×




SAKRAMENTI YA UBATIZO

KASISI

Kwa jina lako, Ee Bwana Mungu wa ukweli na kwa mwana wako wa pekee na kwa Rohob wako mtakatifu, ninaweke|ea mkono wangu kwa mtumishi wako (J) ambaye amestahilika kutafuta ulinzi kwa jina lako takatifu, na kulindwa chini ya uvuli wa bawa zako. Mwondolee dhambi za kale na umjaze na imani yako, tumaini na upendo ili aweze kujua kuwa wewe tu ndiwe Mungu wa kweli.wewe na Mwana wako wa pekee, Bwana wetu Yesu Kristo na Roho mtakatifumjaIie kuishi kulingana na amri zako zote na kufanya mambo ambayo yanakupendeza. Kwa kuwa kila anayefanya mambo haya atapata uhai.andika jina lake katika kitabu chako cha uzima na umuunganishe pamoja na kondoo wa urithi wako; jina lako takatifu na Iile la Mwana wako mpendwa Bwana wetu Yesu Kristo,na ya Roho wako mpaji wa uhai utukuzwe ndani yake.macho yako yamlinde kila mara katika rehema, kila mara masikio yako yasikie sauti za maombi yake.mfanye afurahie katika kazi ya mikono yake na katika kizazi chake ili aweze kutoa shukrani kwako, kwa kuabudu na kutukuza jina lako kuu, na Kila mara akusifu siku zote za maisha yake.

Kwa kuwa kila nguvu ya mbinguni inaimba sifa zako na utukufu wote ni wako, wa Baba, na Mwana na Roho mtakatifu daima sasa na siku zote hata milele na mi|ele.

KUMFUKUZA SHETANI MARA YA KWANZA

SHEMASI

Tumwombe Bwana.

( Bwana, hurumia. )

KASISI

Bwana anakukataza ewe shetani, kwa kuwa alikuja duniani na kukaa pamoja na wanadamuili kumaliza ufalme wako na kumfanya mwanadamu huru;kwa kuwekwa msalabani, alishinda nguvu zote ovu ,jua Iilipokuwa giza na dunia kutikiswa makaburi yalipofunguka na miili ya watakatifu ilipaa; Aliangamiza kifo kwa kifo na alikushinda, ewe shetani uliyekuwa na nguvu za kifo, ninakushurutisha kwa jina la Mungu aliyedhihirisha mti wa uzima na kuweka waheruvi na panga zenye moto inayokata pande zote kuuliinda.Ushindwe na uondoke; kwa kuwa ninakuamuru kwa jina la Yule aliyetembea juu ya maji kama kwamba ilikuwa nchi kavu,na kuleta utulivu; ambaye anakausha kisima na ambayetisho lake linayeyusha milima. Ndiye yule Bwana ambaye sasa anakuamuru kupitia kwetu: ogopa, toka na umwondokee huyu mwanadamu. (hawa wanadamu), na usiwahi kurudi, kujificha ndani yake (yao) wala kukutana au kujionyesha kwake. (kwao); usiku wala mchana, asubuhi au adhuhuri, lakini ondoka kwa giza lako hadi siku ile kuu ya hukumu.mwogope Mungu aketiye juu ya waheruvi; ambaye Malaika wanatetemeka, malaika wakuu, Enzi, mfalme, Hila, Mamlaka, Nguvu na waheruvi na waserafi wenye macho mengi na mabawa sita ambaye mbingu,nchi, bahari na vyote vilivyomo vinatetemeka. Toka na umwondokee mwanajesehi huyu. (wanajeshi hawa) wa Kristo Mungu wetu, kwa kuwa ametiwa alama ya Msalaba na ameorodheshwa upya. kwa kuwa ni kwa jina lake ninakuamuru, jina la Bwana ambaye anatembea kwa bawa za upepo, ambaye anawafanya malaika wake roho na watumishi wake moto, toka na umwondokee mwanadamu huyu (wanadamu hawa) na nguvu zako zote na malaika wako.kwa jina la Baba la Mwana na Roho mtakatifu Iinatukuzwa sasa na siku zote milele na hata milele.

( Amina. )

KUMFUKUZA SHETANI MARA YA PILI

SHEMASI

Tumwombe Bwana.

( Bwana, hurumia. )

KASISI

Mungu mtakatifu, unayetisha, mtukufu, usiyeelezeka na usiyechunguzika kwa kazi na nguvu zako zote,aliyekutwalia ewe Shetani, adhabu ya milele kupitia kwetu sisi watumishi wasiostahili, tunakuamuru, na kwa nguvu zote zinazofanya kazi na wewe, kumwondokea ambaye amewekewa nembo mpya' kwa jina la la Bwaria Yesu Kristo, Mungu wetu wa kweIi.kwa hivyo, ninakuamuru wewe muovu,uliyeharamishwa, mkatili na roho mbaya imutoke mtu huyu na usiwahi kumuingia tena. ondoka, na ukubali kuwa nguvu zako ni bure; ambazo hata hazingeweza kukaa ndani ya nguruwe. Mkumbuke aliyekuamuru kwa hiari yako kuingia ndani ya kundi la nguruwe. Mwogope Mungu ambaye kwa amri yake dunia ilifanywa dhabiti juu ya maji, ambaye aliziumba mbingu, aliyeipima milima kwa uzani na mabonde kwa mizani. (lsaya.4O:12) Aliyeweka mchanga kama mpaka wa bahari, na njia salama ndani ya maji;ambaye anaifanya milima itoe moshi kwa mguso wake, ambaye anajivisha nuru kama vazi, ambaye anafunika makao yake na maji; ambaye aliweka misingi ya dunia imara ili isiwahi kutikiswa; anayeinua maji kutoka baharini na kuirudisha kama mvua, toka na umwondokee anayejitayarisha kupata nuru takatifu. Ninakuamuru kwa uokovu wa Bwana Yesu Kristo na Mwili wake mtakatifu na Damu na kurudi kwake kuzuri; kwa kuwa atarudi bila kukawia kuhukumu dunia yote, na atakuweka na nguvu zote zinazofanya kazi nawe katika moto wa Jehanamu kwa kukukutoa kwa giza la nje ambako wadudu wanashambulia kila mara na moto hauzimiki kamwe. kwa kuwa nguvu ni za Kristo Mungu wetu, pamoja na Baba na Roho mtakatifu sasa na siku zote hata milele na milele.

( Amina. )

KUMFUKUZA SHETANI MARA YA TATU

SHEMASI

Tumwombe Bwana.

( Bwana, hurumia. )

KASISI

Ee Bwana wa majeshi, Mungu wa Israeli anayeponya kila ugonjwa na kila unyonge, mwangalie mtumishi wako; tafuta, chunguza na umwondolee kazi zote za shetani waondoe roho wote wachafu na uwaangamize na utakase kazi ya mikono yako; mkanyage shetani chini ya miguu yake (yao) mpatie ushindijuu ya shetani na roho wake wachafu ili kwa kupokea rehema zako astahili kushiriki katika sakramenti zako za mbinguni na aweze kutoa utukufu kwako, Baba, Mwana na Roho mtakatifu sasa-na siku zote hata milele na milele.

( Amina. )

SHEMASI

Tumwombe Bwana.

( Bwana, hurumia. )

KASISI

Ee Bwana, ambaye kwa kweli uko hai, ambaye ulimwumba mwanadamu kwa mfano wako, na ukampa nguvu za maisha ya milele; na hukumwacha alipoanguka kwa dhambi, lakini ukatoa wokovu kwa ulimwengu kwa Kristo wako Kubali kiumbe huyu katika ufalme wako wa mbinguni, kwa kuwa umemkomboa kutoka kifungu cha adui.fungua macho ya fikira zake,ili nuru ya injili yako imwangazie.muwekee katika maisha yake malaika wa nuru atakaye mlinda kutokana na kila hila ya adui, kutoka kila kisa kibaya, kutokana na shetani wa mchana na ndoto baya.

Mwondolee kila ovu au roha mchafu anayejificha au kumfuata katika moyo wake. (3)

Roho wa makosa, roho wa maovu, roho wa kuabudu miungu, na témaa zote; roho wa uongo na uchafu wote ambao unaletwa na mafunzo ya shetani.na umfanye kondoo aliye kusudishwa katika kikundi cha Kristo wako, mshirika mheshimiwa wa kanisa lako, chombo kilichotakaswa, mwana wa nuru na mrithi wa ufalme wako; ili baada ya kuweka nembo bila unajisi na kuhifadhi vazi lake bila doa, atapokea Baraka za watakatifu katika ufalme wako.

Kwa neema, na rehema, na upendo wa wanadamu wa Mwana wako wa pekee, pamoja na wewe mhimidiwa, na Roho wako Mtakatifu kamili, mwema na mpaji wa uhai, sasa na siku zote, hata milele na milele.

( Amina. )

KASISI

Unamkataa shetani,? na kazi zake zote na ibada zake zote? na malaika wake wote? na hila zake zote?

ANAYEBATIZWA/MDHAMINI

Ndio

KASISI

Umemkataa shetani?

ANAYEBATIZWA/MDHAMINI

Ndio.

KASISI

Mtemeni mate

KASISI

Unaapa kuwa mwaminifu kwa Kristo?

ANAYEBATIZWA/MDHAMINI

Ndio

KASISI

Je, umeapa kuwa mwaminifu kwa Kristo?

ANAYEBATIZWA/MDHAMINI

Ndio

KASISI

Na unamwamini?

ANAYEBATIZWA/MDHAMINI

Ndio ninamwamini kama Mfalme na Mungu.

Nasadiki Mungu mmoja, Baba, Mwenyezi, mwumba wa Mbingu, na Nchi, hata vyote vilivyo onekana na visivyo onekana. Tena Bwana mmoja, Yesu Kristo, Mwana wa pekee wa Mungu, aliyezaliwa na Baba kabla ya wakati wowote. Nuru toka Nuru, Mungu kweli toka Mungu kweli, aliyezaliwa, hakuumbwa, aliye wa asili moja na Baba, kwa yeye vyote vilifanya. Aliyeshuka mbinguni kwa ajili yetu wanadamu na ya wokovu wetu, akapata mwili kwa Maria bikira na kwa Roho Mtakatifu, hata kuwa mtu. Aliye sulubiwa kwa ajili yetu wakati wa enzi ya Pontio Pilato, akateswa, akawekwa kaburini. Aliyefufuka siku ya tatu, kama Maandiko yanenavyo. Akapaa mbinguni ndipo anapokaa kuume kwa Baba. Atakaye kuja mara ya pili kwa utukufu kuwahukumu wa hai na wafu; na ufalme wake utakuwa bila mwisho. Tena nasadiki Roho Mtakatifu, yu Bwana, yu mpaji wa uhai; anayetoka kwa Baba, anayesujudiwa na kutukuzwa pamoja na Baba na Mwana, aliyenena kwa midomo ya manabii. Tena nasadiki Ekklesia Moja, Takatifu, Katholiki na la Mitume. Naungama ubatizo moja kwa maondoleo ya dhambi. Natumaini ufufuo wa wafu, hata uzima wa ulimwengu utakaokuja. [[SWA]] Amina.

Je, umeapa kuwa mwaminifu kwa Kristo?

ANAYEBATIZWA/MDHAMINI

Ndio

KASISI

Inameni chini tumwabudu

ANAYEBATIZWA/MDHAMINI

Nainama chini na kumwabudu Baba Mwana na Roho mtakatifu, utatu mtakatifu asiyetengwa.

KASISI

Ahimidiwe Mungu ambaye mapenzi yake ni kuwa wote wataokoka na kujua ukweli, sasa na siku zote hata milele na milele.

( Amina. )

SHEMASI

Tumwombe Bwana.

( Bwana, hurumia. )

KASISI

Ee Bwana, Mungu wetu mwite mtumishi wako (J) kwa nuru yako takatifu na umstahilishe katika zawadi hii kuu ya ubatizo mtakatifu.muondolee njia za zamani na umfanye upya katika uzima wa milele na umjaze na nguvu za Roho wako Mtakatifu pamoja na Kristo wako ili asiwe tena kuwa mwana wa mwili bali awe mwana wa ufalmne wako. Kupitia kwa mapenzi na neema za mwana wako wa pekee ambaye unatukuzwa pamoja na msalaba wako mtakatifu na mpaji wa uhai,sasa na siku zote hata milele na milele.

( Amina. )

IBADA YA UBATIZO

SHEMASI

Ee padri, himidi.

KASISI

Mhimidiwa ni Ufalme wa Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu, sasa na siku zote hata milele na milele.

( Amina. )

SHEMASI

Kwa amani, tumwombe Bwana.

( Bwana, hurumia. )

Kwa ajili ya amani kutoka juu na ya wokovu wa roho zetu, tumwombe Bwana.

( Bwana, hurumia. )

Kwa ajili ya amani ya dunia yote, na kusimama imara kwa Ekklesia Takatifu ya Mungu, na ya umoja wa wote, tumwombe Bwana.

( Bwana, hurumia. )

Kwa ajili ya nyumba hii takatifu na waingiamo kwa imani, heshima na kumcha Mungu, tumwombe Bwana.

( Bwana, hurumia. )

Kwa ajili ya Askofu wetu mkuu Askofu wetu mkuu (jina) Makasisi, Mashemasi wateule na watu wote tumwombe Bwana.

( Bwana, hurumia. )

Kwa ajili ya taifa letu (jina) na raisi wetu (jina), na viongozi wetu, na wa majeshi wapendao dini, tumwombe Bwana.

( Bwana, hurumia. )

ili maji haya yatakaswe kwa nguvu za Roho mtakatifu.tumwombe Bwana.

( Bwana, hurumia. )

ili neema ‘ya ukombozi na baraka za yorodanizijé ndani maji haya,tumwombe Bwana.

( Bwana, hurumia. )

ili nguvu za utakaso za Utatu mtakatifu zije juu ya maji haya.tumwombe Bwana.

( Bwana, hurumia. )

ili tupokee nuru na ujuzi na kumcha Mungu kupitia kwa Roho mtakatifu, tumwombe Bwana.

( Bwana, hurumia. )

ili maji haya yawe kinga dhidi ya kila hila za maadui wanaoonekana na wasioonekana, tumwombe Bwana.

( Bwana, hurumia. )

ili ambaye anabatizwa awe wakustahilika katika ufalme usio na doa.tumwombe Bwana.

( Bwana, hurumia. )

kwa yeye ajaye kwa nuru takatifu na kwa wokovu, tumwombe Bwana.

( Bwana, hurumia. )

ili afanywe mwana wa nuru na mrithi wa Baraka za mileIe.Tumwombe Bwana.

( Bwana, hurumia. )

ili awe mshiriki katika kifo na ufufuo wa Kristo Mungu wetu.Tumwombe Bwana.

( Bwana, hurumia. )

ili aweze kuhifadhi vazi lake la ubatizo na ahadi za roho bila doa na lawama katika siku ya Kristo Mungu wetu, tumwombe Bwana.

( Bwana, hurumia. )

Ili maji haya yawe usafisho kwa maondoleo ya dhambina vazi lisilo na doa.tumwombe Bwana.

( Bwana, hurumia. )

Ili Bwana Mungu aweze kusikia sauti ya maombi yetu.tumwombe Bwana.

( Bwana, hurumia. )

Ili yeye na sisi sote tuwezae kukombolewa kutika kwa taabu ,hasira,hatari na matakwa, tumwombe Bwana.

( Bwana, hurumia. )

Utusaidie, utuokoe, utuhurumie, utuhifadhi, Ee Mungu, kwa neema yako.

( Bwana, hurumia. )

Tumkumbuke Maria Mtakatifu kamili, asiye na doa, Mbarikiwa zaidi kushinda wote, Bibi wetu mtukufu mzazi Mungu na bikira daima pamoja na watakatifu wote hata sisi pia wenyewe na kila mmoja wetu na wenzetu wote, hata maisha yetu, kujiweka mikononi mwa Kristo Mungu.

( Kwako, Ee Bwana. )

KASISI

Ee Mungu wa upendo na mrahimu, ambaye unachunguza mioyo yetu na hisia zetu ,ambaye wewe pekee unajua siri zetu sote, kwa kuwa hakuna’chochote unawéza kufichwa lakini kila kitu ni wazi na kinadhihirishwa machohi mwako; unayenijua; usinidharau wala kuniondolea uso wako ambaye unona dhambi za wanaume na wanawake ;na kuwaongoza katika kutubu; safisha uchafu wote wa mwili wangu na doa za moyo wangu na unitakase kwa nguvu zako zisizoonekana na uwezo wa roho wakoi ninapotangaza uhuru kwa wengine na kufanyiza ibada hii kwa imani yote katika upendo mkuu kwa mwanadamu, nisikatiliwe kama mtumishi wa dhambi. Ee, Bwana, ambaye wewe tu ndiwe mwenye haki na mpenda Mwanadamu.usinirudishe kwa dharau na aibu lakini unitumie nguvu kutoka juu na unipe nguvu za kufanyiza hii sakramenti yako kuu. Fanyiza mfano wa Kristo ndani huyu ambaye anazaliwa upya ndani yangu kwa kutostahili kwangu, Mjenge katika misingi ya mitume wako na manabm usimwangushe chini ,lakini muweke kama mmea wa ukweli katika kanisa lako la katholiki na Ia mitume, na usiwahi kumng’oa ili anapokua kwa kukucha aweze kutukuza jina lako kuu na takatifu la Baba na Mwana na Roho mtakatifu, daima sasa na siku zote hata milele na milele. Amina.

KASISI

Ewe Mungu ni mkuu na kazi zako ni za ajabu, hakuna maneno yanayotosha kusifu ukuu Wako. (3)

Kwa kuwa wewe kwa mapenzi yako ulifanya vyote vilivyo hai toka bure kuwa hai: kwa nguvu zako umeshikilia viumbe, na kwa kujitolea kwako unatawala u|imwengu.kwa kufanya vyote uliutimiza mwaka na misimu»mine, nguvu zote za kiroho zinasimama mbele za ukuu wako, jua linakusifu, mwezi unakutukuza, nyota zinazungumiza na wewe, mwangaza unakutii mabonde yanatetemeka mbele zako, visima vya maji vinakutumikia.umetandaza mbingu kama pazia, umetega dunia juu ya maji ,umeizingira bahari na nichanga umetoa hewa ya kupumua.nguvu za malaika zinakuhudumia kwaya za malaika wakuu zinakuabudu viumbe wenye macho mengi makeruvi na wenye mabawa sita waserafi wanakuzungukia na kupepea mbele zako na kufunika nyuso zao mbele ya utukufu wako mkuu.kwa kuwa wewe Mungu wetu usiyeelezeka ,usiye na mwanzo usiyeneneka ulikuja duniani ukiwa kama mtumishi ,ulifanana na mwanadamu.kwa huruma zako kubwa, Bwana hungeweza kustahimili kuona wanadamu chini ya mamlaka ya shetani,lakini ulikuja na ukatuokoa .tunatambua neema zako,tunakiri huruma zako hatufichi uzuri wako.umefanya vizazi vyote vijavyo kuwa huru. ulitakasa tumbo la bikira kupitia kuzaliwa kwako na viumbe vyote vilisifu kuja kwako .kwa kuwa wewe Mungu wetu ulukuja duniani ulikaa na wanadamu ,ulitakasa maji ya yorodani kwa kumtuma Roho wako mtakatifu toka mbinguni na kwa kufanya hivyo ulivunja nguvu zote ovu zilizokuwa pale.

Kwa hivyo Ee mfalme mpenda wanadamu, kuja sasa kupitia Roho wako mtakatifu na uyatakase maji haya (3)

Na uyajaze na neema za uponyaji, Baraka za yorodani.ifanye chemichemi bora, kipawa cha utakaso, Yaondoe dhambi, yalinde kutokana na unyonge, yaondoe mapepo, yasiwe a nguvu ovu, yajazwe na nguvu za malaika.Wacha wanaomwazia kiumbe wako maovu wayatoroke, kwa kuwa nimeliita Jina Iako Ee Bwana wa ajabu na mtakatifu uliyemmbaya kwa maadui zako.

Wacha nguvu zote ovu ziangamizwe kwa kufanywa kwa ishara ya msalaba wako wenye thamani. (3)

Wacha mapepo yote ya angani yaondoke mbali nasi pepo yoyote ya giza isijifiche ndani ya maji haya. Ee Bwana pepo yoyote mbaya isilete roho wa kuchanganyikiwa kwa akili au usumbufu wa fikira umfikie huyu ambaye anataka kubatizwa lakini wewe Bwana wa vyote yafanye maji haya kuwa maji ya uponyaji, maji ya utakaso, kwa kuosha mwili na roho, kuondolewa kwa udhaifu, msamaha wa dhambi, kuangaziwa rohoni kusafishwa roho upya, kipawa cha kufanywa mwana vazi lisilo na doa, chemichemi ya uhai.kwa kuwa ni wewe Bwana uliyesema; jiosheni na muwe safi ondoeni maovu yote mioyoni mwenu.ulitupatia toka juu kuzaliwa upya katika maji na Roho. Jidhihirishe Ee Bwana ndani ya maji haya na umjalie anayebatizwa ndani yake aweze kubadilishwa ili kuacha mtu wa kale aliye na doa na tama mbaya na ajivike mtu wa sasa aliyebadilishwa katika mfano wa Mungu muumba, ili ajiunge pamoja nawe katika mfano wa kifo chako katika ubatizo ili awe mshiriki katika ufufuo wako.na baada ya kulinda kipawa cha Roho wako na kuvyongeza neema zako apokee tuzo la kuitwa katika Baraka zako za juu na ahesabiwe pamoja na wazao wako wa kwanza ambao majina yao yameandikwa mbinguni kwako wewe Mungu wetu na Bwana Yesu Kristo.

Na kwako tunatoa utukufu, nguvu, heshima na kukuabudu pamoja na Baba yako asiye na mwanzo na Roho wako mwema na mpaji wa uhai sasa na siku zote hata milala na milele.

( Amina. )

KASISI

Amani kwa wote.

( Na iwe kwa roho yako. )

SHEMASI

Tuinamishe vichwa vyetu kwa Bwana.

( Kwako, Ee Bwana. )

SHEMASI

Tumwombe Bwana.

( Bwana, hurumia. )

Ee Bwana, Mungu wa baba zetu uliyetuma njiwa kwa wale waliokuwa katika safina ya Nuhu akiwa amebeba tawi la zeti kinywani mwake kama ishara ya upatanishp na ukombozi kutoka kwa gharika ' Ambaye kwa ishara hizi ulionyesha neema, uliyetoa matunda ya zeti ili yatimize sakramenti zako takatifu na uliwajaza Roho mtakatifu wale waliokuwa chini ya sheria na kuwakamilisha waliokuwa chini ya neema.yabariki mafuta haya kwa nguvu na Roho mtakatifu ili yawe utakaso na silaha ya haki kufanywa upya kwa roho na mwili, kinga dhidi ya kila hila za shetani na kufanywa huru kutoka kwa maovu, kwa wale wote wanaotakaswa nayo kwa imani au wale wanayashiriki.

Kwa utukufu wako na wa mwana wako wa pekee na Roho wako mwema na mpaji wa uhai sasa na siku zote hata milele na milele.

( Amina. )

SHEMASI

Tusikilize.

WATU

Alleluia, Alleluia, a|leluia.

KASISI

Ahimidiwe Mungu anayeangazia na kutakasa kila mmoja ajaye duniani sasa na siku zote hata milele na milele.

( Amina. )

KASISI

Mtumishi wa Mungu (j) anapakwa mafuta ya furaha kwa jina la Baba na la Mwana na la Roho mtakatifu.

Kwa uponyaji wa roho na mwili.

Kusikia maneno ya imani.

Kutembea kwa nyayo zako.

Mikono yako iliniumba na kunitengeneza mimi.

Mtumishi wa Mungu (J) anabatizwa kwa jina la Baba.

( Amina. )

Na la Mwana.

( Amina. )

Na la Roho mtakatifu.

( Amina. )

(3)


Zaburi ya 31 (32).

Heri aliyesamehewa dhambi, na kusitiriwa makosa yake. [[SWA]] (3)

Heri BWANA asiyemhesabia upotovu, ambaye rohoni mwake hamna hila. Niliponyamaza mifupa yangu ilichakaa kwa kuugua kwangu mchana kutwa. Kwa maana mchana na usiku mkono wako ulinilemea. Jasho langu likakauka hata nikawa kama nchi kavu wakati wa kaskazi. Nalikujulisha dhambi yangu, wala sikuuficha upotovu wangu. Nalisema, Nitayakiri maasi yangu kwa BWANA, nawe ukanisamehe upotovu wa dhambi yangu. Kwa hiyo kila mtu mtauwa akuombe wakati unapopatikana. Hakika maji makuu yafurikapo, hayatamfikia yeye. Ndiwe sitara yangu, utanihifadhi na mateso, utanizungusha nyimbo za wokovu. Nitakufundisha na kukuonyesha njia utakayoiendea; nitakushauri, jicho langu likikutazama. Msiwe kama farasi wala nyumbu, walio hawana akili. Kwa matandiko ya lijamu na hartamu sharti kuwazuia hao, au hawatakukaribia. Naye mtu mwovu ana mapigo mengi, bali amtumainiye BWANA fadhili zitamzunguka. Mfurahieni BWANA, shangilieni, enyi wenye haki; pigeni vigelegele vya furaha; ninyi nyote mlio wanyofu wa moyo.

KASISI

Mtumishi wa Mungu anavikwa vazi la haki kwajina |aBaba na la Mwana na la Roho mtakatifu.

WATU

Watuznipe vazi jipya, Ewe unayejivika nuru kama vazi Ee Kristo Mungu wetu mwenye huruma. [[SWA]] (3)

SHEMASI

Tumwombe Bwana.

( Bwana, hurumia. )

Uinuliwe Ee Bwana Mungu Mwenyezi, chanzo cha baraka zote, jua la haki, ambaye uliangaza nuru ya wokovu kwa wale waliokuwa gizani kwa kujidhihirisha kwa mwana wako wa pekee na Mungu wetu,na ulitupatia hata kama hatukustahili, usafisho mtakatifu kupitia ubatizo mtakatifu na kutakaswa kwa mafuta ya uhai;ambaye kwa sasa umefurahia kumwangazia upya mtumishi wako kwa maji na roho kwa kumwondolea dhambi zaké zote za hiari na zisizo za hiari.Ee Bwana wa huruma na Mfalme wa yote mjalie pia na nembo ya Roho wako mtakatifu,mwenye nguvu na wa kubudu, na pia ushirika wa mwili na damu takatifu ya Kristo wako. Mlinde na utakaso wako; mshirikishe katika imani ya kiorthodoks umkomboe kutokana na yule mwovu na hila zake zote, kupitia wokovu wako. Linda nafsi yake vyema na kwa haki ili kwa kukufurahisha kwa kila neno na tendo aweze kuwa mwana na mrithi wa ufalme wako wa mbinguni.

( Amina. )

KASISI

Nembo ya Roho mtakatifu.

( Amina. )

WATU

Ninyi nyote mliobatizwa katika Kristo mmevaa Kristo. Alleluia. [[SWA]] (3)

Utukufu kwa Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu. Sasa na siku zote hata milele na milele. Amina.

mmevaa Kristo. Alleluia.

Ninyi nyote mliobatizwa katika Kristo mmevaa Kristo. Alleluia.

KASISI

Amani kwa wote.

( Na iwe kwa roho yako. )

Bwana ni nuru yangu na mwokozi wangu.

Mstari Bwana ni mlinzi wa maisha yangu.

SHEMASI

Hekima.

MSOMAJI

Somo kutoka kwa

SHEMASI

Tusikilize.

MSOMAJI

(6:3-11)

Ndugu zangu, sisi tuliobatizwa tukaungana na Kristo Yesu, tulibatizwa na kuungana na kifo chake. Tulipobatizwa tuliungana na kifo chake, tukazikwa pamoja naye, ili kama vile Kristo alivyofufuliwa kutoka wafu kwa kitendo kitukufu cha Baba, sisi pia tuweze kuishi maisha mapya. Maana, kama sisi tumeungana naye katika kufa kama yeye, vivyo hivyo tutaungana naye kwa kufufuliwa kutoka wafu kama yeye. Tunajua kwamba utu wetu wa kale ulisulubiwa pamoja na Kristo, ili hali ya dhambi iharibiwe, tusiwe tena watumwa wa dhambi. Kwa maana, mtu aliyekufa, amenasuliwa kutoka dhambi. Basi, ikiwa tumekufa pamoja na Kristo, tunaamini kwamba tutaishi pia pamoja naye. Maana, tunajua kwamba Kristo amekwisha fufuliwa kutoka wafu na hafi tena; kifo hakimtawali tena. Hivyo, kwa kuwa alikufa--mara moja tu--dhambi haina nguvu tena juu yake; na sasa anaishi maisha yake katika umoja na Mungu. Hali kadhalika nanyi lazima mjione kuwa mmekufa kuhusu dhambi, lakini kama mnaoishi katika umoja na Mungu kwa njia ya Kristo Yesu. [[SWA]]

KASISI

Amani kwako Ee Msomaji.

WATU

Na iwe kwa roho yako.

Alleluia, Alleluia, a|leluia. [[SWA]]

SHEMASI

Hekima. Simameni wima. tusikilize Evanjelio Takatifu.

KASISI

Amani kwa wote.

( Na iwe kwa roho yako. )

Injili Takatifu kama ilivyoandikwa na

( Utukufu kwako, Ee Bwana, utukufu kwako. )

SHEMASI

Tusikilize.

KASISI

(28:16-20)

Wakati huo, wale wanafunzi kumi na mmoja walikwenda Galilaya kwenye ule mlima aliowaagiza Yesu. Walipomwona wakamwabudu, ingawa wengine walikuwa na mashaka. Yesu akaja karibu, akawaambia, "Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani. Nendeni basi, mkawafanye watu wa mataifa yote wawe wanafunzi wangu, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na la Mwana, na la Roho Mtakatifu. Wafundisheni kushika maagizo yote niliyowapeni. Nami nipo pamoja nanyi siku zote; naam, mpaka mwisho wa nyakati." [[SWA]]

( Utukufu kwako, Ee Bwana, utukufu kwako. )

KASISI

Utuhurumie, Ee Mungu kadiri ya huruma yako kubwa, tunakuomba utusikilize na kutuhurumia.

( Bwana hurumia, Bwana hurumia, Bwana hurumia. )

Tena tunaomba kwa ajili ya huruma, maisha, amani, afya na wokovu kwa watumishi wako (j) Wazazi, wasimamizi, familia zao na wote walio hapa.

( Bwana hurumia, Bwana hurumia, Bwana hurumia. )

( Bwana hurumia, Bwana hurumia, Bwana hurumia. )

( Bwana hurumia, Bwana hurumia, Bwana hurumia. )

( Bwana hurumia, Bwana hurumia, Bwana hurumia. )

Kwa kuwa U Mungu Mwema na mpenda wanadamu, na kwako tunatoa Utukufu, kwa Baba na Mwana na Roho Mtakatifu, sasa na siku zote, hata milele na milele.

( Amina. )

Maombi ya kutakasa na uzima

Ee Bwana ambaye kupitia ubatizo mtakatifu umempa mtumishi wako ukombozi wa dhambi na umempa maisha mapya, pendezwa na umwangazie daima moyoni mwake na nuru yako, Linda imani yake isishambuliwe na adui linda vazi ambalo yamevaa Iisiwe na doa. Hifadhi nembo yake ya kiroho-isivunjike kwa neema yako na umwonyeshe huruma pamoja nasi kwa wingi wa huruma zako.

Kwa kuwa utukufu na nguvu ni kwa jina lako heshimiwa, la Baba na Mwana na Roho mtakatifu sasa na siku zote hata milele na milele.

( Amina. )

SHEMASI

Tumwombe Bwana.

( Bwana, hurumia. )

KASISI

Ee Bwana Mungu wetu ambaye kupitia kwa maji ulitoa nuru yako ya mbinguni kwa wale wanabatizwa, ambaye amemfanya upya mtumishi wako ambaye ameangaziwa kwa maji na roho na umempa msamaha wa dhambi zake za hiari na zisizo za hiari.wekelea mkono wako mkuu juu yake na umlinde kwa nguvu za uzuri wako, hifadhi kiapo chake na umstahilishe katika maisha ya milele na upendo wako mkuu.

Kwa kuwa wewe ndiwe utakaso wetu na kwako tunatoa utukufu kwa Baba na Mwana na Roho mtakatifu,sasa na siku zote hata milele na milele.

( Amina. )

KASISI

Tuinamishe vichwa vyetu kwa Bwana.

( Kwako, Ee Bwana. )

SHEMASI

Tumwombe Bwana.

( Bwana, hurumia. )

KASISI

Ambaye amekuvaa wewe, Kristo wetu na Mungu wetu pamoja nasi ameinamisha kichwa chake kwako; m|inde kila mara kama shujaa asiyeonekana dhidi ya shambulizi ambazo Zinaelekezwa kwake na kwetu. kwa taji lako lisilo na doa tutangaze kuwa washindi mwishoni.

Kwa kuwa wewe unatuhurumi na kutuokoa na kwako tunatoa utukufu pamoja na Baba yako asiye na mwanzo na Roho wako mtakatifu mwema na mpaji wa uhai, sasa na siku zote hata milele na milele.

( Amina. )

Ombi la kunyoa nywele

SHEMASI

Tumwombe Bwana.

( Bwana, hurumia. )

KASISI

Ee Bwana Mungu wetu ambaye umewaheshimu wanadamu na mfano wako, kwa kuwafanyia nafsi kamilifu na mwili ambao unalingana na mahitaji yao ili mwili utumikie nafsi ambaye umeweka kichwa juu na kukitia hisia nyingi ili zisihitilafiane ambaye umefunika kichwa na nywele ili kisidhuriwe na mabadiliko ya anga, ambaye umepanga sehemu zetu zote kwa njia ya manufaa ili kwa yote tunatoa shukurani kwako. Ambaye kupitia kwa chombo chako kiteule, Paulo mtume umetuambia tufanye mambo yote kwa ajili ya utukufu wako Ee Bwana bariki mtumishi wako (J) ambaye amekuja kutoa sadaka yake ya kwanza kwa kunyoa nywele za kichwa chake, na umbariki msimamizi wake na uwajalie kufanya kila kitu kulingana na sheria zako na kufanya chochote kile kinapendeza machoni mwako.

Kwa kuwa wewe ni Mungu mrahimu na mpenda wanadamu na kwako tunatoa utukufu kwa Baba na Mwana na Roho mtakatifu, sasa na siku zote hata milele na milele.

( Amina. )

KASISI

Amani kwa wote.

( Na iwe kwa roho yako. )

SHEMASI

Tuinamishe vichwa vyetu kwa Bwana.

( Kwako, Ee Bwana. )

Tumwombe Bwana.

( Bwana, hurumia. )

KASISI

Ee Mungu wetu, ambaye kwa ujazo wa maji, kwa uzuri wako umetakasa wale wote wanaokuamini mbariki mtoto huyu (watoto hawa), mtumishi (watumishi) wako ambaye yuko hapa na Baraka zako zimshukie juu ya kichwa chake.na kama vile ulimbariki Daudi mfalme kupitia nabii wako samueli ,bariki pia kichwa cha mtumishi wako (J) kwa mkono wangu,mimi mwenye dhambi kwa kumtembelea na Roho wako mtakatifu ili akue kwa miaka na afikie umri mzee, atatoa utiikufu kwako naumjalie na Baraka zote za Yerusalemu siku zote za maisha yake.

Na kwako tunatoa utukufu kwa Baba na Mwana na Roho mtakatifu, sasa na siku zote hata milele na milele.

( Amina. )

SHEMASI

Utuhurumie, Ee Mungu kadiri ya huruma yako kubwa, tunakuomba utusikilize na kutuhurumia.

( Bwana hurumia, Bwana hurumia, Bwana hurumia. )

Kwa kuwa wewe ni Mungu mrahimu na mpenda wanadamu na kwako tunatoa utukufu kwa Baba na Mwana na Roho mtakatifu, sasa na siku zote hata milele na milele.

KASISI

Kwa kuwa wewe ni Mungu mrahimu na mpenda wanadamu na kwako tunatoa utukufu kwa Baba na Mwana na Roho mtakatifu, sasa na siku zote hata milele na milele.

( Amina. )

KUMALIZIA

KASISI

Utukufu kwako, Ee Kristo Mungu wetu na matumaini yetu, utukufu kwako.

MSOMAJI

Utukufu. Sasa. Bwana hurumia, Bwana hurumia, Bwana hurumia.

KASISI

Aliyekubali kubatizwa katika Yorodani na Yohanna kwa wokovu wetu, Kristo Mungu wetu wa kweli, kwa maombi ya Mama yake asiye na doa na asiye na waa, mtakatifu kamili; ya nbii mtakatifu n mtangulizi Yohanna mbatizaji, ya Mitume watakatifu, watukufu na wasifiwa; ya watakatifu na wenye haki Yohakim na Anna; ambao majina yao yamepatiwa watoto hawa. ya mtakatifu (jina) (wa kanisa); na ya watakatifu wote, atuhurumie na atuokoe, yu Mungu mwema, mrahimu na mpenda wanadamu.

Kwa maombi ya mababa wetu watakatifu, Ee Bwana Yesu Kristo Mungu wetu, utuhurumie na utuokoe.

( Amina. )