Ibaada kwa Lugha Yangu
×




LITURGIA TAKATIFU ILIYO ANDIKWA NA MTAKATIFU YOHANA KRISOSTOMO

LITURGIA YA WAKATEKUMENI

Mwanzo.

Shemasi, akiwa amepokea baraka kwa Kasisi, anatoka nje ya Madhabahu, kupitia Mlango wa Kaskazini na anasimama mahali pake pa kawaida mbele ya Milango Mitakatifu, anasujudu mara tatu na kuanza:

Shemasi

Ee Padri, himidi.

[ Kama Shemasi hayupo, Kasisi anasoma maombi yote akiwa Madhabahuni. ]

Kasisi anainuwa Kitabu cha Injili Takatifu na anafanya ishara ya Msalaba juu ya Antimensio akisema kwa sauti nyofu:

Kasisi

Uhimidiwe Ufalme wa Baba na Mwana na Roho Mtakatifu, sasa na siku zote, hata milele na milele.

Watu

Amina.

Litania Kubwa ya Amani (Irinika)

Shemasi

Kwa amani tumwombe Bwana.

Watu

Bwana, hurumia.

Shemasi

Kwa ajili ya amani kutoka juu na ya wokovu wa roho zetu, tumwombe Bwana.

Watu

Bwana, hurumia.

Shemasi

Kwa ajili ya amani ya dunia yote na kusimama imara kwa Makanisa Matakatifu ya Mungu, na umoja wa wote, tumwombe Bwana.

Watu

Bwana, hurumia.

Shemasi

Kwa ajili ya nyumba hii takatifu na wanaoingia humu kwa imani, heshima na kumcha Mungu, tumwombe Bwana.

Watu

Bwana, hurumia.

Shemasi

Kwa ajili ya Wakristo Waorthodoksi wanaomcha Mungu, tumwombe Bwana.

Watu

Bwana, hurumia.

Shemasi

Kwa ajili ya Askofu wetu mkuu (jina), mapadri waheshimiwa, mashemasi katika Kristo, wateule na watu wote, tumwombe Bwana.

Watu

Bwana, hurumia.

Shemasi

Kwa ajili ya Taifa letu linalomcha Mungu, utawala na mamlaka yote ya nchi yetu, viongozi na majeshi yetu yanayompenda Kristo, tumwombe Bwana.

Watu

Bwana, hurumia.

Shemasi

Kwa ajili ya mji huu na miji yote na nchi zote na waishimo kwa imani, tumwombe Bwana.

Watu

Bwana, hurumia.

Shemasi

Kwa ajili ya majira mema ya mwaka, kupata mvua ya kutosha, hewa safi, rutuba ya kutosha kwa ardhi, na mazao ya kutosha tumwombe Bwana.

Watu

Bwana, hurumia.

Shemasi

Kwa ajili ya wanaosafiri angani, baharini na nchi kavu, na kwa ajili ya wagonjwa, wanaolemewa, mateka na kwa wokovu wao, tumwombe Bwana.

Watu

Bwana, hurumia.

Shemasi

Kwa ajili ya kuokolewa kwa kila sikitiko, ghadhabu, hatari na uhitaji, tumwombe Bwana.

Watu

Bwana, hurumia.

Shemasi

Utusaidie, utuokoe, utuhurumie, na utuhifadhi, Ee Mungu, kwa neema yako.

Watu

Bwana, hurumia.

Shemasi

Tumkumbuke Maria Mtakatifu kamili, asiye na doa, mbarikiwa zaidi kushinda wote, Mama yetu mtukufu, Mzazi-Mungu na Bikira daima, pamoja na watakatifu wote, tujiweke sisi wenyewe na kila mmoja wetu na wenzetu wote na maisha yetu yote mikononi mwa Kristo Mungu.

Wakati jina la Maria linapotajwa katika litania linalotangulia ni desturi watu kuimba, “ Mzazi Mungu Mtakatifu sana utuokoe. ”

Watu

Kwako. Ee Bwana.

Kasisi (Kwa mnong’ono)

Sala ya Antifono ya Kwanza

Ee Bwana, Mungu wetu, mwenye enzi yote na utukufu kupita kila ufahamu, uliye na huruma isiyopimika na upendo kwa wanadamu usioelezeka, wewe ndiwe Bwana wa mabwana, kulingana na huruma yako ututazame sisi na hekalu hili takatifu na utupatie sisi pamoja nao tunaokuomba huruma tele na rehema zako.

Kasisi (Kwa sauti.)

Kwa kuwa utukufu wote, heshima na usujudu ni haki yako, Baba, Mwana na Roho Mtakatifu, sasa na siku zote, hata milele na milele.

Watu

Amina.

Watu:

Antifono ya Kwanza

Kila JumaBwana (Jumapili) au katika sikukuu za watakatifu, Antifono ifuatayo kwa kawaida huimbwa.

Sauti ya Pili. Zaburi ya 102 (103 katika Swahili Union Version)

Mstari 1: Ee nafsi yangu, umhimidi Bwana. Naam, vyote vilivyo ndani yangu vilihimidi jina lake takatifu.

Kwa maombi ya Mzazi Mungu, Ee Mwokozi, utuokoe.

Mstari 2: Ee nafsi yangu, umhimidi Bwana, wala usizisahau fadhili zake zote.

Kwa maombi ya Mzazi Mungu, Ee Mwokozi, utuokoe.

Mstari 3: Bwana ameweka kiti chake cha enzi mbinguni, na ufalme wake unavitawala vitu vyote.

Kwa maombi ya Mzazi Mungu, Ee Mwokozi, utuokoe.

Utukufu kwa Baba na Mwana na Roho Mtakatifu, sasa na siku zote hata milele na milele. Amina.

Kwa maombi ya Mzazi Mungu, Ee Mwokozi, utuokoe.

Wakati Antifono hii ikiimbwa, Shemasi anasujudu na kuondoka mahali pake mbele ya Milango Mitakatifu, na kusimama mbele ya Picha Takatifu ya Mzazi Mungu, akitazama mbele ya Picha Takatifu ya Kristo, huku akishika orarioni yake kwa vidole vitatu vya mkono wake wa kulia.

Baada ya Antifono hurudi na husimama mahali pake pa kawaida, husujudu na kusema Litania Fupi.

Shemasi

LITANIA FUPI

Shemasi

Tena na tena kwa amani tumwombe Bwana.

Watu

Bwana, hurumia.

Shemasi

Utusaidie, utuokoe, utuhurumie, na utuhifadhi, Ee Mungu, kwa neema yako.

Watu

Bwana, hurumia.

Shemasi

Tumkumbuke Maria Mtakatifu kamili, asiye na doa, mbarikiwa zaidi kushinda wote, Mama yetu mtukufu, Mzazi-Mungu na Bikira daima, pamoja na watakatifu wote, tujiweke sisi wenyewe na kila mmoja wetu na wenzetu wote na maisha yetu yote mikononi mwa Kristo Mungu.

Wakati jina la Maria linapotajwa katika litania linalotangulia ni desturi watu kuimba, “ Mzazi Mungu Mtakatifu sana utuokoe. ”

Watu

Kwako. Ee Bwana.

Kasisi (Kwa mnong’ono)

Sala ya Antifono ya Pili

Ee Bwana, Mungu wetu, uwaokoe watu wako na ubariki urithi wako, uilinde jamii ya Kanisa lako, tena utakase hao wanaopenda uzuri wa nyumba yako, uwape utukufu kwa uweza wako wa Umungu, na usijitenge nasi tunaokutumaini wewe.

Kasisi (Kwa sauti.)

Kwa kuwa utawala ni wako na ufalme na uweza na utukufu ni vyako, Baba, Mwana na Roho Mtakatifu, sasa na siku zote, hata milele na milele.

Watu:

Amina.

Watu:

Antifono ya Pili

Kila JumaBwana au katika sikukuu za watakatifu tunaimba Antifono hii:

Sauti ya Pili. Zaburi ya 145 (146 katika Swahili Union Version).

(Mistari ya Zaburi huambatana na wimbo:)

Antifono ya Pili Sauti ya Pili.

Mstari 1: Ee nafsi yangu, umsifu Bwana. Nitamsifu Bwana muda ninaoishi, Nitamwimbia Mungu wangu ningali hai. [GB]

Ee Mwana wa Mungu, uliyefufuka katika wafu, utuokoe sisi twakuimbia: Aleluya!

Mstari 2: Heri ambaye Mungu wa Yakobo ni msaada wake, na tumaini lake ni kwa Bwana, Mungu wake.

Ee Mwana wa Mungu, uliyefufuka katika wafu, utuokoe sisi twakuimbia: Aleluya!

Mstari 3: Bwana atamiliki milele, Mungu wako, Ee Sayuni, kwa vizazi vyote.

Ee Mwana wa Mungu, uliyefufuka katika wafu, utuokoe sisi twakuimbia: Aleluya!

Utukufu kwa Baba na Mwana na Roho Mtakatifu.

Sasa na siku zote hata milele na milele. Amina.

Ee Mwana wa pekee tena Neno wa Mungu, ukiwa usiyekufa, ulikubali kwa ajili ya wokovu wetu, kupata mwili kwa Maria Mzazi Mungu tena Bikira daima, ukawa mtu bila kujigeuza; na ukasulubiwa, Ee Kristo Mungu, ukakanyaga kifo kwa kifo; ukiwa mmoja wa Utatu Mtakatifu na unatukuzwa pamoja na Baba na Roho Mtakatifu, utuokoe.

LITANIA FUPI

Shemasi

Tena na tena kwa amani tumwombe Bwana.

Watu

Bwana, hurumia.

Shemasi

Utusaidie, utuokoe, utuhurumie, na utuhifadhi, Ee Mungu, kwa neema yako.

Watu

Bwana, hurumia.

Shemasi

Tumkumbuke Maria Mtakatifu kamili, asiye na doa, mbarikiwa zaidi kushinda wote, Mama yetu mtukufu, Mzazi-Mungu na Bikira daima, pamoja na watakatifu wote, tujiweke sisi wenyewe na kila mmoja wetu na wenzetu wote na maisha yetu yote mikononi mwa Kristo Mungu.

Wakati jina la Maria linapotajwa katika litania linalotangulia ni desturi watu kuimba, “ Mzazi Mungu Mtakatifu sana utuokoe. ”

Watu

Kwako. Ee Bwana.

Kasisi (Kwa mnong’ono)

Sala ya Antifono ya Tatu

Ee Bwana uliyetupatia sala hizi za pamoja; na uliyeahidi kwamba watu wawili au watatu watakapo patana kwa jina lako, utatimiza dua zao; timiza hata sasa dua za watumishi wako iwafaavyo, na utupatie ujuzi wa kujua kamili ukweli wako katika maisha haya, tena uzima wa milele katika maisha yajayo.

Kasisi (Kwa sauti.)

Kwa kuwa wewe ni Mungu Mwema na mpenda wanadamu, na tunatoa utukufu kwako Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu, sasa na siku zote, hata milele na milele.

Watu:

Amina.

Watu:

Antifono ya Tatu

(Mistari ifaayo ya zaburi huambatana na Apolitikio)


Sauti ya Wiki: Zaburi 117 (118 katika Swahili Union Version)

1 Mshukuruni BWANA kwa kuwa ni mwema, Kwa maana fadhili zake ni za milele.

Kisha Apolitikio ya Ufufuko huimbwa kwa sauti ya wiki.

2 Wamchao BWANA na waseme sasa, Ya kwamba fadhili zake ni za milele.

Kisha tunarudia Apolitikio ya Ufufuko.

3 Siku hii ndiyo aliyoifanya BWANA, Tutashangilia na kuifurahia.

Kisha tunarudia Apolitikio ya Ufufuko.

KUINGIA KUDOGO

Apolitikio inapoimbwa, Kasisi na Shemasi wanasujudu mara tatu mbele ya Meza Takatifu. Kisha Kasisi anampa Injili Takatifu Shemasi ambaye anabusu mkono wa Kasisi anapoipokea na kisha kuzunguka Meza Takatifu na Kasisi akimfuata. Wakitanguliwa na wahudumu wa Madhabahu wanaoshika mishumaa na Makerubi. Wakitoka kupitia Mlango wa Kaskazini, kwa kile kiitwacho Kuingia Kudogo. (Ikiwa Shemasi hayupo, Kasisi huchukua Injili Takatifu na kuishika mbele ya uso wake.) Wanapofika katikati ya Kanisa, wanasimama na kuinamisha vichwa vyao.

Shemasi anasema kwa mnong'ono:

Shemasi (Kwa mnong’ono)

Tumwombe Bwana.

Kasisi (Kwa mnong’ono)

Ee Mfalme, Bwana, Mungu wetu, uliyeweka mbinguni makundi ya majeshi ya Malaika, na Malaika majemadari kuadhimisha utukufu wako, ufanye kuingia kwetu kuwe pamoja na Malaika watakatifu, wanao adhimisha pamoja nasi tukiutukuza wema wako. Kwa kuwa utukufu wote, heshima na usujudu ni haki yako, Baba, Mwana na Roho Mtakatifu, sasa na siku zote, hata milele na milele.

Shemasi (Kwa mnong’ono)

Ee padri, bariki kuingia kutakatifu.

Kubarikiwe kuingia kwa patakatifu pako, daima sasa na siku zote, hata milele na milele. Amina.

Shemasi

Hekima! Simameni wima!

Watu:

Sauti ya Pili.

Njooni tumsujudie, na kumwangukia, Kristo, Ee Mwana wa Mungu, uliyefufuka katika wafu, utuokoe sisi twakuimbia: Aleluya!


__________

Ee Mwana wa Mungu, uliye wa ajabu katika watakatifu utuokoe sisi twakuimbia: Aleluya!

Mhimidini Mungu katika mikutano, Bwana katika makusanyiko ya Israeli. Ee Mwana wa Mungu, uliyefufuka katika wafu, utuokoe sisi twakuimbia: Aleluya!

Utukufu kwa Baba na Mwana na Roho Mtakatifu, sasa na siku zote hata milele na milele. Amina.

Uliye ulinzi wa Wakristo, usiyeaibika, umneneaji kwa Muumba usiyebadilika, usidharau sauti za maombi ya wenye dhambi, lakini tangulia kama mwema we kutusaidia sisi, wenye kupaza sauti kwako. Harakisha kututetea, na ufanye hima kutuombea, uliyemtunza daima, wanaokuheshimu, Ee Mzazi Mungu. [GB]

Shemasi

Tumwombe Bwana.

Watu:

Bwana, hurumia.

Kasisi (Kwa mnong’ono)

Sala ya Wimbo wa Takatifu Tatu

Ee Mungu Mtakatifu, unayekaa mahali patakatifu, unayeimbiwa na Maserafi kwa sauti takatifu, na kutukuzwa na Makerubi, na kusujudiwa na Majeshi yote ya mbinguni; uliyeumba vitu vyote kutoka utupu, uliyemuumba mtu kwa mfano na sura yako, tena kumpamba kwa kila kipaji chako; unayempa anayekuomba hekima na ufahamu, usiyemwacha mwenye dhambi, bali umeweka toba ili aokolewe; umetustahilisha watumishi wako wanyenyekevu na wasiostahili, hata wakati huu kusimama mbele ya utukufu wa madhabahu yako takatifu, na kukuletea kusujudu na sifa iliyo haki yako. Pokea, Ee Mwenye enzi, hata kutoka katika vinywa vyetu sisi wenye dhambi wimbo huu Mtakatifu unaoimbwa mara tatu na utujie kwa wema wako. Utusamehe dhambi zetu tulizozifanya kwa hiari na si kwa hiari; utakase nafsi na miili yetu; na utuwezeshe kukuabudu kwa utakatifu siku zote za maisha yetu; kwa maombi ya Mzazi Mungu Mtakatifu na ya Watakatifu wote waliokupendeza tangu kale.

Kasisi (Kwa sauti.)

Kwa kuwa wewe ndiwe Mtakatifu, Mungu wetu, na tunatoa utukufu kwako, Baba, Mwana na Roho Mtakatifu, sasa na siku zote,

Shemasi

hata milele na milele.

Watu:

Amina.

Mungu Mtakatifu, Mweza Mtakatifu, Usiyekufa Mtakatifu, utuhurumie.

Utukufu kwa Baba na Mwana na Roho Mtakatifu. Sasa na siku zote hata milele na milele. Amina.

Usiyekufa Mtakatifu, utuhurumie.

Shemasi

Kwa nguvu.

Watu:

Kwa nguvu.

Mungu Mtakatifu, Mweza Mtakatifu, Usiyekufa Mtakatifu, utuhurumie.

Shemasi (Kwa mnong’ono)

Ee Padri, Amuru.

Kasisi (Kwa mnong’ono)

Abarikiwe ajaye kwa jina la Bwana.

Shemasi (Kwa mnong’ono)

Ee Padri himidi kiti cha Enzi kilicho juu.

Kasisi (Kwa mnong’ono)

Mhimidiwa ni wewe uliye katika kiti cha Enzi cha ufalme wako, uketiye begani mwa Makerubi, daima, sasa na siku zote, hata milele na milele.

Shemasi

Tusikilize.

Kasisi

Amani kwa wote.

Watu:

Na iwe rohoni mwako.

Shemasi

Hekima!

Shemasi

Tusikilize.

Shemasi

Hekima!

Shemasi

Tusikilize.

Kasisi

Amani kwako msomaji.

Watu:

Aleluya. Aleluya. Aleluya.

Kasisi (Kwa mnong’ono)

Ee Mfalme, mpenda wanadamu, angazia mioyo yetu na nuru yako takatifu ya ujuzi wa kumjua Mungu; tena ufungue macho ya fikra zetu, ili tufahamu mahubiri ya Injili yako. Uweke ndani yetu hofu ya amri zako zenye heri, kusudi tupate kuzikanyaga tamaa mbaya zote za kimwili, na kufuata njia ya kuishi kiroho, hata kufikiri na kufanya vyote vinavyo kupendeza. Kwa kuwa wewe ndiwe mwangaza wa roho na miili yetu, Ee Kristo Mungu, na kwako tunatoa utukufu, pamoja na Baba yako asiye na mwanzo, na Roho wako Mtakatifu kamili, mwema na mpaji wa uhai, sasa na siku zote hata milele na milele. Amina.

(jina)

Kasisi

(jina)

Amina.

Shemasi

Hekima! Simameni wima! Tusikilize Injili Takatifu.

Kasisi

Amani kwa wote.

Watu:

Na iwe rohoni mwako.

Shemasi

Somo kutoka katika Injili Takatifu ilivyo andikwa na (Mathayo, Marko, Luka, Yohana) Mtakatifu.

Kasisi

Tusikilize.

Watu:

Utukufu kwako Ee Bwana, utukufu kwako.

Shemasi

Kasisi

Amani kwako.

Watu:

Utukufu kwako Ee Bwana, utukufu kwako.


Shemasi

Tuseme sisi sote kwa roho zetu zote na kwa mawazo yetu yote, tuseme.

( Bwana, hurumia. )


Ee Bwana Mwenyezi, Mungu wa baba zetu tunakuomba, utusikilize na utuhurumie.

( Bwana, hurumia. )


Utuhurumie Ee Mungu kadiri ya huruma yako kubwa tunakuomba utusikilize na utuhurumie.

( Bwana, hurumia. )


Tena tunaomba kwa ajili ya Askofu wetu mkuu (jina)

Tena tunaomba kwa ajili ya watumishi, wamchao Mungu, Wakristo wote Waorthodoksi, wanaokaa au kutembelea katika mji huu na nchi hii, washirika, viongozi, wasaidizi, wanaoweka wakfu katika kanisa hili takatifu, ili wapewe huruma, uzima, amani, afya, wokovu, msaada, msamaha na maondoleo ya dhambi.

Tena tunaomba kwa ajili ya wenyeheri, wanaokumbukwa milele, waasisi wa Kanisa hili takatifu; hata baba zetu na ndugu zetu wote na Waorthodoksi wote waliolala, ambao wamezikwa kwa uchaji hapa na mahali popote.

Tena tunaomba kwa ajili ya wanaoleta matoleo, wanaotunza uzuri wa hekalu takatifu na heshimiwa, wenye juhudi, waimbaji, hata watu wote wanaosimama hapa, wakitumaini huruma yako tele.

Sala ya Litania Ndefu

Kasisi (Kwa mnong’ono)

Ee Bwana, Mungu wetu, tunakusihi uyapokee maombi haya ya kina ya watumishi wako, na utuhurumie kadiri ya wingi wa huruma yako, utupatie rehema zako na watu wako wote wanaotumaini huruma yako tele.

Kasisi

Kwa kuwa wewe ndiwe Mungu mrahimu na mpenda wanadamu; na tunatoa utukufu kwako Baba, Mwana na Roho Mtakatifu, sasa na siku zote, hata milele na milele.

( Amina. )

Shemasi

Enyi wakatekumeni, ombeni kwa Bwana.

( Bwana, hurumia. )

Sisi waumini tuwaombee wakatekumeni.

( Bwana, hurumia. )

Ili Bwana awahurumie.

( Bwana, hurumia. )

Ili awafundishe neno la ukweli.

( Bwana, hurumia. )

Ili awafunulie Injili ya haki.

( Bwana, hurumia. )

Ili awaunganishe na Kanisa lake Takatifu, Katoliki na la Mitume.

( Bwana, hurumia. )

Uwaokoe, uwahurumie, uwasaidie na uwahifadhi, Ee Mungu, kwa neema yako.

( Bwana, hurumia. )

Enyi wakatekumeni, inamisheni vichwa vyenu kwa Bwana.

( Kwako. Ee Bwana. )

Kasisi (Kwa mnong’ono)

Ee Bwana, Mungu wetu, unayekaa juu, na kutazama wanyenyekevu wako, uliyemtuma Mwanao wa pekee, Bwana Mungu wetu, Yesu Kristo, kwa ajili ya wokovu wa wanadamu: uwatazame watumishi wako, wakatekumeni, walioinamisha shingo zao mbele yako, wastahilishe wakati mwafaka kuoshwa kwa kuzaliwa upya, na kuondolewa dhambi na kupewa vazi lisiloharibika, uwaunganishe na Kanisa lako Takatifu, Katoliki na la Mitume, na uwahesabie katika kundi lako teule.

Kasisi

Ili hata hawa walitukuze pamoja nasi jina lako adhimu na linaloheshimiwa sana, la Baba, Mwana na Roho Mtakatifu, sasa na siku zote hata milele na milele.

( Amina. )

Shemasi

Walio wakatekumeni, tokeni. Enyi wakatekumeni, tokeni. Walio wakatekumeni, tokeni. Mtu mkatekumeni asikae ndani.

Tuliowaumini, tena na tena kwa amani tumwombe Bwana.

( Bwana, hurumia. )

Utusaidie, utuokoe, utuhurumie, na utuhifadhi, Ee Mungu, kwa neema yako.

( Bwana, hurumia. )

Hekima!

Kasisi (Kwa mnong’ono)

Tunakushukuru, Ee Bwana, Mungu wa majeshi uliyetustahilisha hata wakati huu kusimama mbele ya madhabahu yako takatifu na kusujudu mbele ya rehema zako, tukiomba huruma yako kwa ajili ya dhambi zetu na makosa ya watu ya kutokujua. Ee Mungu, upokee sala yetu, na utustahilishe kukuletea maombi, dua na dhabihu isiyo ya damu, kwa ajili ya watu wako wote; na uliotuweka katika utumishi huu, utuwezeshe kwa uwezo wa Roho wako Mtakatifu, ili tunapokuita wakati wowote na mahali popote bila lawama na vikwazo, kwa dhamiri safi, utusikilize na utuhurumie kadiri ya wingi wa wema wako.

Kasisi

Kwa kuwa utukufu wote, heshima na usujudu ni haki yako, Baba, Mwana na Roho Mtakatifu, sasa na siku zote, hata milele na milele.

( Amina. )

Shemasi

Tena na tena kwa amani tumwombe Bwana.

( Bwana, hurumia. )

Utusaidie, utuokoe, utuhurumie, na utuhifadhi, Ee Mungu, kwa neema yako.

( Bwana, hurumia. )

Hekima!

Kasisi (Kwa mnong’ono)

Tena na mara nyingi tunakusujudu na kukuomba, wewe uliyemwema na mpenda wanadamu, ili unaposikia maombi yetu usafishe roho zetu na miili yetu na kila unajisi wa mwili na wa roho, tena utupe kusimama mbele ya madhabahu yako bila hatia na hukumu. Hata uwape hao wanaosali pamoja nasi maendeleo ya maisha, imani na hekima ya roho, uwajalie kukuabudu daima kwa hofu na upendo, tena kushiriki ushirika wako, wastahilishe kuingia katika ufalme wako wa mbinguni juu.

Kasisi

Ili tukilindwa daima kwa kutawala kwako, tutoe utukufu kwa Baba, Mwana na Roho Mtakatifu, sasa na siku zote hata milele na milele.

( Amina. )

Watu:

Kama Makerubi, kwa siri tunaofanana na tunaoimbia Utatu Mpaji wa uhai wimbo [ Mtakatifu-Utatu ] [ Tatu-Takatifu ] tuweke mbali kila tafakari ya maisha. Kwa kuwa Mfalme wa wote tunamkaribisha.

Kasisi (Kwa mnong’ono)

Hakuna mtu wa tamaa na anasa za mwili anayestahili kukujia au kukukaribia na kukuabudu, Ee Mfalme wa utukufu; kwa sababu kukutumikia ni kwa hofu sana, hata kwa Majeshi ya mbinguni: Lakini, kwa ajili ya upendo kwa wanadamu umekuwa mtu bila kubadilika na bila kujigeuza na umekuwa Kuhani wetu Mkuu; na wewe ndiwe umetupatia kuadhimisha dhabihu hii isiyo na damu, wewe uliye Mtawala wa vyote. Kwa kuwa ndiwe, Bwana Mungu wetu wa pekee unatawala vilivyo mbinguni na duniani, unayebebwa na Makerubi, ambacho ni kiti chako cha enzi, uliye Bwana wa Maserafi tena Mfalme wa Israeli. Ndiwe Mtakatifu pekee, unayekaa mahali patakatifu, basi nakusihi wewe uliye mwema pekee na kusikia vema; uniangazie mimi mtumishi wako mwenye dhambi na nisiyefaa; utakase roho na moyo wangu na kila dhamiri mbaya; tena unijalie kwa nguvu ya Roho Mtakatifu, ili nikivaa neema ya ukasisi, nisimame mbele ya Meza yako hii Takatifu; na kuadhimisha Mwili wako Mtakatifu wa usafi na Damu yako ya thamani. Kwa kuwa nakujia wewe, nikiinamisha shingo yangu, nakusihi, usinifiche uso wako na usinikatae kuwa miongoni mwa watumishi wako; bali unistahilishe mimi mtumishi wako nisiyestahili, kukuletea vipaji hivi. Kwa kuwa wewe ndiwe unayetoa na unayetolewa, unayepokea tena unayegawanywa, Ee Kristo Mungu wetu, na kwako tunatoa utukufu, pamoja na Baba yako asiye na mwanzo na Roho wako Mtakatifu kamili, mwema na mpaji wa uhai, sasa na siku zote, hata milele na milele. Amina.

Kasisi

Kama Makerubi, kwa siri tunaofanana na tunaoimbia Utatu Mpaji wa uhai wimbo [ Mtakatifu-Utatu ] [ Tatu-Takatifu ] tuweke mbali kila tafakari ya maisha.

Shemasi

Kwa kuwa Mfalme wa wote tunamkaribisha. Akifuatwa na majeshi ya Malaika kwa kutoonekana. Alleluia, Alleluia, Alleluia.

Tukiwa tumeona ufufuko wake Kristo tumsujudu Yesu Bwana Mtakatifu aliye pekee bila dhambi. Tunasujudu msalaba wako, Ee Kristo, tena tunasifu na kutukuza ufufuko wako mtakatifu. Kwa kuwa wewe ndiwe Mungu wetu, tunakujua wewe pekee, hatumjui mwingine, jina lako tunaliita. Njooni, enyi waumini wote, tusujudu ufufuko mtakatifu wa Kristo. Kwa kuwa kwa msalaba furaha imefika katika dunia yote. Tukimhimidi Bwana siku zote, tunasifu utukufu wake. Kwa sababu akivumilia msalaba kwa ajili yetu, aliangamiza kifo kwa kifo chake.

Njooni, tumwinamie na tumsujudu Mungu mfalme wetu. Njooni, tumwinamie na tumsujudu Kristo yu Mungu Mfalme wetu. Njooni, tumwinamie na tumsujudu yeye Kristo, aliye Mfalme na Mungu wetu.

Ee Mungu, uniumbie moyo safi, Uifanye upya na kuithibiti roho yangu. Usinitenge na uso wako, Wala roho yako mtakatifu usiniondolee.

Mnisamehe.

Ee Mungu, uniwie radhi mimi mtu mwenye dhambi na unihurumie.

Ee padri, inua.

Bwana Mungu, atukumbuke sisi sote katika ufalme wake, daima, sasa na siku zote, hata milele na milele.

Watu:

Amina.

Watu:

Kwa kuwa Mfalme wa wote tunamkaribisha. Akifuatwa na majeshi ya Malaika kwa kutoonekana. Alleluia, Alleluia, Alleluia.

Bwana Mungu aukumbuke ukasisi wako katika ufalme wake, daima, sasa na siku zote hata milele na milele.

Bwana Mungu aukumbuke ushemasi wako katika ufalme wake, daima sasa na siku zote hata milele na milele .

Mheshimiwa Yosefu alipotoa mwili wako mtakatifu kutoka kwa mti, aliuweka kwenye sanda safi, akaupaka manukato mazuri, akaulaza kwenye kaburi jipya.

Shemasi

Ee Padri, utende mema.

Kasisi (Kwa mnong’ono)

Ee ndugu yangu tunayeadhimisha pamoja, unikumbuke.

Shemasi (Kwa mnong’ono)

Kasisi (Kwa mnong’ono)

Roho mwenyewe ataadhimisha pa- moja nasi siku zote za maisha yetu.

Amina. Amina. Amina. Iwe kwangu kama ulivyosema.

Shemasi

Tumalize maombi yetu kwa Bwana.

( Bwana, hurumia. )

Kwa ajili ya Vipaji viheshimiwa vilivyowekwa mbele, tumwombe Bwana.

( Bwana, hurumia. )

Kwa ajili ya nyumba hii takatifu na wanaoingia humu kwa imani, heshima na kumcha Mungu, tumwombe Bwana.

( Bwana, hurumia. )

Kwa ajili ya kuokolewa kwa kila sikitiko, ghadhabu, hatari na uhitaji, tumwombe Bwana.

( Bwana, hurumia. )

Utusaidie, utuokoe, utuhurumie, na utuhifadhi, Ee Mungu, kwa neema yako.

( Bwana, hurumia. )

Siku hii yote iwe kamili, takatifu, tulivu na bila dhambi, tuombe kwa Bwana.

( Tujalie, Ee Bwana. )

Kwa ajili ya kuwa na Malaika wa amani, mwongozi mwaminifu, mlinzi wa roho zetu na miili yetu, tuombe kwa Bwana.

( Tujalie, Ee Bwana. )

Kwa ajili ya msamaha na maondoleo ya dhambi zetu na makosa yetu, tuombe kwa Bwana.

( Tujalie, Ee Bwana. )

Kwa ajili ya vitu vyema vifaavyo kwa roho zetu na amani ya dunia yote, tuombe kwa Bwana.

( Tujalie, Ee Bwana. )

Kwa ajili ya kumaliza maisha yetu yanayobaki kwa amani na toba, tuombe kwa Bwana.

( Tujalie, Ee Bwana. )

Tuombe ili mwisho wa maisha yetu uwe wa kikristo kwa amani, bila maumivu, aibu tena utetezi mwema mbele ya kiti cha hukumu cha Kristo.

( Tujalie, Ee Bwana. )

Tumkumbuke Maria Mtakatifu kamili, asiye na doa, mbarikiwa zaidi kushinda wote, Mama yetu mtukufu, Mzazi-Mungu na Bikira daima, pamoja na watakatifu wote, tujiweke sisi wenyewe na kila mmoja wetu na wenzetu wote na maisha yetu yote mikononi mwa Kristo Mungu.

( Kwako. Ee Bwana. )

Kasisi (Kwa mnong’ono)

Ee Bwana, uliye Mungu mwenye enzi na mtakatifu pekee, unayepokea dhabihu ya sifa ya hawa wanaokuita kwa mioyo yao yote, upokee hata maombi yetu sisi tulio na dhambi, na uyalete juu ya madhahabu yako matakatifu. Tena utujalie kukuletea vipaji na dhabihu za roho kwa ajili ya dhambi zetu na ya makosa ya watu. Tena utustahilishe kuona neema mbele yako, ili upendezwe na dhabihu yetu, na Roho mwema wa neema yako akae juu yetu, juu ya vipaji hivi na juu ya watu wako wote.

Kasisi

Kwa huruma za Mwana wako wa pekee, pamoja na wewe unayehimidiwa, na Roho wako Mtakatifu kamili, mwema, na mpaji wa uhai, sasa na sikuzote, hata milele na milele.

Watu:

Amina.

Kasisi

Amani kwa wote.

Watu:

Na iwe rohoni mwako.

Shemasi

Tupendane sisi kwa sisi, ili sote kwa nia moja tuungame.

Watu:

Baba, Mwana na Roho Mtakatifu, Utatu wa asili moja, na asiyetengana.

Kristo yupo katikati yetu. Alikuwepo, yupo na atakuwepo.

Shemasi

Milango; milango; tusikilize kwa hekima.

Watu

Ninasadiki kwa Mungu mmoja, Baba Mwenyezi, Muumba mbingu na nchi, na vitu vyote vinavyoonekana na visivyoonekana. Tena Bwana mmoja, Yesu Kristo , Mwana wa pekee wa Mungu, aliyezaliwa na Baba kabla ya wakati wowote. Nuru toka nuru, Mungu kweli kutoka kwa Mungu kweli, aliyezaliwa, hakuumbwa, mwenye asili moja na Baba, ambaye vitu vyote viliumbwa na Yeye. Alishuka kutoka mbinguni kwa ajili yetu wanadamu na kwa ajili ya wokovu wetu, akapata mwili kwa Maria Bikira na kwa Roho Mtakatifu, akawa mwanadamu. Akasulubiwa kwa ajili yetu wakati wa enzi ya Pontio Pilato, akateswa, akazikwa. Alifufuka siku ya tatu, kama Maandiko yanavyonena. Akapaa mbinguni; amekaa kuume kwa Baba. Atakuja tena katika utukufu kuwahukumu wazima na wafu; ambaye ufalme wake hautakuwa na mwisho. Tena nasadiki kwa Roho Mtakatifu, yu Bwana, yu mpaji wa uhai; anayetoka kwa Baba; anayesujudiwa na kutukuzwa pamoja na Baba na Mwana, aliyenena kwa vinywa vya manabii. Tena, kwa kanisa moja, takatifu, katoliki na la Mitume. Naungama ubatizo mmoja kwa maondoleo ya dhambi. Ninangojea ufufuko wa wafu, na uzima wa milele utakaokuja. [GB]

Watu:

Amina.

Shemasi

Tusimame wima vizuri; tusimame wima kwa hofu; tuangalie kuleta sadaka takatifu (Anafora) kwa amani.

Watu:

Huruma ya amani; dhabihu ya sifa.

Kasisi

Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo, na upendo wa Mungu Baba, na ushirika wa Roho Mtakatifu, uwe na ninyi nyote.

Watu:

Na [iwe] [uwe] [viwe] rohoni mwako.

Kasisi

Tuinue mioyo yetu juu.

Watu:

Tumeiinua kwa Bwana.

Kasisi

Tumshukuru Bwana.

Watu:

Ni wajibu na haki.

Kasisi (Kwa mnong’ono)

Ni wajibu na haki kukuimbia, kukuhimidi, kukusifu, kukushukuru, kukusujudu katika mahali popote pa utawala wako. Kwa kuwa wewe ndiwe Mungu usiyeelezeka, usiyewazika, usiyeonekana, usiyechunguzika, uishiye milele, uliye sawa nyakati zote, wewe na Mwana wako wa pekee, na Roho wako Mtakatifu. Wewe uliyetufanya toka utupu na tukawa na tulipokuwa tumeanguka, wewe ulituinua tena, na hukuchoka kufanya yote, mpaka kutupaliza mbinguni, na kutupatia ufalme wako utakaokuja. Kwa ajili ya haya yote tunakushukuru wewe, na Mwana wako wa pekee, na Roho wako Mtakatifu, tunakushukuru kwa wema wote uliotutendea, tunaoujua na tusioujua, unaoonekana na usioonekana. Tunakushukuru hata kwa ajili ya Liturgia hii uliyokubali kuipokea kutoka mikononi mwetu, ingawa wanasimama mbele yako maelfu ya Malaika wakuu na makumi elfu ya Malaika, Makerubi na Maserafi, wenye mabawa sita, macho mengi wakipepea juu [wakikaa hewani] [wakikaa angani].

Kasisi

Wakiimba wimbo wa ushindi, wakishangilia, wakipaza sauti kuu, nakusema:

Watu:

Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu, Bwana Sabaothi, nchi na mbingu zimejazwa utukufu wako. Hosana, juu mbinguni, mhimidiwa ajaye kwa jina la Bwana, Hosana, uliye juu mbinguni.

Kasisi (Kwa mnong’ono)

Na sisi pia pamoja na hawa Majeshi wenye heri, tunapaza sauti, na kusema kwako, Ee Mfalme mpenda wanadamu, wewe ni Mtakatifu na Mtakatifu kamili na Mwana wako wa pekee na Roho wako Mtakatifu. Wewe ni Mtakatifu na Mtakatifu kamili, na utukufu wako adhimu. Uliyeupenda ulimwengu wako jinsi hii, hata ukamtoa Mwana wako wa pekee kusudi kila mtu anayemwamini asipotee, bali awe na uzima wa milele. Yeye, alipokuja na kukamilisha chote kilichokusudiwa na Mungu kwa ajili yetu, usiku ule alitolewa na zaidi alijitoa kwa ajili ya uzima wa ulimwengu, akachukua mkate katika mikono yake mitakatifu isiyo na doa, akashukuru, akaubariki, akautakasa, akaumega na akawapa Wanafunzi na Mitume wake Watakatifu akasema:

Kasisi

Twaeni, kuleni; huu ndio mwili wangu unaomegwa kwa ajili yenu, kwa maondoleo ya dhambi.

Watu:

Amina.

Kasisi (Kwa mnong’ono)

Vivyo hivyo baada ya kula akachukua kikombe akisema:

Kasisi

Nyweni nyote katika hiki, hii ndiyo Damu yangu ya Agano Jipya, imwagikayo kwa ajili yenu na ya wengi, kwa maondoleo ya dhambi.

Watu:

Amina.

Kasisi (Kwa mnong’ono)

Kwa hiyo tukikumbuka amri hii ya kutuletea wokovu, tena vyote vilivvofanywa kwa ajili yetu, Msalaba, kaburi, ufufuko baada ya siku tatu, kupaa mbinguni, kuketi kuume, na kuja mara ya pili kwa utukufu.

Kasisi

Vilivyo vyako kutoka vilivyo vyako, tunakutolea kadiri ya vyote na kwa ajili ya vyote.

Watu:

Tunakuimbia, tunakuhimidi, tunakushukuru, Ee Bwana, na kukuomba wewe Mungu wetu.

(Kwa mnong’ono)

Tena tunakutolea ibada hii ya kiroho na isiyo ya kumwaga damu, na tunakuuliza, tunakuomba na kukusihi kwa unyenyekevu; utume Roho wako Mtakatifu juu yetu na juu ya vipaji hivi vilivyowekwa mbele yetu.

Ee Padri, bariki mkate mtakatifu.

(†) Na ufanye mkate huu kuwa Mwili mtakatifu wa Kristo wako.

( Amina. )

Ee Padri, bariki Kikombe Kitakatifu.

(†) Na iliyo ndani ya kikombe hiki kuwa Damu takatifu ya Kristo wako.

( Amina. )

Ee Padri, bariki vitakatifu vyote viwili.

(†) Kwa kuvibadilisha kupitia Roho wako Mtakatifu.

( Amina, Amina, Amina. )

Ili viwaletee wanaovipokea mkesha wa roho, maondoleo ya dhambi, ushirika na Roho wako Mtakatifu, ukamilifu wa ufalme wa mbinguni, uthabiti mbele yako, lakini visiwe kwa lawama au hukumu. Tena tunakuletea ibada hii ya kiroho kwa ajili yao waliolala katika imani, Mababu, Mapadri, Mapatriaka, Manabii, Mitume, Wahubiri, Wainjili, Mashahidi, Waungama, Watawa, Walimu na kwa roho ya kila mwenye haki aliyekamilika katika imani.

Kasisi

Kasisi (Kwa mnong’ono)

Askofu wetu mkuu (jina)

Watu:

Bwana, hurumia.

Shemasi

Watu:

Kasisi (Kwa mnong’ono)

Kasisi

Watu:

Amina.

Kasisi

Watu:

Shemasi

( Bwana, hurumia. )

( Bwana, hurumia. )

( Bwana, hurumia. )

( Kwako. Ee Bwana. )

Kasisi (Kwa mnong’ono)

Kasisi

Watu

Kasisi

( Amina. )

Kasisi

Amani kwa wote.

( Na iwe rohoni mwako. )

Shemasi

( Kwako. Ee Bwana. )

Kasisi (Kwa mnong’ono)

Kasisi

( Amina. )

Kasisi (Kwa mnong’ono)

Ee Mungu, uniwie radhi mimi mtu mwenye dhambi na unihurumie.

Shemasi

Tusikilize.

Kasisi

Watu:

Watu:


Shemasi (Kwa mnong’ono)

Kasisi

Shemasi

Kasisi

Shemasi (Kwa mnong’ono)

Amina.

Kasisi

Shemasi

Kasisi

Shemasi

Kasisi

Shemasi

Kasisi

Shemasi

Watu

Watu:

Kasisi

Watu:

Sauti ya Pili.

Shemasi

Kasisi

Kasisi

( Amina. )

Watu:

Shemasi

( Bwana, hurumia. )

( Utukufu kwako Ee Bwana, utukufu kwako. )

Utusaidie, utuokoe, utuhurumie, na utuhifadhi, Ee Mungu, kwa neema yako.

( Bwana, hurumia. )

( Kwako. Ee Bwana. )

Kasisi (Kwa mnong’ono)

Kasisi

( Amina. )

Kasisi

Watu:

Shemasi

Tumwombe Bwana.

( Bwana, hurumia. )

Kasisi

( Amina. )

Watu:

Kasisi (Kwa mnong’ono)

Shemasi

Tumwombe Bwana.

( Bwana, hurumia. )

Kasisi

( Amina. )

Watu

Utukufu kwa Baba na Mwana na Roho Mtakatifu, sasa na siku zote hata milele na milele. Amina.

Kasisi

Watu:

Kasisi

( Amina. )

Kasisi

Watu: