri; tusimame wima kwa hofu; tuangalie kuleta sadaka (Anafora) takatifu kwa amani.

WATU

Huruma ya amani; dhabihu ya sifa.

KASISI

Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo, na upendo wa Mungu Baba, na ushirika wa Roho Mtakatifu, uwe na ninyi nyote.

WATU

Na iwe kwa roho yako.

KASISI

Tuweke mioyo juu.

WATU

Tumeiweka kwako ee Bwana

KASISI

Tumshukuru Bwana.

WATU

Ni wajibu na haki.

KASISI (kwa mnong''ono)

Ni wajibu na haki kukuimbia, kukuhimidi, kukusifu, kukushukuru na kukusujudu katika mahali popote pa utawala wako.Kwa kuwa wewe ndiwe Mungu usiye elezeka, usiye wazika usiye onekana, usiye chunguzika, usiye na mwanzo tangu milele, uliye sawa sawa nyakati zote, wewe na mwana wako wa pekee, na Roho wako Mtakatifu; wewe ulitufanya toka bure, na tukawa; na tuangakapo wewe hutusimamisha, na ulifanya vyovyote, mpaka kutupaza mbinguni ili kutupatia ufalme wako utakaokuja. Kwa ajili ya vyote hivi tuna kushukuru wewe, na Mwana wako wa pekee, na Roho wako Mtakatifu, tunakushukuru kwa ajili ya vitu vyote vinavyo onekana na visivyo onekana ulivyo tutendea. Tunashukuru hata kwa ajili ya Liturghia hii uliyokubali kuipokea kwa mikono yetu, ingawa wasimama mbele yako maelfu ya Malaika majemadari, na maelfu ya Malaika, Wakheruvi na Waserafi wenye mabawa sita, macho-mengi wanaopepea juu.

KASISI

Wakiimba na kulia, wakipaza sauti, na kusema wimbo wa shangwe.

WATU

Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu, Bwana Saboath (wa majeshi); nchi na mbingu zimejazwa na utukufu wako; Hosana mbinguni juu; mhimidiwa ajaye kwa jina la Bwana, Hosana uliye mbinguni juu.

KASISI (kwa mnong''ono)

Hata sisi pamoja na hao majeshi heri, tunapaza sauti, na kusema kuwa wewe, Ee Bwana wa Mabwana, mpenzi wa wanadamu; wewe ni Mtakatifu, Mtakatifu kamili, na Mwana wako wa pekee, na Roho Mtakatifu. Wewe ni Mtakatifu, Mtakatifu kamili, na utukufu wako adhimu; uliyependa ulimwengu wako jinsi hii, hata ukamtoa Mwana wako wa pekee, kusudi kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele; yeye, alipokuja na kumaliza chote kikusudiwacho na Mungu kwa ajili yetu, usiku ule alipotolewa, na zaidi alijitoa kwa ajili ya uzima wa ulimwengu, akichukua mkate mikononi yake mitakatifu na isiyo na doa. Akashukuru, akaubariki, akautakasa, akaumega na kuwapa wanafunzi wake na mitume wake watakatifu akisema.

KASISI

Twaeni, kuleni; huu ndiyo mwili wangu unaomegwa kwa ajili yenu, na kwa maondoleo ya dhambi.

WATU

Amina.

KASISI (kwa mnong''ono)

Sawasawa na kikombe baada ya kula akisema:

KASISI

Nyweni nyote na hii, hii ndiyo damu yangu iliyo ya agano jipya, imwagikayo kwa ajili yenu na ya wengi, kwa maondoleo ya dhambi.

WATU

Amina.

KASISI (kwa mnong''ono)

Kwa hivyo tukikumbuka amri hii ya kuleta wokovu, tena vyote vilivyo fanywa kwa ajili yetu, Msalaba, kaburi, ufufuko wa siku ya tatu, kupaa mbinguni, kukaa kuume na kuja mara ya pili kwa Utukufu.

KASISI

Vilivyo vyako kutoka vilivyo vyako, tunakuletea kadiri ya vyote na kwa ajili ya vyote.

WATU

Tunakuimbia,

(kwa mnong''ono)

Tena tunakuletea dhabihu hii ya akili na bila damu, na tuna kuomba na kukusihi na kukurongaronga (kukuuliza); utume Roho wako Mtakatifu juu yetu sisi na juu ya vipaji hivi vilivyo mbele.

Na ufanye mkate huu kuwa Mwili mheshimiwa wa Kristo wako.

( Amina. )

Na iliyo ndani ya kikombe hiki kuwa Damu heshimiwa ya Kristo wako.

( Amina. )

Kwa kuvigeuza kwa Roho wako Mtakatifu.

( Amina. Amina. Amina. )

Ili vitakuwa kwao wanao vipokea kuwaletea makesha ya roho, maondoleo ya dhambi, ushirika wa Roho wako Mtakatifu, utimilifu wa ufalme wa mbinguni, uthabiti mbele zako, bila kuwa na hatia au hukumu. Tena tunakuletea dhabihu hii ya akili kwa ajili yao walio rehemia katika imani, Manabii, Mababa, Mapatriaka, Mitume, Wahubiri, Mashahidi, Waungama, Watawa na kila roho ya mwenye haki aliye malizika katika imani.

KASISI

Kwa ajili ya Maria Mtakatifu kamili, asiye na doa, mbarikiwa zaidi kushinda wote, Bibi wetu mtukufu, Mzazi Mungu {Theotokos} na Bikira daima.

Wimbo wa Kumkuza Mariamu

Ni Wajibu kweli kukuita heri, Ee Mzazi Mungu (Theotokos), mbarikiwa daima na bila ndoa tena Mama wa Mungu wetu, uliye wa thamani kushinda Wakheruvi, unaye utukufu kupita bila kiasi Waserafi, uliye mzaa Mungu Neno bila kuharibu, uliye Mzazi – Mungu {Theotokos} kweli tuna kukuza wee.

KASISI (kwa mnong''ono)

Ya Yohana nabii, mtangulizi na mbatizaji; ya mitume watukufu na wasifiwa kamili; ya {Jina la mtakatifu wa siku}; hata ya Watakatifu wako wote; kwa maombi yao utujie , Ee Mungu, Na ukumbuke wote hawa waliolala katika matumaini ya ufufuo ya uzima milele (Majina); na kuwa rehemia mahali pa mwangaza wa nuru ya uso wako. Tena tunakusihi, ukumbuke, Ee Bwana , kila uaskofu, wa Orthodoksi, walioshika imara neno la ukweli wako, ukasisi wote, ushemasi katika Kristo, hata kila jeshi la ukasisi na la utawa. Tena tunakuletea ibada hii ya akili kwa ajili ya Ekklisia lako takatifu la ulimwengu wote, Katholiki na la Mitume, ya hawa wanaoishi katika usafi na mwenendo wa kiasi; ya watawala wetu, walio amini na kumpenda Kristo; wape kutawala katika amani; ili hata sisi tupite maisha yetu katika utulivu na shauri, kwa kila heshima ya Mungu na mwenendo mwema.

Ee Bwana, ya kwanza umkumbuke Askofu wetu mkuu (jina) na umlinde katika Ekklesia lako Takatifu, ili aishi maisha ya amani, uzima, heshima, afya na miaka kwa kushika imara neno la ukweli wako.

Hata hawa walio ndani ya fikira ya kila mmoja wetu; tena wanaume wote na wanawake wote.

WATU

Bwana, hurumia.

SHEMASI

Hata hawa walio ndani ya fikira ya kila mmoja wetu; tena wanaume wote na wanawake wote.

WATU

Wanaume wote na wanawake wote.

KASISI (kwa mnong''ono)

Ee Bwana, ukumbuke mji {au Monastiri} huu, na mahali hapa tunapokaa, hata kila mji na nchi, na hawa wanaokaa humo kwa imani. Uwakumbuke, Ee Bwana, wasafiri hewani, baharini na nchini kavu, wagonjwa, wachoshwa na mateka, na kwa ajili ya wokovu wao. Ee Bwana, uwakumbuke hawa wanaotenda matendo mema katika Maekklisia yako matakatifu na wakumbukao maskini; na utuletee sisi sote huruma yako.

KASISI

Na utujalie sisi ili kwa kinywa kimoja na moyo mmoja tutukuze na kusifu jina lako adhimu na heshimiwa, la Bwana na Mwana na Roho Mtakatifu, sasa na siku zote hata milele na milele.

WATU

Amina.

KASISI

Rehema za Yesu Kristo, Mungu Mwenye Enzi na Mwokozi wetu, ziwe pamoja na ninyi nyote.

WATU

Na ziwe kwa roho yako.

SHEMASI

Baada ya kuwakumbuka watakatifu wote, tena na tena kwa amani, tumwombe Bwana.

( Bwana, hurumia. )

Kwa ajili ya vipaji viheshimiwa vilivyo wekwa mbele na kutakaswa, tumwombe Bwana.

( Bwana, hurumia. )

Ili Mungu wetu mpenda wanadamu aliye vipokea katika madhabahu yake matakatifu, yaliyo ya mbinguni juu na ya kiroho, kuwa manukato ya harufu ya kiroho, aturudishie neema ya Mungu, na karama ya Roho Mtakatifu, tumwombe Bwana.

( Bwana, hurumia. )

Tukiomba umoja wa imani na ushirika wa Roho Mtakatifu, sisi na kila mmoja wetu, na wenzetu wote hata maisha yetu, kujiweka mikononi mwa Kristo Mungu.

( Kwako, Ee Bwana. )

KASISI (kwa mnong''ono)

Ee Bwana wa Mabwana, tunaweka maisha yetu na matumaini yetu mikononi mwako, na kukuomba, na kukusihi, na kukuuliza; utujalie kushiriki katika fumbo (sacramenti) zako za mbinguni na za kutisha sana; za Meza hii ya kiumungu na kiroho, kwa dhamira safi, tupate maondoleo ya dhambi, msamaha wa makosa, ushirika wa Roho Mtakatifu, urithi wa ufalme wa mbinguni, uthabiti mbele zako, bila kuwa na hatia au hukumu.

KASISI

Na utustahilishe, Ee Bwana wa Mabwana, tukiwa na uthabiti, bila hukumu, tuwe na ujasiri kukuita Baba, wewe Mungu uliye mbinguni, na kusema:

WATU

SALA LA BWANA

Baba yetu uliye Mbinguni; Jina lako litukuzwe; Ufalme wako uje; mapenzi yako yatimizwe, hapa Duniani kama huko Mbinguni. Utupe leo mkate wetu wa kila siku; na utusamehe deni zetu; kama sisi tuwasamehevyo wadeni wetu; tena usitutie majaribuni, lakini tuokoe na yule mwovu.

KASISI

Kwa kuwa ufalme ni wako, na nguvu, na utukufu, wa Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu, sasa na siku zote hata milele na milele.

( Amina. )

KASISI

Amani kwa wote.

( Na iwe kwa roho yako. )

SHEMASI

Tuinamishe vichwa vyetu kwa Bwana.

( Kwako, Ee Bwana. )

KASISI (kwa mnong''ono)

Tunakushukuru, Mfalme usiye onekana, kwa nguvu yako isiyopimika, umeviumba vyote, tena kwa wingi wa huruma zako umevitoa vyote toka bure, na vikawa. Wewe ndiwe, Ee Bwana wa Mabwana, utazame toka mbinguni juu ya hawa walioinama kwako vichwa vyao; Kwa kuwa hawainami kwa mwili na damu, ila kwako, uliye Mungu wa kutisha. Basi wewe, Bwana wa Mabwana, utupatie vipaji hivi vifae kila mmoja wetu kwa haja yake; usafiri pamoja nao wanao safiri baharini, hewani na nchini; uponye wagonjwa wewe uliye tabibu (daktari) wa roho na miili yetu.

KASISI

Kwa neema, na rehema, na upendo wa wanadamu wa Mwana wako wa pekee, pamoja na wewe mhimidiwa, na Roho wako Mtakatifu kamili, mwema na mpaji wa uhai, sasa na siku zote, hata milele na milele.

( Amina. )

USHIRIKA MTAKATIFU

KASISI (kwa mnong''ono)

Ee Bwana Yesu Kristo Mungu wetu, toka Maskani yako matakatifu na toka enzini mwako mwa utukufu wa ufalme wako, uangalie utujie na ututakase, wewe unayekaa juu pamoja na baba, tena hapa pamoja nasi bila kuonekana. Na ukubali kutushirikisha, kwa mkono wako, Mwili wako na Damu yako heshimiwa, na kwa mikono yetu kuwashirikisha washirika wote.

SHEMASI

Tusikilize.

KASISI

Vitu Vitakatifu kwa watu watakatifu wa Mungu.

WATU

Mtakatifu mmoja, Bwana ni mmoja, Yesu Kristo, kwa utukufu wa Mungu Baba. Amina.

WATU

Wimbo wa Ushirika Zaburi ya 148.

Haleluya. Msifuni BWANA kutoka mbinguni; msifuni katika mahali palipo juu. [[SWA]] Alleluia.

(Wimbo wa ushirika hubadilika kulingana na Sikukuu)


SHEMASI (kwa mnong''ono)

Ee Padri, mega Mkate Mtakatifu.

KASISI

Anamegwa na kugawanywa Mwana-kondoo wa Mungu, akatwaye kila mara bila kutengana, anayeliwa kila mara bila kumalizika, lakini awatakasa washiriki wake.

SHEMASI

Ee Padri, jaza kikombe kitakatifu.

KASISI

Ujazo wa Roho Mtakatifu.

SHEMASI (kwa mnong''ono)

Amina.

Ee Padri, bariki maji ya moto.

KASISI

Ubarikiwe umoto wa watakatifu wako, daima, sasa na sikuzote, hata milele na milele.

SHEMASI

Moto wa Roho Mtakatifu. Amina.

KASISI

Tazama, namjia Kristo, Mfalme asiyekufa na Mungu wetu

Mimi (jina), kasisi nisiyestahili, napewa Mwili mtakatifu na wa thamani wa Yesu Kristo, Bwana Mungu na Mwokozi wetu, kwa maondoleo ya dhambi zangu na uzima wa milele.

Ee Shemasi, uje.

SHEMASI

Tazama, namjia Kristo, Mfalme asiyekufa na Mungu wetu. Ee Padri, nipe mimi (jina), shemasi nisiyestahili, Mwili mtakatifu na wa thamani wa Yesu Kristo, Bwana Mungu na Mwokozi wetu, kwa maondoleo ya dhambi zangu na uzima wa milele.

KASISI

Wewe (jina), shemasi mtauwa, unapewa Mwili mtakatifu na wa thamani wa Yesu Kristo, Bwana Mungu na Mwokozi wetu, kwa maondoleo ya dhambi zako na uzima wa milele.

Tena, mimi (jina), kasisi nisiyestahili, napewa Damu heshimiwa, takatifu na ya uzima ya Yesu Kristo, Bwana Mungu na Mwokozi wetu, kwa maondoleo ya dhambi zangu na uzima wa milele.

Hii imegusa midomo yangu na kuondoa maovu yangu na kutakasa dhambi zangu.

Ee shemasi uje tena.

SHEMASI

Tena namjia Kristo. Ee Padri, nipe mimi (jina), shemasi nisiyestahili, Damu heshimiwa katifu na ya uzima ya Yesu Kristo, Bwana Mungu na Mwokozi wetu, kwa maondoleo ya dhambi zangu na uzima wa milele.

KASISI

Wewe (jina), shemasi mtauwa, unapewa Damu heshimiwa na takatifu ya Yesu Kristo, Bwana Mungu na Mwokozi wetu, kwa maondoleo ya dhambi zako na uzima wa milele.

Hii imegusa midomo yako, na kuondoa maovu yako na kutakasa dhambi zako.

SHEMASI

Kwa kumcha Mungu, kwa imani, na upendo mkaribie.

WATU

Na abarikiwe yeye ajaye kwa jina la BWANA; BWANA ndiye aliye Mungu, naye ndiye aliyetupa nuru.

Mtumwa {au mjakazi} wa Mungu {jina} anapewa Mwili na Damu ya Yesu Kristo Bwana wetu, kwa maondoleo ya dhambi na uzima wa milele.

WATU

Unipokee leo, Ee Mwana wa Mungu, kuwa mshiriki wa karamu yako ya fumbo (sakramenti); sitafunua kamwe fumbo lako kwa maadui wako, wala kukubusu kama Yuda; bali kama yule mnyang'anyi nauungama; unikumbuke, "Ee Bwana, katika ufalme wako."

Alleluia, Alleluia, a|leluia.


KASISI

Ee Mungu, waokoe watu wako na ubariki urithi wako.

WATU

Sauti 2.

Tumeona nuru ya ukweli, tumepata Roho wa mbinguni, tumeona imani kweli, tukimsujudu utatu asiotengwa; kwa kuwa huyu ametuokoa.

Ee Bwana, kwa Damu yako Takatifu uzifute dhambi za watu wako walio kumbukwa hapa, kwa maombi ya Mzazi–Mungu na watakatifu wako wote. Amina.

SHEMASI

Ee Padri, Paza

KASISI

Ee Mungu, utukuzwe juu ya mbingu, na juu ya nchi yote uwe utukufu wako.

Mhimidiwa ni Mungu wetu

KASISI

Daima sasa na sikuzote hata milele na milele.

( Amina. )

WATU

Acha vinywa vyetu vijawe na sifa zako, Ee Bwana, ili tuimbie Utukufu wako, kwa kuwa umetuwezesha kupokea Mistri yako, Takatifu, Isiyokufa na ya uzima. Tuhifadhi katika utakatifu wako, ili siku zote tutafakari juu ya haki zako. Alleluia Alleluia Alleluia.

SHEMASI

Simameni wima; baada ya kushiriki Fumbo (Sakramenti) la umungu takatifu, bila doa, la milele, la mbinguni juu, la uzima na kuogopa kweli, tumshukuru Bwana.

( Bwana, hurumia. )

Ama:

( Utukufu kwako, Ee Bwana, utukufu kwako. )

Utusaidie, utuokoe, utuhurumie, utuhifadhi, Ee Mungu, kwa neema yako.

( Bwana, hurumia. )

Tukimaliza kuomba siku hii yote iwe kamili, takatifu, tulivu bila dhambi, sisi na kila mmoja wetu na wenzetu wote, hata maisha yetu pia tujiweka mikononi mwa Kristo Mungu..

( Kwako, Ee Bwana. )

KASISI (kwa mnong''ono)

OMBI LA KUSHUKURU

Tunakushukuru, Ee Bwana mpenda wanadamu, mfadhili wa roho zetu kwa kuwa umetujalia tena kwa wakati huu kupoke Fumbo (Mistri} lako la mbinguni na la uzima. Uimarishe njia yetu sawasawa kwa ukweli; ututegemeze sisi sote katika hofu yako; ulinde maisha yetu, uzisalimishe hatua zetu; kwa sala na maombi ya Maria-Mzazi Mungu na Bikira daima na watakatifu wako wote.

KASISI

Kwa kuwa wewe ni utakaso wetu na kwako tunatoa utukufu, kwa Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu, sasa na sikuzote, hata milele na milele.

( Amina. )

KUMALIZIA

KASISI

Twende kwa amani.

SHEMASI

Tumwombe Bwana.

( Bwana, hurumia. )

OMBI LA KUMALIZA - APOLISI

KASISI

Ee Bwana, unayebariki wanao kuhimidi na unaye takasa wanao kutegemea, waokoe watu wako na ubariki urithi wako; ulinde ujazo wa Ekklesia lako; uwatakase wanaopenda uzuri wa nyumba Yako. Wewe uwape marudio ya utukufu kwa uweza wako wa Umungu; tena usituache sisi tunao kutumaini. Upatie dunia yako amani, tena Maekklesia Yako, Makasisi, Viongozi wetu, majeshi na watu wako wote. Kwa kuwa kila ukarimu wema na kila kipaji kilicho kamili kinatoka kwako juu, uliye Baba wa nuru; na kwako tunatoa utukufu, ushukuru na usujudu, kwa Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu, sasa na sikuzote hata milele na milele.

( Amina. )

WATU

Jina la BWANA lihimidiwe tangu leo na hata milele. (3)

KASISI (kwa mnong''ono)

Ee Kristo Mungu wetu, uliye ukamilifu wa sheria na wa Manabii, Uliye kamilisha makusudi yote ya Baba, ujaze mioyo yetu kwa furaha na shangwe, daima sasa na siku zote hata milele na milele. Amina.

SHEMASI

Tumwombe Bwana.

( Bwana, hurumia. )

KASISI

Baraka ya Bwana na huruma yake imfikie ninyi, kwa neema yake ya Umungu na upendo wake kwa wanadamu, daima, sasa na siku zote hata milele na milele.

( Amina. )

Utukufu kwako, Ee Kristo Mungu wetu na matumaini yetu, utukufu kwako.

WATU

Bwana hurumia, Bwana hurumia, Bwana hurumia.

KASISI

Yeye Kristo Mungu wetu wa kweli, kwa maombi ya Mama yake asiye na doa na asiye na waa, mtakatifu kamili; kwa nguvu ya msalaba wenye thamani na mpaji wa uhai; kwa ulinzi wa nguvu zisizo na mwili waheshimiwa wa mbinguni; kwa maombi ya Yohana, Nabii, mtangulizi na mbatizaji, mheshimiwa na wa sifa; ya Mitume watakatifu, watukufu na wasifiwa; ya mashahidi watakatifu, wasifiwa na washindaji wazuri; ya watawa watakatifu na wacha Mungu; (Mtakatifu wa Kanisa); ya watakatifu na wenye haki Yohakim na Anna; na ya watakatifu wote, atuhurumie na atuokoe, yu Mungu mwema, mrahimu na mpenda wanadamu.

WATU

Anayetubariki na kututakasa, Ee Bwana umlinde kwa miaka mingi.

KASISI

Kwa maombi ya mababa wetu watakatifu, Ee Bwana Yesu Kristo Mungu wetu, utuhurumie na utuokoe.

( Amina. )

KASISI

WATU

Anayetubariki na kututakasa, Ee Bwana umlinde kwa miaka mingi. [[SWA]]